Inaweza kuwa habari mbaya zaidi kwa watoto lakini kitaalamu inaonyesha kuwa uangaliaji
wa wa runinga kupita kiasi ni hatari kwa afya zao. Utafiti uliofanywa na chuo
kikuu cha McGill cha Canada unaonyesha kuwa uangaliaji wa runinga na kompyuta
kwa zaidi ya saa mbili unaweza kumsababishia mtoto kupata shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa wataalamu hali hiyo usababishwa na kukaa kwa muda mrefu hivyo mwili kushindwa kufanya kazi yake
ipasavyo ikiwemo mzunguko wa damu.
“Mtoto anapokaa muda mrefu kwenye luninga
lazima atakuwa hapati muda wa kufanya mazoezi , kula vizuri na wakati mwingine
kupata mapumziko ya kutosha , hivyo anakuwa kwenye hatari ya kupata shinikizo
la damu, alisema mmoja wa washiriki wa utafiti huo,Dr. Ronald James . Utafiti
huo ulikwenda mbali zaidi na kuonyesha mtoto mwenye shinikizo la damu yupo
kwenye katika hatari zaidi ya kupatwa na maradhi ya moyo , maradhi ya figo na
kupooza.
Maoni 1 :
Duuh, sasa itakuwaje maana huku kwetu sasa ni dampo la vilivyoshindikana, au uchafu wa kutupwa
Chapisha Maoni