Alhamisi, Mei 15, 2014

NAMNA YA KUTUMIA MPAPAI KUJIKINGA NA HOMA YA DENGUE

Dalili za ugonjwa wa Dengue ni homa kuumwa kichwa, uchovu na maumivu ya viungo huanza kujitokeza  kuanzia kati ya siku tatu hadi 14 tangu mtu anapoambukizwa kirusi cha homa hii, Dalili nyingine ni kutokwa na damu kwenye fizi na puani na chini ya ngozi  na iwapo mgonjwa ataumia sehemu yeyote ya mwili  ni rahisi kupoteza damu  nyingi kupitia kwenye michubuko lakini wapo wanaopoteza fahamu wakati mwingine dalili zake hufanana na za malaria . Kutokana na kutokuwepo kwa tiba ya ugonjwa huu kwa nchi kama za Thailand, Malaysia na India wameweza kupata kinga na tiba kwa kutumia papai au majani ya mpapai. 
Wanasema ni vyema mtu akala papai pamoja na mbegu zake katika kumsaidia kujikinga na dengue. Unachukua majani mawili ya mpapai  na kuyasafisha vizuri kisha unayatwanga kwa kutumia kitambaa kisafi halafu unakamua kupata juisi yake ambayo huwa ni sawa na vijiko viwili vikubwa vya chakula. Ila kwa wale wenye blenda wanaweza kuyasaga majani hayo kwa mashine hiyo na kuchuja kupata juisi yake.Wataalamu wanatoa tahadhari kutokuchemsha, kupika au kusafisha na maji ya moto kwani itaondoa nguvu yake pia wanasema mtu atumie majani tu na si mizizi au shina. Juisi hiyo inaelezwa kuwa ni chungu sana hivyo unaweza kuinywa hivyohivyo au kuchanganya na asali kidogo. 

Chanzo cha kuonekana kuwa papai linasaidia ilikuwa ni mwanafunzi huko Malaysia kuugua ugonjwa huo na kupoteza damu nyingi. Hivyo rafiki wa baba yake alimpatia juisi ya papai alilosaga bila kumenya na baada ya sikumbili damu yake iliongezeka sana na kupata nafuu.Mbali na miujiza ya papai wataalamu wa afya wanashauri hatua nyingine za kuchukuliwa katika kujikinga na ugonjwa huo. Miongoni mwao nikumaliza mazalia ya mbu kwa kufunika madimbwi ya maji yaliyotuama  na kunyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwi vya mbu, kuondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalia ya mbu kama vifuu vya nazi, makopo, matairi ya magari yaliyotupwa ovyo.

 Pia kufyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu, kuhakikisha maua yaliyopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama, kufunika mashimo ya maji taka na kusafisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.Vilevile kutumia viuatilifu vya kufukuza mbu, kuvaa nguo ndefu na zenye rangi ya uangavu , kutumia vyandarua vilivyosindikwa  viuatilifu na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi. Kujikinga na homa ya dengue ni rahisi iwapo kila mtu atakuwa makini kumzuia mbu asimuume kwa kuweka mazingira safi na kutekeleza njia zote za kumzuia.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom