Pages

Jumamosi, Mei 24, 2014

UJUMBE WA LEO "ELIMU NI ZAIDI YA KUKAA DARASANI"

Katika maisha unaweza kuwa na elimu na vyeti vizuri lakini kama haujimbui haitakusaidia chochote. Elimu zaidi baada Unaambiwa vyeti vinazalisha jamii isiyoelimika kwa kuwa wengi huamini kwa kumaliza shahada au elimu nyingine, hawezi kuendelea kufundishwa, wakati ukweli ni kwamba kuna elimu zaidi ya kukaa darasani nayo ni kujitambua.

 "Kila kitu katika maisha yako kinaweza kubadilika ndani ya dakika moja. Ni pale utakaposema basi kwa unachohisi kinakurudisha  nyuma na kuchukua hatua moja mbele, Unafanya kazi lakini huifurahii, unasomea fani kwasababu wazazi wamekuchagulia, unamng'ang'ania mpenzi  kwasababu ukiachana naye watu watacheka, hayo ni maisha ya motoni unaungua ndani yako kwasababu unaogopa kuchukua hatua itakavyobadilisha mkondo uliopo sasa. 

Dakika utakayotumia kuchukua njia nyingine , ndiyo itakayobadilisha kila kitu katika maisha yako, Mabadiliko ni magumu lakini ndiyo njia pekee ambayo watu wengi waliofanikiwa walichukua. NA JULIETH KULANGWA.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom