Pages

Jumanne, Mei 13, 2014

Ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete kuhusu Ugonjwa Wa Dengue Kuitikisa Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete amewaomba Watanzania kwenda kwenye Hospitali na vituo vya afya kupima afya zao wakati wanapopata dalili za malaria ili kujua kama ni homa hiyo ili wapatiwe matibabu sahihi. Aidha ameagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha inasambaza vifaaa vya kupimia ugonjwa huo nchi nzima ili kutoa huduma haraka kwa waathirika. Alitoa kauli hiyo jana jijini Arusha, wakati alipokuwa akizungumza na wauguzi katika maadhimisho ya wauuguzi duniani ambayo kitaifa ilifanyika jijini Arusha.


 Amesema Ugonjwa huo kwasasa ni tishio nchini kwani kwa mara ya kwanza uliibuka mwaka 2010 na watu 30 walipata matibabu, lakini umeibuka tena january mwaka huu na kwamba hadi mwezi huu 369 wameugua na kati yao wawili wamepoteza maisha. 

"Watanzania wengi tumezoea tunaposikia dalili za homa kama malaria, tunaenda kununua dawa za malaria, lakini sasa haifai kabisa kwasababu unaweza kununua ya malaria kumbe ni Dengue. Amesema wilaya inayoongoza ni Kinondoni ambayo inawagonjwa 322, ilala 61 na temeke 16. Alisema vifaa hivyo ni vichache, hivyo ni vizuri MSD ikasambaza vifaa hivyo pamoja na dawa ili kupambana na janga hilo.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom