Alhamisi, Juni 05, 2014

Tukio la mtoto wa Boksi liwe fundisho kwa jamii "Wazazi na walezi kamili hawahitaji kukumbushwa juu ya umuhimu wa malezi bora"

Mama huyu ndiye alikuwa mama mlezi wa Mtoto Nasra ambaye anashikiliwa na polisi
Ikiwa zimepita siku chache toke Mtoto Nasra apoteze maisha,  ikiwa ni baada ya miaka minne yamateso makubwa katika uhai wake. Ni mtoto aliyewekwa ndani ya chumba akifungiwa kwenye boksi ambalo ndio lilikuwa chumba cha maakuli, bafu na choo chake.

Vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi wamekuwa wakiripoti taarifa za maendeleo ya mtoto huyu hadi kufikia kifo chake juni 1 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam. Jamii inatakiwa kukumbuka mtoto tangu akiwa tumboni mwa mama yake siyo tu ni wa wazazi husika wa ujauzito huo pekee bali ni wa wote na kila mmoja katika jamii anapaswa kumlinda mtoto huyo hadi atakapozaliwa na kutunzwa,kusomeshwa na hatimaye aweze kujitegemea kulitumikia taifa lake.

Ni wajibu wa kisheria wa wazazi kuwapatia matunzo sahihi na bora watoto wao tangu wakiwa tumboni kwa mama zao hadi kufikia umri wa miaka 18 ambapo ndipo hutambulika kuw ni mtu mzima na hata baada ya umri huo wajibu wa malezi huendelea hadi watakapojitegemea kwa maana ya kuweza kuendesha maisha yao. WAZAZI NA WALEZI KAMILI WOTE HAWAHITAJI KUKUMBUSHWA UMUHIMU HUO iwapo watajisahau basi mkondo wa sheria upo wazi kuwakumbusha wajibu wao.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom