Pages

Jumanne, Juni 10, 2014

Wapenzi wa simulizi ya BADO MIMIusikose kuisoma hapa na soon utapata kitabu chake

Najua mliikosa sana, jikumbushe ilipoishia na sasa utaendelea kupata mambo mazuri.

Ilipoishia:...Baadaye Charito alirudi na nilimsimulia hali halisi na kile alichokiona Tumaini. Alibaki akiwa anashangaa "Haiwezekani mmmh mambo gani haya itabidi tuende kuonana na mchungaji" Alisema Charito huku akiwa ananitizama.Tulikubaliana ni vyema kwenda kuonana na Mchungaji Mkombozi ili aweze kutusaidia. Binafsi nilikuwa na hofu zaidi kutokana na  ujauzito niliokuwa nao. Baada ya mwezi mmoja tukiwa tunaendelea na maisha. Siku moja mume wangu alikuja akiwa amebeba chupa ya juisi amabapo alifika na kunimiminia kwenye kikombe kisha alinipa "Mke wangu hii juisi ni nzuri sana  kwa hali yako kwani inasaidia kuongeza damu mwili, si unajua, Mama mjamzito anatakiwa kuwa na damu nyingi"Charito alizungumza huku akitabasamu.Nilikunywa ile juisi yote ilikuwa na harufu nzuri sana ya zabibu. Kila siku Charito alikuwa akiniletea juisi.


Ilipita kama wiki moja, siku hiyo nilikuwa nimepumzika peke yangu, huku nikiwa natizama tamthilia. Ghafla tumbo lilianza kuniuma sana "Mama yangu, uwiiii, aaaah aaaah , Mamaaaaa, mbona tumbo linauma hivi. Eeeh Mungu wangu, maumivu yanzidi." Yaani nilikuwa nasikia maumivu makali sana, pale nyumbani kulikuwa hakuna mtu zaidi ya mdogo wangu Renata. Maumivu yalinizidi hatimaye damu zikaanza kunitoka kwa wingi, niliogopa huku nikilia kwa uchungu. Renata alikuja na kunishika huku akipiga kelele kuomba msaada. Majirani walikuja na kunibeba haraka kunikimbiza hospitalini. JE ...NINI KITAENDELEA USIKOSE...SEHEMU YA ...29...
 INAKUJIA SOON TUENDELEE KUWA PAMOJA

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom