Jumanne, Julai 01, 2014

HONGERA TCRA KWA KUPATA CHETI CHA UBORA KIMATAIFA


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhiwa cheti cha kuwa wafanyakazi bora kwa kiwango cha kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.


Cheti  hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam jana, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa Kimataifa kutoka Uingereza, Andrew Rowe, kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Mkoma (pichani).

Mkoma alisema kinatokana  na ubora wa kazi uliotambulika kimataifa na ambao unatokana na juhudi za wafanyakazi wa mamlaka hiyo na kwamba wataendelea kutoa huduma bora ili kuendelea kupata cheti hicho.

“Cheti tulichopata leo chenye namba ISO 900:2008 ni kutokana na juhudi za wafanyakazi wote wa TCRA za kuhakikisha tunatoa huduma bora zinazokidhi haja za wateja wetu. Tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti hicho ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma.

Akizungumzia cheti hicho,  TCRA, Mhandisi  kutoka Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Salvatory Rusimbi, alisema kinatokana na viwango bora vya kazi, uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali zinazo tumika kunufaisha utendaji kazi.

“Mkaguzi wa kimataifa amekuja hapa kutoka nchini Uingereza kutoa cheti hicho cha kiwango kinachotokana na  utendaji bora wa kimataifa ambao pia unawanufaisha wateja na utendaji wa mamlaka hii, hii inaonyesha wazi kuwa utendaji kazi wa TCRA  ni bora zaidi,” alisema Rusimbi.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom