Jumanne, Julai 15, 2014

SOMA HII KWA UMAKINI "SIYO KILA JAMBO NI LA KUULIZA"


Usimuulize yatima:
Babako alikufa vipi au mamako alikufaje?
Na usiwaulize wazazi:
Mtoto wenu alikufaje?
Na usimuulize mtu asiye na kazi, mbele za watu:
Wewe kwanini hufanyi kazi?
Usimcheke mwenye watoto mabadhuli hujuwi wakakwo watakuaje
Na usimuulize maskini:
Wataka pesa? Mpe bila ya kumuuliza, hivi ni kumkirimu khasa akiwa ataonana nawe mara kwa mara.
Na usimuulize mwanamke asiyezaa:
Wewe huna watoto?
Na usimuulize ambaye ana alama usoni sababu yake! Kwani uso ni sehemu ya utukufu.
Na usimcheke kilema kwani hakuomba kumbuka hujafa hujaumbika
Na usimuulize mgeni:
Unataka chakula? Au kinywaji? Mpe bila ya kumuuliza, ukimuuliza unamnyima.
Na usimuulize mwanamwali sababu ya kuchelewa kuolewa.
Wala Usimuilize mwanamke kwanini umekubali kuolewa ktk ukewenza asije mmeo akaoa kesho
Usije ukamuuliza mtu kwanini umeo zaidi ya mmoja
Na usijaribu kumfanyia stihzai rafiki kwa ajili ya kutaka kufurahisha wengine..kwani inamuumiza sana!
Daima jiweke mahala pa mpokezi na ujaribu kuhisi hisia zake♡ !
"Mkono kwa mkono hadi peponi" KUTOKA FACEBOOK

Maoni 1 :

emu-three alisema ...

Tupo pamoja

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom