Ijumaa, Julai 18, 2014

UZEMBE KATIKA BAADHI YA VITUO VYA AFYA NI MOJA YA CHANZO CHA VIFO VYA KINA MAMA WAJAWAZITO, "Masikini Mama Huyu"

Mwanamke mmoja nchini India ametoa shutuma kwa wauguzi wa Hospitali ya Royal Bolton akidai kuwa walimpa ruhusa kurudi nyumbani wakati akiwa katika hatua za mwisho za ujauzito wake, Zenat Patel (26) alidai kuwa muda mfupi baada ya kufika nyumbani alijifungua huku akisaidiwa na Mama yake mzazi licha ya Mama huyo kutokuwa na ujuzi wowote wa kuzalisha. 

Alisema muuguzi aliyempokea alipofika Hospitalini hapo alimtaka arudi nyumbani licha ya kumueleza anahisi maumivu yanayoashiria kujifungua kumewadia. Amesema "Hali niliyokuwa nayo ilieleza wazi kuwa muda mfupi ningejifungua lakini kila nilivyokuwa najaribu kuwaelezea hawakuonyesha kujali na kunitaka nirudi nyumbani. Alisema Patel.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom