ILIPOISHIA
MOJA: NADIA alifanya uchangudoa kumbe DES alimtimua? Alitoa wapi ujasiri huo.MBILI: Akalawitiwa akifanya uchangudoa….akaacha uchangudoa halafu??
TATU: JADIDA alimwongoza katika njia ipi sasa?
NNE: DES ana akili kweli yaani anamzushia mtu kuwa ana majini?? Vipi dua za Nadia zitamkumba Desmund??
INAPOENDELEA
Tulipofika hotelini sikuhitaji Nadia aseme neno
lolote la ziada maana hakika alikuwa amechoka, alikuwa Amelia haswa. Na alikuwa
na hasira.Mawazo aliyokuwa nayo hakika yalikuwa yakimtafuna
ndani kwa ndani. Nilijisikia vibaya kama vile alikuwa dada yangu wa kuzaliwa
tumbo moja.
Niliamini kuwa hata Nadia atakuwa amechoka na
atakuwa anahitaji kupumzika lakini sikuwa sahihi hata kidogo.
Tulipofika chumbani Nadia aliendelea kuzungumza,
sasa kwa hasira zaidi tofauti na wakati ule tulipokuwa nje.
“Japo nilihisi nimetengwa na kila kitu na dunia
ikiwa imenitukana kila aina ya tusi, naweza kukiri kuwa Jadida alikuwa mwanamke
ambaye alikuwa zaidi ya ndugu kwangu. Alinisimamia hadi dakika ya mwisho,
hakika niliujua umuhimu wake kiukweli lakini niliutambua vyema baada ya
kuhakikishiwa kuwa Jadida hatarudi tena alikuwa amekufa. Moja kwa moja!!
Nilibaki katika kile chumba alichokuwa akiishi na
wale machangudoa wengine.
Baada ya majuma mawili nikaanza kuombwa pesa ya
matumizi, ama la nitajua jinsi nitakavyokula mimi mwenyewe.
Mwandishi ujue tangu nilipoingiliwa kinyume na
maumbile sikutaka kabisa kujiingiza katika katika uchangudoa. Hata Jadida
alisema nisijiingize tena, yeye atajiuza name nitakula na kulala bila mashaka,
sasa hayupo tena watu wabaya walikuwa wamemuua, ni hapa nilipoanza kujiona
mkiwa tena na kisha kujiuliza hivi nilizaliwa kwa ajili ya kuteseka, nikamlilia
Mungu na kuona kwa hakika sikutakiwa kuendelea kuadhibiwa baada ya yote
niliyopitia.
Hata kama ilikuwa adhabu basi ilikuwa imetosha. Lakini Mungu
hapangiwi, nilibaki kunung’unika tu huku nikiendelea kuteseka. Baada ya
kunivumilia siku kadhaa hatimaye likafuata suala la kulipa kodi ya pango, hapa
sikuonewa huruma yoyote, nilitakiwa kuchangia pango.
Ningetoa wapi pesa na Jadi hakuwepo!! Nikaumiza
akili yangu sana kisha nikamkumbuka Ramadhani ama Ramso…” akasita kidogo, kisha
akanitazama kwa uchungu mkuu.
“Mwandishi yaani ni basi tu sina mtoto, ni basi tu
nasema sikuweza kuzaa lakini kama ningekuwa na kizazi nisingeweza kumwita mtoto
wangu jina hilo hata kidogo, yaani nisingeweza kumwita Rama nasema. Yaani basi
tu hatukupewa uwezo wa kujua lijalo nasema jambo hili kwa mara nyingine lakini
laiti tungewezeshwa kujua huenda ningeliepuka.
Na bado haya yote yalitokea kwa sababu tu Jadi
hakuwepo maana Rama alikuwa amenitongoza siku nyingi sana lakini sikuwahi
kumkubalia, naweza kukiri kuwa ule urembo wangu ulikuwa umeanza kuchepua tena
baada ya matunzo mazuri kutoka kwa Jadida na ilikuwa lazima wanaume waanze
kunitamani, kweli Rama akaanza kunitongoza mara kwa mara lakini Jadi
aliyesimama kama dada yangu alinikemea kabisa, lakini sasa Jadida amekufa.
Natakiwa kulipa kodi nikajikuta sina kimbilio zaidi ya Rama.
Nikamtafuta
mwenyewe na kumweleza kuwa nina shida na shilingi elfu tatu, alkanitazama kisha
akakumbushia lile lengo lake la awali kuhusu kunitaka kimapenzi. Nilijua lazima
tu atataka kitu hicho, nikajikuta katika maamuzi ya aina mbili tu nikose mahali
pa kulala nikalale stendi wahuni wanibake bila kunipa hata senti tano ama
nikubali kufanya mapenzi na Rama anipe hiyo pesa nikalipie pango niendelee
kulala sehemu ambayo walau kidogo ina usalama.
Tukakubaliana na Rama kuwa nitaenda kuchukua
nyumbani kwake, na sio nyumba bali ni chumba kikubwa. Majira ya saa tisa
sitasahau ilikuwa saa tisa na robo maana saa kilikuwa kitu cha kwanza kuangalia
baada ya kuingia katika chumba chake. Niliketi katika stuli iliyokuwa wazi, Rama
akaniuliza natumia kinywaji gani nikaagiza maji, nililetewa nikayanywa huku
nikijisikia aibu kuu, aibu kwa sababu nilikuwa pale kwa ajili ya kudhalilishwa.
Nadia mimi niliyeitunza bikira yangu hadi chuo kikuu leo hii nauza ngono. Nauza
nipate pesa ya kulipia chumba.
Niliumia sana kwa kweli, lakini wakati naumia
katika nafsi Rama alikuwa akiniita majina ya kimahaba ambayo hayakuwa na maana
kwangu, huwezi kuniita mpenzi mtu kama mimi ambaye nilijiona kama uchafu tu.
Alipotaka kunivutia kitandani nilimsihi kitu kimoja
kuwa nilikuwa nina njaa kali, hakika sikuwa namdanganya yaani baada ya kuwa
nimekula muhogo mmoja asubuhi hiyo sikuwa nimepata kitu chochote tena. Kweli
Rama alitoka nje na kisha akaingia na sahani ya wali nikauvamia na kwa fujo,
kisha nikashushia na maji. Sasa hapa niliweza kumridhisha Rama. Tukapanda
kitandani anifanye anachotaka.
Akafanya kweli huku nikimzuga kuwa ninafurahia
tendo lile. Lakini sikuwa pale hata kidogo.Rama akamaliza, nikadhani nimemaliza kulipa deni
lakini mara kutokea chini ya kitanda wakatokea wanaume wengine watatu ambao
naweza kuwaita wababe.Nikamuuliza Rama kulikoni akaanza kuniambia jambo
ambalo sikutarajia hata kidogo mwanaume anaweza kufanya hivyo.
Rama akadai kuwa nilijifanya mjanja sana kumkatalia
kimapenzi mapema, sasa nitamkoma yeye sio wa kuzungushwa hovyo. Nilijaribu
kujitetea huku nikimtupia lawama dada Jadida lakini haikusaidia, wale wanaume
wakaanza kuniingilia kwa zamu, nikiwa nimezibwa na kanga yangu mdomoni. Ramso
ameketi akivuta sigara huku akicheka, mwandishi sio siri niliumia mno,
nilijitahidi kuwahimili lakini walinizidi kwa nguvu, nikajikuta sasa nazizima!!
Nikaanza kuona maluweluwe tupu!!
Na bado niliwasikia wanaendelea kuniingilia……
Kabla sijapoteza fahamu kuna mabo niliyasikia
wakisemezana na sikujua yana maana gani maana ni kama nilikuwa nasikia kiarabu
na kihindi ikiwa lugha wanayotumia. Masikio yalisikia kama kengere kali sana
zikipigwa. Kisha kimya kikatanda…..kimya kikuu.
Nilikuja kushtuka usiku sana nikiwa kando kando ya
maji ya ziwa viktoria. Nilijaribu kusimama lakini nilianguka tena, nikajaribu
kupiga kelele lakini sauti haikuweza kutoka, nikaanza kujikongoja huku nikiwa
nimepatwa na hali fulani iliyonikumbusha jambo fulani, nilijaribu kupingana na
hali hiyo lakini ukweli ulikuwa huu huu ninaokueleza sasa. Rama akishirikiana
na washirika wake walikuwa wamenifanyisha mapenzi kinyume na maumbile. Nilizidi
kutambaa gizani, mara mbwa wakaanza kubweka.
Walibweka hasa kisha wakanifikia
nilipokuwa, mbwa mmoja akanisukuma chini na kuanza kunikwangua na makucha yake.
Nilijaribu kujitetea lakini haikuwezekana, mara akaongezeka mbwa mwingine huyu
alinivamia moja kwa moja na kuning’ata mkono wangu hapa (akajifunua mkono na
kunionyesha kovu). Nililia kwa nguvu mara akafika mmiliki wa hizo mbwa, huyu
alikuwa ni mlinzi. Akawafukuza wale mbwa. Akanimulika na tochi huku akiniuliza
mimi ni nani, wakati huo sikuwa na nguo mwili, mbwa walizigawana.
Labda hata hili lilikuwa tatizo lililonifanya
nizidi kuuchukia usiku ule mgumu kupindukia.
Yule mlinzi kijana alizima tochi yangu,
akanisogelea na kujifanya anataka kunisaidia, lakini na yeye akanifanya vibaya.
Alinibaka upesiupesi kisha akajiondokea, nilidhani ameondoka kweli lakini
haikuwa hivyo alikuwa ameenda kuwashirikisha na walinzi wengine wenye tamaa. Wawili wakanikuta nikiwa bado pale, mmoja aliomba
sana niachwe kama nilivyo lakini bahati mbaya hakuwa mbabe kuliko wenzake.
Mwenye nguvu akashinda nikabakwa tena. Kwa mara nyingine nikapoteza fahamu.
Nilikuja kushtuka alfajiri, bado sikuwa na nguo.
Lakini kabla sijajua nini cha kufanya mara akina mama wanaowahi katika biashara
zao asubuhi walinikuta nikiwa pale bila hili wala lile. Wakanipa msaada wa
kanga wakiamini mimi ni changudoa niliyepata ajali kazini.
Labda walikuwa sawa….lakini siamini kama nilizaliwa
kuwa changudoa.
Fadhaa ile ikanifanya nijikute katika maamuzi ya
aina yake, maamuzi ya kurejea Musoma kudai changu….ni lazima nipewe
changu…..ama la! Desmund anieleze kwanini aliamua kunitenda vile.
Sikuwa na la kupoteza kwa sasa, nikajikuta napoteza
rasmi tabasamu langu, bila shaka roho ya Jadida ilinivamia…..niaamua kurejea
Musoma kulisaka jibu la matatizo hayo. Maana haiwezekani yaani nimelawitiwa
kisa Desmund, nikabakwa tena na teana kisa yeye, halafu anaendelea kuyafurahia
maisha wakati mimi nadhalilishwa hapana Hapana mwandishi, mnyonge mnyongeni
lakini haki yake……” Nadia hakuweza kumalizia, akaingia katika kilio cha kwikwi.
“Usilie nadia, nipo kwa ajili yako kama
nilivyokwambia sawa!!” nilimweleza kwa sauti ya chini. Kisha nikamvuta na
kumkumbatia. Hapa sasa akaanza kulia kwa sauti ya juu kabisa. Kwa sababu hakuwa akiniona, nami uvumilivu
ukanishinda nikajikuta natokwa na chozi hadharani kwa mara ya kwanza tangu
nianze kuifuatilia simulizi hii ya Nadia.USIKOSE NINI KITAENDELEA.
Maoni 1 :
Maskin Nadia. Amekutana na changamoto za kikatili.
Chapisha Maoni