Ijumaa, Agosti 01, 2014

Wanaume wametakiwa kuwaunga mkono wanawake katika harakati za kupambana na ukatili wa kijinsia.


"Uhuru tulipigania wote, lakini sasa inashangaza kuona wakati huu wa kupigania haki za wanawake na kupinga ukatili tumebaki peke yetu, wanawake tumeteseka sana, wanawake wanauawa na kubakwa kila kukicha sasa ifike mwisho jamani, Serikali, viongozi wa dini na jamii iko wapi wakati wanawake wakiendelea kufanyiwa ukatili, lazima tufike wakati tusimame pamoja wanawake, wanaume na jamii kwa ujumla tukemee vitendo hivi."

Wito huo umetolewa na mwanaharakati Getrude Mongella wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake wa Africa jijini Dar es salaam jana.Maadhimisho hayo yaliratibiwa na shirika la Wanawake katika Sheria na maendeleo Africa (WILDAF).

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom