Pages

Alhamisi, Februari 05, 2015

UJUMBE WA LEO "Ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na mtu anayekufanya ujisikie mpweke"

Inaumiza sana unapojisikia mpweke wakati unajua kabisa nina mtu ambaye najua ni mwenza wangu ambaye angeweza kuwa na wewe katika mambo mbalimbali pale unapomuhitaji, sasa unakuta mtu upo naye lakini ni kama haupo naye kwani hakujali, kila kitu unakuwa wewe ndiyo wa kwanza kukifanya ama wakati mwingine kila siku wewe ndiyo unamkumbuka kutuma ujumbe ama kumpigia simu haijalishi una shida ama upo kwenye raha yeye anajifanya kama hakuoni  vile.

 Lakini pale atakapokuwa anakuhitaji basi utamuona ndiyo anakutafuta ukiona hali kama hiyo ujue hapo hakuna kitu yaani ni bora kuwa peke yako na kufikiria maisha mapya, unaambiwa mpende akupendaye asiyekupenda achana naye, mjali anayekujali na mthamini anayekuthamini.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom