Ahadi ya kuwa pamoja maishani katika
shida na raha,taabu na shida viapo hivi ama ahadi hizi zinaonekana
kuchukuliwa kirahisi mno na wanandoa wapya, lakini kwa muujibu wa
utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni unathibitisha kuwa ni rahisi mno
kutamka kuliko utekelezaji wa viapo vyenyewe .
Mtafiti uliofanywa
kwa wanandoa wenye bahati 2,700 waliooana umegundua kwamba ,ikiwa
mwanamke katika ndoa hiyo ataugua kwa muda mrefu asilimia sita hukaribia
kupewa talaka kuliko wale ambao wana afya njema .
Ukilinganaisha
na wanaume ambao huugua wakiwa kwenye ndoa,hatari ya kuvunjika kwa ndoa
ni ndogo mno,hatahivyo upendo huendelea hadi hapo mmoja wao atakapo baki
kuwa mgane ama mjane. Utafiti ulioongozwa na wanazuoni wa chuo
kikuu nchini Marekani,kinapendekeza kwamba kwa asili, wanawake wao
wameumbwa kutoa huduma katika familia zao nah ii inamaanisha kwamba
wanaume wao huwa hawana uvumilivu wake zao pindi wanapokumbwa na maradhi
ya muda mrefu ,ambayo pia yanweza kuwa hayatabiriki kuyakabili.
Walifanyiwa
utafiti wanandoa nchini Marekani,ambao wote walikuwa na umri wa miaka
50, mnamo mwaka 1990 ambao waliulizwa juu ya afya zao kuhusiana na
maisha yao wakichnugza kwa miaka miwili,miwili ndani ya utafiti
uliofanywa kwa miaka ishirini. Asilimia thelathini na mbili ya
ndoa ziliishia kwa kuachana na asilimia ishirini na nnenzilivunjika
kutokana na vifo vya mmoja wa wanandoa.
Kikosi cha utafiti
kiliongozwa na Amelia Karraker, ambaye ni profesa msaidizi juu ya
masuala ya maendeleo ya binaadamu na utafiti juu ya familia kutoka
katika chuo cha Iowa State University,analinganisha matukio ya namna nne
kansa,magonjwa ya moyo,kiharusi na magonjwa ya njia ya hewa kwa
wanawake na wanaume na matokeo ya ndoa.
Utafiti huo
umebainisha kwamba , kuna tofauti ya kujisikia mgonjwa sana na huwezi
kupika chakula cha jioni, ama unahitaji mtu hasa wa kukulisha masuala
haya yanaweza kubadili upepo ndani ya ndoa .
Katika hali
hiyo,utafiti huo hauoneshi dhahiri kuwa mume ama mke anadai
talaka,takwimu kamili zinaonesha kwamba wanawake ni wepesi zaidi kuomba
talaka kuliko wenza wao.
Bi Karraker anasema amegundua kwamba
kwamba inawezekana baadhi ya wanawake ambao huachwa kwasababu ya huduma
zao ama kushindwa kuhudumia
Tafakari juu ya Uhai ama kifo
husababisha watu wajitafiti wenyewe na kujiuliza maswali muhimu kuwa ni
nini muhimu maishani mwao? Anaeleza mtafiti huyo.
Wanawake wakati
mwingine huribuka kwa kusema kuwa waume zao hawawajali,na hawafurahishwi
na suala hilo ama husema sikufurahishwa na mwanzo wa mahusiano yao, na
wansema kwamba wako radhi kubaki peke yao kuliko kujitosa katika ndoa
isiyofaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni