Pages

Jumanne, Machi 24, 2015

LEO NI SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI (Ugonjwa unaowatesa watu masikini zaidi"


Kifua Kikuu ni nini
Kitaalamu, unaelezwa kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa.
Inaelezwa kuwa mtu menye vijidudu vya ugonjwa huo akihoa, kupiga chafya au kwa namna yoyote nyingine kurusha vitone vya makohozi yake kutoka katika mfumo wake wa hewa na kuvieneza hewani na mtu mwingine kumpata akivuta hewa ndani na hivyo kuingia katika mfumo wa hewa.
 
Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu yanayotokea kwa  kiasi kikubwa na kuwapata watu masikini  zaidi . Kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa ambao unafahamka kwa watu wengi  katika Tanzania kutokana na madhara mengi ambayo yamejitokeza na kuonekana iwe katika familia au katika jamii kwa namna moja au nyingine.


Huu, ni ugonjwa ambao umedumu kwa karne nyingi tangu ulipogunduliwa na mtaalam kutoa Ujerumani, Dk Robert Koch mwaka 1882 na kuushangaza ulimwengu wa tiba kwa ugunduzi wake huo.
Dk Koch aliduwaza wengi kwa kutangaza mjini Berlin kuwa alikuwa amegundua chanzo cha ugonjwa huo ambao nyakati hizo ulikuwa ukisumbua wengi huko Marekani na Ulaya, kusababisha vifo.
Mgunduzi wa Kifua Kikuu,  Robert Koch alipewa tuzo ya amani ya Nobel kwa ugunduzi wake huu ambao kwa kiasi kikubwa umeiokoa dunia. Wakati ule, TB ilisababisha kifo kwa mtu mmoja kati ya saba  na tangu wakati huo harakati mbalimbali zimekuwa zikiendelea katika kukabiliana nao.
 
Zikiwa zimebaki siku mbili dunia  iadhimishe siku hiyo, Machi 24  ni vyema kuuzungumzia ugonjwa huo ambao umeendelea kuwa hatari, unaoua mamilioni ya watu ingawa kwa sasa si Marekani au Ulaya kama zama za Dk Koch, bali katika nchi maskini.
Siku ya Kifua Kikuu Duniani
Kwa nyakati tofauti, walimwengu wakiwamo wanasayansi walikaa na, kukubaliana hivyo kuanzisha Siku  ya Kifua Kikuu duniani, Machi 24.
Siku hii ni mahsusi  kwa ajili ya kufanya mapitio kuhusu hali halisi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom