Jumatano, Aprili 29, 2015

SOMA KWA UMAKINI SHAIRI HILI "Maisha Changamoto kwa Vijana"

 Dar es Salaam Maisha  safari ndefu, mwenzenu nashuhudia,

Kama kamba ni ndefu, msibishe nakwambia,

Mioyo yetu kunjufu, yote yaja twapokea,

Mola wetu simamia, maana jibu halipo.


Kazini watu wahema, hawana yao riziki,

Kwa kuamka mapema kukisaka kitu hiki,

Kukibwa malezi mema, watoto wapate haki,

Mola wetu simamia, maana jibu halipo.


Achana bado elimu, wengi wetu wanalia,

Hapa kila mtu zamu, apate kuijulia,
Mwisho ndipo ni patamu, ukisoma wajutia,
Mola wetu simamia, maana jibu halipo.

Migodini nako sasa, watu wanahangaika,
Watakacho wanakosa, kila siku shughulika,
Vifo tu vinawatesa, miamba kutikisika,
Mola  wetu simamia, maana jibu halipo.
Angalia na masoko,  watu wanahurumiwa,
Utokako uendako, vitu vyote vyaanikwa,
Raha kwao ni miko, salio linatumiwa,
Mola wetu simamia, maana jibu halipo.

Akosa malezi mema, kutamani kaisha,
Matajiri watazama, bila ya kusaidia,
Mola wetu simamia, maana jibu halipo.
Bungeni napo pa moto, maelezo bila mwisho,
Wananchi ni majuto, ni kama maadhimisho,
Mafanikio ni ndoto, mateso twaomba shusho,
Mola  wetu simamia, maana jibu halipo.
Tazameni wasichana, biashara za mauzo,
Kipato mnagawana mkisahau tatizo,
Makaburi yatashona, bila hata ya kigezo.
Mola wetu simamia, maana jibu halipo.
Na madaktari nao, gumzo wameshukiwa,
Ugonjwa uingiao, ndotoni washituliwa
Dawa ipi ya mg’ao, watu waweze tibiwa.
Mola wetu simamia, maana jibu halipo.
Tamati nimefikia, kalamu naweka chini,
Ninatamani kulia, ninajikaza lakini,
Naamua kuachia, kwenu iwe ni yakini,
Mola wetu simamia, maana jibu halipo.
Jefroda Peter Mdemu,
0765 121227,
Dar es Salaam

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom