Ijumaa, Julai 31, 2015

SOMA KWA UMAKINI MACHACHE ALIYOSEMA LOWASA.



 
“Wapo watu wanaonishambulia kwa nini nimejiunga na Chadema, lakini wanapoteza muda hawatanirudisha, nimeridhika ndani ya CCM mabadiliko hayawezi kupatikana wakati Watanzania wengi wanataka mabadiliko,” alisema.
 
Lowassa alifafanua kuwa uamuzi wake wa kujiunga na Chadema ni katika kutekeleza maelekezo ya muasisi wa CCM, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyesema Watanzania wanataka mabadiliko wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.
 
Alisema tatizo la umaskini limekuwapo toka mwaka 1961 hadi sasa, hivyo Watanzania walio wengi wanataka mabadiliko na kwamba vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimejipanga kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu pasipo kutumia lugha za kuudhi na kejeli.
 
Lowassa alisema kitu cha msingi ni kushikamana kuhakikisha ushindi unapatikana na kwamba wananchi ambao bado hawajajiandikisha wakafanye hivyo na wale waliojiandikisha watunze shahada zao za kupigia kura.
 
“Nafurahi kwa heshima mlionipa, najiandaa kufanya kazi iliyotukuka na kazi itakayotuletea ushindi na Watanzania ushindi,” alisema.Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amechukua fomu ya kuomba kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku akiwarushia madongo wanaomshambulia kutokana na uamuzi wake wa kujiunga na chama hicho kwani ametafakari na kubaini kuwa ndani ya CCM mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana.
 
Alisema hayo jana baada ya kukabidhiwa fomu  ya kuomba kuwania  Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  katika hafla iliyofanyika makao makuu ya chama hicho Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi na viongozi wandamizi wa chama hicho. 

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom