Pages

Jumatatu, Agosti 10, 2015

Edward Lowassa kuchukua fomu yake leo.Leo wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake watashuhudia historia ikiandikwa pale vyama vinne vilivyosimamisha mgombea urais mmoja vitakapomsindikiza, Edward Lowassa (pichani) kwenda kuchukua fomu katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
 
Lowassa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alijiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kisha akachaguliwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kugombea urais.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema na kusambazwa kwa wanachama wote, Lowassa atachukua fomu shuku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo pamoja na wanachama.
 
Taarifa hiyo iliwataka wanachama katika maeneo mbalimbali ya jiji pamoja na mikoa jirani kuungana na Lowassa wakati atakapokwenda kuchukua fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo ya juu ya nchi.
 
Wiki iliyopita wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, walishuhudia mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Dk. John Magufuli akichukua fomu, huku shughuli mbalimbali za wananchi zikisimama kupisha msafara wake.
 
 Dk. Magufuli wiki iliyopita alichukua fomu huku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana; Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye; wajumbe wa Kamati Kuu na wanachama.
 
CHANZO: NIPASHE

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom