Alhamisi, Agosti 06, 2015

MIAKA 21 YA GAZETI LA NIPASHE


Leo ni siku muhimu kwa uhai wa gazeti la Nipashe tangu lianze kuchapishwa miaka 21 iliyopita. Ni siku ya kukumbuka kwa kuwa ni safari ndefu, tumevuka milima na mabonde, tuliteleza na kusimama, tuliimarika na kukabiliana na changamoto mbalimbali, lakini leo kwa ujasiri kabisa tunaona fahari kubwa kwamba bado tupo imara, safari yetu ya kuwaletea wasomaji wetu habari moto moto inaendelea kwa ari kubwa.
Kila tukitazama nyuma tunawiwa mno kwa wasomaji wetu, watangazaji na kila mdau ambaye kwa miaka yote hii 21 amekuwa nasi katika safari hii ya uhakika na mafanikio tuliyopata. 
Kwa moyo mkunjufu kabisa tunawashukuru wote waliotuunga mkomo, tunatoa shukrani hizi tukiamini kwamba wakati huu tunapoanza muongo mwingine wa kuwahabarisha, kuwaburudisha na kuwafikirisha kwa habari mbalimbali kama ilivyo desturi ya Nipashe, mtaendelea kuwa pamoja nasi, mtatuunga mkono na mtakuwa sehemu ya mafanikio yetu.
Wakati tunapiga hatua hizi, tunaweka wazi jukumu letu ambayo ni ahadi dhabiti kwenu kwamba tutaendelea kuwa gazeti linaloandika habari za uhakika, zilizofanyiwa uchunguzi, linalozingatia weledi, na maadili ya taalaum ya uandishi wa habari.
Tunaahidi kuendelea kuwaletea wasomaji wetu habari za uhakika, kwa kuzingatia kiu yao tumeboresha maudhui ya Nipashe kwa kila siku ya wiki kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi. Tunafanya hivyo tukiamini kwamba tutamgusa kila msomaji na matarajio yake.
Tutaanza wiki tukiwakumbusha wasomaji wetu katika ulimwengu wa michezo nini kilitokea, michezo mbalimbali iliyochezwa kwenye viwanja na ligi mbalimbali duniani mwishoni mwa wiki. Kutakuwa na tathmini mbalimbali za yalijojiri katika viwanja hivyo, ni siku ambayo kwa hakika kijarida kipya cha SPOTIKA kitatamba mitaani.
Jumanne tutajielekeza kwenye ujumbe murua juu ya tekinolojia, elimu na sayansi. Tujajituma kadri ya uwezo wetu kuwahabarisha kwa kina juu ya masuala hayo ndani ya kijarida ambacho kitatoka kwa jina la TESA.
Jumatato kama ambavyo imekuwa ada, siasa itaendelea kutawala. Makala na safu mbalimbali zitatamba. 
Tutakaribisha wataalam wa fani ya sayansi ya siasa na uchumi, wanasaikolojia na kila taaluma kujadili kwa kina masuala ya siasa na utawala, ili mwisho wasomaji wetu wapate kile kilicho bora kabisa.
Nipashe mpya Alhamisi inajielekeza kwenye masuala ya afya na mamzingira, hii ni ndani ya kijarida cha AMA, tunaahidi kuwa jukwaa la kutoa elimu kuhusu masuala ya mazingita na afya. Wataalam wa afya na mazingira watakaribishwa kutumia fursa hiyo kutoa darasa kwa umma wa Watanzania.
Ni ahadi yetu kwamba Ijumaa itakuwa siku njema kwa wasomaji wetu. Nipashe itakuwa ni jukwaa la kutoa elimu na biashara, uchumi na mambo ya fedha. Ni siku ambayo itavuta wajasiriamali, wachuuzi na hata wafanyabiashara wakubwa katika kuonyesha mafanikio yao na changamoto, ili kuwa chachu ya kuwatia wengine moyo. Kwa kufanya hivyo nao watajitambua na kujibiisha ili wapambane na adui umasikini. 
Tunaahidi kijarida cha BUFE kuwa nyezo ya kuwawezesha wasomaji wetu kujitambua.
CHANZO: NIPASHE

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom