Jumanne, Desemba 14, 2010

Etii ni kwanini baadhi ya wanaume ambao ni mahandsome kwa sana huwa wana mapozi na nyodo nyingi katika mahusiano

Kwa asilimia kubwa imekuwa ni kawaida kwa wanawake wengi kulalamika kuwa ukiwa na mwanamume mzuri wengine hupenda kuwaita mashalobalo,,,basi ni tatizo kwani anapendwa na wanawake wengi lakini pia kwa asilimia kubwa ya wanawake wanapenda wanaume wazuri na wengi wao huishia kuumizwa,,vilevile wanaume hao wazuri baadhi yao wengi wapo kwaajili ya pesa na si mapenzi,,,sasa sijui ni kwa nini hali inakuwa hivi labda nikusikilize mdau,,

Maoni 11 :

Simon Kitururu alisema ...

Kwani mwanamume Handsome ni wa aina gani huyo?

Si nasikia kuwa - kila mtu na ladha yake aka uzuri wa kitu uko jichoni mwa mtu mwenyewe kwa hiyo kila mtu handsome kwa ampendaye?

Bila jina alisema ...

Simon, kuna wanaume wazuri bwana, hiyo ukubali tu,inspite ya kwamba kila mtu namuona mzuri wake bt wapo wale wazuri kwa wote. Ni kweli wamejaa nyodo na kupenda kufugwa. Ni bse wanawake wengi wanawapapatikia tena wanawahonga ili wawapate ndo maana wanajisikia, hawanaga mapenzi kamwe. Bora kuwa na mwanaume wa kawaida unaishi kwa amani bila matatizo

emu-three alisema ...

`Hakuna mwanaume mzuri, uzuri wa mwanaume ni uanaume wake' aliniambia babu yangu. Nikamuuliza huo uanaume wake ni nini? Akacheka akasema, mke mzuri hutokana na uanauke wake, uwajibikai wake kama mwanamke, na mara nyingi mke unaweza kusema ni mzuri,lakini mwanaume, ni kutokana na uanaume wake...jinsi gani anavyotoa jasho lake kama mwanaume...' sikumuelewa!
Akaendelea, mwanaume akiwa na sura nzuri kama mwanamke lakini kama hatimizi ile hali ya kuitwa mwanaume sio kitu...kwahiyo mwanaume mzuri ni yule `mwanaume kweli'...akacheka.
Mimi najua kama walivyo wanawake wazuri kuringa ndivyo walivyo wanaume pia, ila ninachojiuliza bila kupata jibu ni je wanaringia nini kama wanaume, ni heri wanawake waringe, lakini mwanaume..inatia shaka kidogo.
Ni hayo tu dada yetu, karibi kwetu pia!

Bila jina alisema ...

Jamani wapo wanaumw wazuri!yani I mean kila atakayemuona atasema kweli ni mzuri kuanzia sura,body and smart!kweli hawa wanaume ni wazuri kwa nje tu!kwenye suala la uanaume hakuna kitu!then huwa hawajiamini kwenye hayo maswala thus why unakuta mara nyingi anakuwa na wanaweke wengi na hawezi kustay long in relationship.
Kuhusu kuwa na nyodo ni kweli wana nyodo ila hapo ndio ilipo confidence yao!

Simon Kitururu alisema ...

Mimi binafsi hata katika swala la wanawake,....
....mara kibao IMETOKEA nikisikia watu wanakidai Mwanamke fulani ni mzuri sana,....
....na nikabaki kujiuliza hivi mimi ni nininakosea kukiangalia kwa kuwa hua sistukii wastukiacho hasa kisababishacho wadhani KIMWANA ni mzuri kupindukia ni nini.


Na huwa nachanganyikiwa zaidi nikiwa nchi tofautitofauti au nikiwa tu na marafiki zangu watokao nchi na mabara tofautitofauti wakiwa wanaongelea kwanini MSICHANA fulani ni mzuri.:-(

Na katika swala la WANAUME nafikiri komenti yangu hapo juu imetoa siri kuwa swala hili jicho sina na labda ni WASICHANA na WAVULANA wapendao mabasha ndio wenye kulijulia zaidi na nashukuru kwa kujulishwa zaidi kuhusu hili swala.

@Anony wa9.33AM :Uliyeandika ``Simon, kuna wanaume wazuri bwana, hiyo ukubali tu,inspite ya kwamba kila mtu namuona mzuri wake bt wapo wale wazuri kwa wote......´´

Hili kwangu ni jipya kwa kuwa BADO siamini kuna mtu MZURI KWA WWOTE!:-(

Bila jina alisema ...

Kuna wanaume wazuri kweli kwa wadau mnaobisha, mfano mdogo, kama umeona 'Don mess with an angel" Miguel ni mfano wa wanaume wazuri. Wapo wachache ambao wanajiheshimu na wana mapenzi kweli, lakini majority ushuzi mtupu.

Bila jina alisema ...

Mtukufu ni kweli usemayo. Kizuri kwako kinaweza kuwa si kizuri kwa mwingine. Kuna wanawake wanapenda wanaume warefu, weupe na wenye mwili wa wastani kwake yeye huyo ni mzuriwengine wanapenda kinyume cha huyo utamsikia mwanamke anasema mwanaume mweupe sitaki hata kumuona. Kuna wanaume pia wanapenda wanawake wembamba wengine wanapenda wanawake wanene. kwa hiyo kila mmoja atasema wa kwake mzuri kuliko mwingine. Salimia Helsinki......

Simon Kitururu alisema ...

@Anony wa 4.29PM: Salamu zitafika Helsinki!

Na kama ulivyosema siamini kuna UZURI universal ingawa ni rahisi kudhani udhabniacho ni kizuri sana ndio ukweli mtupu na ndicho kipendwacho na wote kama wadhaniao hata kwa imani zao kwa kuwa ni WAKRISTO basi UKRISTO ndio jibu la yote kwa hiyo waislamu yao sio KWELI .:-(

Bila jina alisema ...

mimi nilikuwa natoka na mwanamme mzuri tu, yaani tulikuwa tunadate enzi hizo(mchagga) yaani kijana ni mzuri mweupe, mrefu, wee akicheka utampenda, basi siku ikatimia tukaaamua ha mchezo wa baba na mama! loh! ilikuwa mara yangu ya kwanza, sikuelewa. nikaenda zangu kwa moi kusoma nikakutana na kijana mmoja kanipenda sasa, si mzuri kama wa kwanza, mfupi, mweusi tii! tukawa na uhusiano tukiwa chuo, wee mbona yule handsome nilimwacha usiku ule! this is so tru amd am happy to share with u! niliporudi likizo tukaendelea na mapenzi yetu but nothing, eti akimaliza tu anakimbilia bafu kuoga, mara hivi, halafu inalast 4 mins only! kweli wakaka wazuri balaa, hamna kitu huku chini

Bila jina alisema ...

naungana na anonymous wa december 19,2010 12:57 mwanaume mzuri hakuna kitu,kulinga kwao ndio silaha yao!kuwa nae ni kupoteza mda tu!

Bila jina alisema ...

jaman kweli wanaume wazuri wanamashauzi ila siyo wote me nimewai kuwa na mwanaume mzuri mweupe kwan fani yangu mwanaume mweupe ila uye kaka alikuwa akipita kila mtu ana muangalia akaja kutoka msichana mmoja mm nilpo maliza xl niliumia sana nikamuuliza why akasema eti ule msichana ndo alimtongoza kweli wanaume wazuri pasua kichwa kila mtu anamtazama

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom