Jumatano, Desemba 15, 2010

Jamani ni kwa nini unakuta baadhi ya mabosi wanawabaka wafanyakazi wa ndani?Huko Morogoro bosi anasakwa kwa kumbaka mfanyakazi wake.

Inaumiza na kusikitisha kuona matukio ya kikatili kwa wanawake yakitokea kila kukicha kweli unakuta mtu ana mke wake mzuri lakini anaamua kumbaka msichana wa kazi chanzo ikiwa ni tamaa za kimwili,, huko Morogoro Jeshi la polisi linamsaka Moses David kwa tuhuma za kumbaka mfanyakazi wake mwenye umri wa miaka 13  baada ya kumlaghai kwa kumuonyesha picha kwenye luninga, na hivyo baada ya binti huyo kuingia ndani kwa njia hiyo ya kumrubuni mtuhumiwa alimkamata na kumbaka na kutoroka,Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na aliko mtuhumiwa huyo ili akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka la ubakaji...Haya ni mambo ambayo yanatokea katika baadhi ya sehemu tofauti na kwa namna tofauti ikiwa ni kwa kubaka au ni kwa makubaliano baina ya msichana wa kazi na baba mwenye nyumba,,hivi nini hasa chanzo jamani na nini kifanyike wadau.....

Maoni 6 :

emu-three alisema ...

Ukiliangalia tatizo hili kwa juu juu unaweza kusema ni tamaa mbaya za wanaume. Na tukawaona wanaume ni watu wabaya,wana tamaa, hawatosheki nk. Lakinii huwa ninapenda kuuliza swali hili mara kwa mara, `inawezekana kweli umshibishe mtoto wako vyema aende kuomba kwa jirani?'
Mara nyingi tunapenda kutizama mambo katika hitimisho lake na kuacha mizizi na shina. Ndio kuna tamaa mbaya za kibinadamu , hiyo ipo, lakini hili kweli linaweza kutatua tatizo sugu, bila kuangalia kiini chake. Nahisi kuna tatizo kubwa ambalo hatutaki kulikubali nalo ni `uhaba au uelewi wa kushibishana ndani ya ndoa'
Huu ndio ukweli halisi wenye hekima watalitambua hili kuwa nina maana gani!
Unafikiri kwanini kuna kitu kitchen party, kulikuwa na unyago, nk. Hili wenzetu waliliona, na kujua kuwa binadamu anatawaliwa na `tamaa' hasa mwanaume! Je ifanyike nini kuizibiti hii tamaa, ndio maana wakawa wanweka vidarasa kama hivyo, ili kusaidia , angalau...lakini wenzetu wamelichukulia kama sehemu ya burudani na ile maana halisii haipo tena.
Jamani ndoa ni kitu athimu, ni kitu kitakatifu, ni sehemu ambayo mke na mume mnatakiwa `muwe kitu kimoja' mtulizane mitima nyongo yenu...na mtaliweza hili kama mtaielewa ndoa na misingi yake. Na mojawapo ni kushibishana. kama hamtalifanyia kazi hili, kila siku kesi kama hizi zitajitokeza sana. Lawama nyingi, lakini mwisho wa siku watu wanaumia. TUTAFAKARI KWA MAPANA
Ni hayo kwa leo wapendwa!

EDNA alisema ...

Hizo ni tamaa zao za mwili zinawasumbua viumbe hawa.

Yasinta Ngonyani alisema ...

inasikitisha kwa kweli kila kona siku hizi unasikia hizi habari yaani ndo zinazidi. Na ni lipi linalompa raha huyu anayebaka? Yaani inauma na inasikitisha kiasi kwamba natamani kama ninge...naacha!!

Bila jina alisema ...

tamaa za kimwili ndizo zinasababisha hayo mambo na kutomshirikisha mungu kutokana na ukosefu wa imani,mana kama una imani na unaijua dini huwezi kufanya kitendo cha aibu kama hicho.

Bila jina alisema ...

Swali wapendwa, kama ni tamaa kifanyike nini kiizibiti hiyo tamaa, tutafaute `chanzo na suluhisho' Naona M3 Kajitahidi kudodosa, lakini je ni hayo tu....Mimi napendekeza, kutafutwe dawa za kupunguza `libido' kwa wanaume kama hawo, wakikamatwa pamoja na kifungwa wanpewa hiyo dawa, mjamaa anakuwa hana makali tena! Mwasemaje?

Bila jina alisema ...

Kwa upande wangu namuunga mkono m3 kwa alichotangulia kuelezea hapo juu tutake tusitake haya matatizo yanaanzia ndani ya ndoa husika wakina mama hawakawii kusema mie nimechoka sijui nini na ninihali kadhalika waume nao utasikia oh mie leo nimefanya kazi nyingi nina uchovu sasa hapo ndipo yanapoanzia hayo matatizo kama ni baba anaona ana nyama karibu anaishawishi na kutekeleza matakwa ya hamu zake ambazo mama mwenye nyumba kachemsha kuzihudumia pia akina mama nao akiona hivyo kwa nini asimshawishi house boy au mtanashati wa karibu na hera za ndani za chakula watapatiwa hawo waokoa jahazi hilo hivyo matatizo huanzia ndani ya ndoa zenyewe sasa ifanyweje ili hili tatizo likome kabisa kitakiwacho hapo kila muhusika katika ndoa ajue wajibu wake kikamilifu na kila mwanandoa kumjali mwenza wake katika kila hali na ktk swala la unyumba hamna kuchoka kama wanandoa watafuata hivyo sizani kama kutakuwa na matatizo kama hayo katka jamiii- Rchie wa ughaibuni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom