Ijumaa, Desemba 17, 2010

Swali kutoka kwa Ramadhani mkazi wa Dar es salaam,,nachukia tabia ya mke wangu kusikiliza maneno ya watu na kunitukana mbele za watu imefikia wakati nawaza kumuacha.

Katika mapenzi migogoro ni jambo ambalo linatokea  na hivyo wengine kujikuta wakipigana,kuachana,kudharauliana nk....Ramadhani anasema,,,mke wangu anayo tabia ya kusikiliza maneno ya watu bila ya kuchunguza ili kupata ukweli na hii tabia imekuwa ikijirudia kila kukicha na baada ya kuambiwa hayo maneno huwa ananitukana mbele za watoto kwa lugha chafu ambazo siwezi hata kuzitaja nilishamuambia huwa sipendezwi na hiyo tabia lakini bado anaendelea kiasi kwamba hata watoto wameanza kunidharau inaniuma sana kwani nampenda mke wangu na watoto wetu wanne lakini kwa hatua aliyofikia kunitukana na kunisema kwa majirani kwa maneno machafu nahisi kukata tamaa nataka nimuache kwani nimeshindwa hata nimuelekeze vipi hanielewi naomba ushauri...Je nini ushauri wako mdau....

Maoni 2 :

Unknown alisema ...

Nimeipenda sana hii profile yako. Big up sana

emu-three alisema ...

Tatizo ni lile lile la watu kutokuelewa nini maana ya ndoa na kutokujua kuwa ndoa ni jambo takatifu ambalo ukiingia ndani yake unatakiwa uliheshimu kama unavyoheshimu vitu vitakatifu.
Ndani ya ndoa na mambo ya ndoa ni nyeti haitakiwi kuyatangaza, kama sio lazima kufanya hivyo. Labda kwa nia ya kuelimishana au kusaidia ili ndoa hiyo iwe katika msimamo! Mkikizana mnatakiwa muhakikishe mnayaongea chumbani, na ikiwezekana watoto wasijue.
Kuna kisa kimoja cha bosi wetu mmoja, mzungu yeye anasema kuwa kuna wakati yeye na mume wake walikuwa hawaelewani, na ilifikia hatua kwamba wanalala mzungu wa nne. Lakini anasema kwa jinsi anavyoihehimu ndoa yake, haikuwezekana.
mume wangu, alinihitaji kindoa nami nikaitikia haraka haraka, na jinsi tulivyohitajiana ndivyo ile hasira ilivyoyeyuka,....akatushauri kuwa tendo la ndoa huangamiza hasira na chuki, na ni dawa ya mambo hayo na pia huleta baraka.
Kama mkikosana na mwenzako jaribuni kuitafuta hii dawa, ina baraka zake na huleta mafanikio makubwa kama mumekwama kimaisha! Lakini wengine huitumia kama silaha ya kumpigia mwenzake, kumbe kufanya hivyo ni kujiangamiza mwenyewe.
Sasa kwa huyu anayebwabwaja mitaani kuhusu mume wake ajue kuwa anaifukuza baraka ndani ya nyumba.
Lakini wewe kama mwanandoa usikimbilie kuachana, kwani hiyo haisaidii, wewe ni kukaa naye na kujaribu kumwelezea ubaya wa hayo. Kama unakumbuka kisa kimoja cha jamaa aliye toa ahadi kuwa akifanikiwa jambo fulani atatoa sadaka kwa shetani, alipofanikiwa akashindwa kumjua shetani ni nani ili ampe hiyo sadaka, akaenda kuulizia kwa watu wa imani wakamwambia kuwa shetani anaweza kuwa binadamu mwenyewe,akaambiwa akimkuta mwanamke au mwanaume anayetoa siri za ndoa, au anayemzungumza mkewe au mumewe vibaya basi huyo ni shetani mpe sadaka yako!
Jamani tusikubali kuwa mashetani wa kibinadamu!
Ahsante

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom