Mwanamume yeyote ambaye anajua maisha ya mahusiano lazima atakuwa anajipenda na kujitunza na atakuwa makini kwa yule anayempenda ili kumridhisha na si kuwa kero,kingine katika kazi wanawake humtaka mwanamume ambaye amejiwekea malengo katika maisha yake,,hata hivyo mwanamume anatakiwa kuepuka kudanganya kazi yeke halisi kwani haitasaidia chochote zaidi ya kukuharibia pindi mwenza wako atakapobaini baadaye,kingine ni kwamba wanawake wengi huwa hawapendi wanaume ambao hawana uelewa na chochote kinachoendelea yaani wajinga,,pia tabia ya kunywa na kukaa muda mrefu kwenye baa sifa hiyo ya kijinga haiwezi kumfanya mwanamke akuangukie kimapenzi au kuvutiwa na wewe badala yake utamkimbiza,,kingine ni kwamba usifiche vitu unavyovipenda kama mchezo wa soka nk..lakini usifanye kile unachokipenda kikawa kero kwa mwenzio.Hivyo basi kwa mwanamume mwenye malengo ya kuanzisha mahusiano inabidi awe mvumilivu na mwenye nia kutoka moyoni.......MAPENZI SI MCHEZO BALI NI MALENGO NA MAISHA YENYE UPENDO NA FURAHA NDANI YAKE. |
Maoni 2 :
Na kweli maisha ni malengo, na malengo haya yatakamlika kama nyote mke na mue mtakuwa pamoja bila kutegeana. Ni vyema mke na mume mkawa na muda wa kukaa pamoja na kujadili maisha yenu , nini kifanyike na mikakati ya baadaye.
Inashngaza sana wanawake kuwa wanasubiri mikakati ifanywe na mwanaume, mipango na kila kitu cha maendleo ya familia hapana, lazima mkae pamoja mjadili hili linafaa, hili halifai.
Umenikumbusha kisa kimoja cha jamaa alimuoa mke, yeye alikuwa na umbo dogo, na mke wake alikuwa pande la mama. Sasa yeye akirudi kazini mke wake anampokea, halafu mke anamuinua mume kichwa chini miguu juu, kuhakikisha kila kitu alichokuja nacho kinadondoka toka mifukoni...baadaye anmuita mezani , haya ulichopata ndio hiki tupange mtumizi...ni kichekesoo kama mnavyokiona lakini kina maana kubwa na tafsiri ni nyingine kabisa!
Samahani dada Adela, usije ukaona nimehamisha visa toka kule kwangu kuvileta hapa. Ni hayao kwa leo!
hahahahaha nimeipenda sana @Emu three ni kweli maisha ni kusaidia na si kumtegemea au kumnyanyasa mmoja hili ni la wote mwanamke na mwanamume
Chapisha Maoni