Katika mapenzi wapo baadhi ya wanawake ambao huwalaghai wenza wao na hii hufanikiwa pale ambapo wanawake hao huwasomaakili waume zao hivyo basi kinababa inabidi kuwa makini katika hili ,,kwa mfano mama kuwa na mahusiano nje ya ndoa hili kosa hata baadhi ya kina baba hulitenda lakini huonekana ni kosa zaidi linapojitokeza kwa kinamama ambapo kutokana na sababu ya kukosa haki ya msingi kutoka kwa waume zao basi anaamua kuanzisha mahusiano ya nje kisirisiri na kujikuta anapata ujauzito nje ya ndoa kitu ambacho inawezekana baba kugundua iwapo mtoto akizaliwa na sura tofauti na hivyo kuamua kwenda kupima vipimo vya DNA au inawezekana asigundue asipokuwa makini.
Upo ulaghai mwingine ambapo kina baba wanafanyiwa na na baadhi ya wenzi wao inawezekana wakawawanaugundua au wasiugundue kwa mfano mama anakuambia anasafiri kikazi kumbe yupo sehemu fulani,,au ameenda kumtembelea rafiki kumbe sivyo mwingine ananunua vitu vya gharama kuliko uwezo mlio nao kama kiwanja,,gari,,nguo za kifahari na mambo mengine mengi huku akikudanganya anapata mikopo bila wewe kufanya uchunguzi kumbe kuna mtu anamfanyia yote hayo.Ujanja huu hufanywa pia na wanaume laghai kwa wake zao..TATIZO LA ULAGHAI KATIKA MAPENZI LIPO PANDE ZOTE ILA KINACHOTOFAUTIANA NI VIWANGO,,Au unasemaje mdau..............
Maoni 3 :
Mimi mara nyingi nashindwa kuelewa, `ulaghai huo unamdanganya nani? ni kama kutoa pesa mfuko huu na kuuweka mfuko huu. Kasababu mnapooana nyie ni kitu kimoja, hili sijui kama watu wanaelewa. Je unaweza kujikata kidole mwenyewe makusudi. Huwezi, sasa mbona watu wanajifanya hawaelewei, kuwa wewe mke au wewe mume ukifanya baya la kumuumiza mwenzako ni sawa na kuiumiza mwenyewe. Kwahiyo ukimdanganya mwenzio ukajifanya umjanja, umejidanganya mwenyewe, kwani mwisho wa siku itakula kwako, its just a matter of time..
Some times kina mama uwa wanafanya kwa kulipiza kisasi,inakera sana mtu unajiheshimu,halafu mwenzio anaenda hovyo,kwani nani hatongozwi bana?mtu anaona kama noma na iwe noma tu.
david jermos kwa upande wangu mimi naona kuwa baadhi ya watu wanashindwa kuelewa nini maana ya mapenzi/upendo wa kweli ktk mahusiano,kutoelewa kwao kitu hicho ndipo kinapelekeya ulaghai katika huhusiano.
Chapisha Maoni