Jumatatu, Desemba 20, 2010

Disko toto marufuku sikukuu ya Krismasi na Mwakampya..........

Watoto wanapenda kucheza na kufurahi pamoja sehemu mbalimbali kipindi cha sikukuu..Huko mkoani Tabora Polisi wamepiga marufuku disko toto wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya ni baada ya vifo vya watoto 19 miaka miwili iliyopita wakati wa Sherehe za Idd el Fitri.Polisi wamesema ni marufuku kwa wamiliki wa kumbi za starehe kupiga disko toto kwenye mkesha wa Krismasi na Mwaka Mpya.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Liberatus Barow amesema Jeshi hilo limejipanga vilivyo kuhakikisha raia pamoja na mali zao zinalindwa wakati wa sikukuu.. pia amesema bado tuna majeraha makubwa mioyoni mwetu kuhusu tukio la kufariki dunia watoto 19 waliopoteza maisha kwenye ukumbi wa disko na kusisitiza ni marufuku disko toto na mmliki yeyote atakayekutwa anapiga disko toto atakamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani..Je mdau nini ushauri wako kuhusiana na disko toto mikoa mbalimbali kipindi cha sikukuu

Maoni 1 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

hakuna kulala hata kama hujala....kwakweli ni jambo la busara walifanyalo maana ni kweli furaha lakini mwisho wake ukiwa mauti hakuna furaha tena.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom