Jumanne, Desemba 21, 2010

Unaizungumziaje tabia ya baadhi ya wanawake kutupa watoto wachanga baada ya kujifungua kwa madai kuwa mwanamume amekataa ujauzito.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanawake kutupa watoto baada ya kujifungua kila kukicha huku kukiwa na madai tofauti kama kwasababu mwanamume aliyempa mimba ameikataa,kwa nia ya kuendelea na masomo,,mwingine anafanya hivyo kutokana na hali duni ya maisha na kwasababu hakuwa tayari kuzaa kwa wakati huo hizo ni baadhi ya sababu ambazo huwa wanazitoa baadhi ya wanawake wanapokamatwa kwa kuwatupa watoto wachanga.Huko Morogoro Muuguzi wa Hospitali ya Mtakatifu Kizito Mikumi wilayani Kilosa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua mtoto mchanga muda mfupi baada ya kumzaa,Kamanda wa Polisi Mkoani hapo Adolphina Chialo amesema muuguzi huyo alimzaa mtoto wa kiume desember 19 mwaka huu kisha kumtupa na kuokotwa tayari akiwa ameshafariki,Chanzo cha muuguzi kumtupa mtoto huyo kinaelezwa kuwa ni kukataliwa na mwanamume aliyempa ujauzito huo.Hata hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi na wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi.....Haya matukio yamekuwa yakitokea mara kwa mara  nini kifanyike jamani katika hili kwani sizani kama ni sahihi kuua mtoto kwa madai yoyote yale.............

Maoni 1 :

emuthree alisema ...

``Huko Morogoro Muuguzi wa Hospitali ya Mtakatifu Kizito Mikumi wilayani Kilosa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua mtoto mchanga muda mfupi baada ya kumzaa...''
Nimenukuu kwa `mshangao' ni kama kumkuta polisi anakwiba, au dakitari bingwa wa akili anavuta bangi...inakuna kichwaa.
Lakini vyovyote iwavyo sote ni binadamu, hata awe raisi au kasisi au shehe, makosa yakibinadamu hayakwepeki kwani sisi sio mitume!
Cha kujiuliza ni `kwanini' na hata hiyo sababu aliyotoka haiwezi kukidhi kosa hilo kubwa, kwani huyo kiumbe anahusikaje...mbona mwamuazibu asiyehusika? Dhambi kubwa sana na laana kubwa sana, na watu kama hawa wanweza wasizae tena...!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom