“ Mungu naomba unisaidie maisha yangu yamekuwa na matatizo mengi kila ninalofanya linashindikana, sijui nikimbilie wapi nashindwa kuelewa kosa langu ni nini? nimepitia tabu nyingi sana, lakini bado maisha yangu sina raha siku zote mimi nimekuwa ni mtu wa kulia nisaidie Mungu wangu ”.
“Nimechoka sana leo na bado kuna
kazi zinanisubiri halafu sijisikii vizuri nahisi nataka kuugua” ni maneno
aliyokuwa akiwaza moyoni Mama Joyce ambaye alikuwa alikuwa akiosha vyombo, “Hii
hali yangu nahisi kama kuna jambo ambalo
haliko sawa embu niandae chakula cha mchana Joyce na James wakirudi wakute
nimekwisha waandalia chakula” Alinyanyuka na kuelekea jikoni kuandaa chakula.
Ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya
saa kumi na mbili jioni Mzee Ndesanjo alikuwa akiendesha gari aina ya Eskudo. Alifika nyumbani na haraka alishuka ndani ya gari kitendo cha kuingia ndani tu alianza kuita kwa sauti "Mama Joyce Mama
Joyce" huko chumbani Mama Joyce alimsikia na kuitika "Abeeee Mume
wangu,vipi mbona mbiyo mbiyo hivyo "?
Alihoji Mama Jocye huku akiwa
anamuangalia mume wake kwa umakini.
Mzee Ndesanjo ambaye ni mume wa Mama Joyce,
alionekana kuwa na wasiwasi mwingi huku akimsisitiza mke wake ajiandae haraka
"Hakuna muda wa kupoteza, "Mimi
ndani siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro, kuna matatizo
yamejitokeza. Rafiki yangu Mzee Simba
ambaye tunafanya kazi ofisi moja amefiwa na mke wake wake inabidi tuwahi
kwenda msibani”
Mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari kwani ile habari ilimshtua "Mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa! masikini" Aliongea kwa masikitiko "Alikuwa anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke". Mama Joyce akamjibu "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani"? Aliuliza Mama Joyce.
Mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari kwani ile habari ilimshtua "Mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa! masikini" Aliongea kwa masikitiko "Alikuwa anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke". Mama Joyce akamjibu "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani"? Aliuliza Mama Joyce.
Wakati huo Jocye na mdogo wake aliyeitwa
James walikuwa wameenda shule , Joyce alikuwa darasa la tano na James akiwa
darasa la kwanza. Na pale walipokuwa wakiishi ilikuwa ni nyumba ya kupanga
Maeneo ya Kimara Stop Over jijini Dar es salaam. Baba Joyce alimgeukia tena mke
wake "Hawa watoto tutamkabidhi
jirani yetu Mzee Ngonyani na mkewe, kwani
hatuendi kukaa zaidi ya siku mbili wewe jiandae tuondoke wakirudi kutoka shule
watakuta maagizo kutoka kwa mke wa Ngonyani".Baba Joyce aliongea kwa
msisitizo.
Kwa haraka Mama Joyce akaenda kwenye chumba cha Mke wa Ngonyani na kumwachia maagizo ya kuwaangalia watoto wake kwa muda wa siku mbili. Baada ya hapo aliingia chumbani na kujiandaa tayari kwa safari, ambapo safari ilianza taratibu na baadaye Baba Joyce alionekana kuendesha gari kwa mwendo wa kasi “Mume wangu mbona unaendesha kwa kasi hivyo jamani punguza mwendo kidogo” Aliongea kwa kuonyesha hali ya uoga.
Kwa haraka Mama Joyce akaenda kwenye chumba cha Mke wa Ngonyani na kumwachia maagizo ya kuwaangalia watoto wake kwa muda wa siku mbili. Baada ya hapo aliingia chumbani na kujiandaa tayari kwa safari, ambapo safari ilianza taratibu na baadaye Baba Joyce alionekana kuendesha gari kwa mwendo wa kasi “Mume wangu mbona unaendesha kwa kasi hivyo jamani punguza mwendo kidogo” Aliongea kwa kuonyesha hali ya uoga.
Baba
Joyce alicheka kidogo na kusema “Acha kuogopa Mke wangu mbona naendesha katika mwendo wa
kawaida sana”. Safari iliendelea wakiwa
njiani maeneo ya Kidatu, ghafla gari lilipata pancha tairi ya mbele na
kupinduka. Ilikuwa ni ajali mbaya sana
kwani Baba Joyce alifariki palepale na Mama Jocye alikuwa ameumia sana sehemu
za kichwani hivyo wasamaria wema walimchukua na kumkimbiza hospitalini.
Baada
ya wasamaria kumkimbiza hospitalini Mama Joyce ambaye kwa wakati huo alikuwa
hajitambui, Askari Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili
wa marehemu wa Baba Joyce na kuupeleka chumba cha maiti hospitali ya Morogoro.
Gari lilikuwa limeharibika sana kutokana na ajali ilivyokuwa mbaya hivyo
ulifanyka utaratibu wa kulisogeza hadi kituo cha polisi, wakiwa hospitalini
Mama Joyce alikuwa hajitambui kabisa.
Polisi
waliamua kufanya utaratibu wa kufahamu ndugu ambao wangeweza kuwa naye karibu
kwa wakati huo, mmoja wa wale Askari Polisi alimwambia mwenzake "Sasa
tutafanyaje kuwapata ndugu zao kwani huyu mama hajitambui na mume wake
amekwisha fariki inabidi tuwatafute ili waendelee na taratibu nyingine".
Mwenzake ambaye alikuwa naye akamjibu na kusema "Inabidi tuangalie
namba zilizopo katika simu zao ili tuweze kuwasiliana na ndugu zao".
........nini kitaendelea usikose sura ya .....2........ NI SIMULIZI YA KUSISIMUA AMBAYO KITABU CHAKE KIPO JIKONI. Niliwahi kuiweka kidogo zamani sana lakini hii ya sasa imekamilika na marekebisho yamefanyika kwa umakini. Endelea kupata uhondo.
Maoni 5 :
jmn uwiiiiiiiiii,kuanza na mikosi,ila c ungetumalizia ya mama bilionea na hkna siri mpz?au hutaweza kumudu kutuwekea zote?
asante rafiki nimeweka ratiba kila siku ya jumatatu na siku ya alhamisi ni simulizi ya Bado mimi na siku ya jumanne na siku ya ijumaa ni hakuna siri lakini siku ya jumatano na siku ya jumamosi itakuwa kosa langu ni nini...karibu sana tuendelee kuwa pamoja
Kma ivyo hkn neno mpz,mdau no moja ktk blog yako,mana kile kitabu cha kwanza nilitumiwa kutoka bongo
asante sana mdau tuko pamoja
Thanx
Chapisha Maoni