Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KOSA LANGU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo KOSA LANGU. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, Oktoba 14, 2013

SIMULIZI YA KOSA LANGU NI LIPI SEHEMU YA ...........20...........


ILIPOISHIA 
Joyce aliinama chini kwa aibu "Mama naomba unisamehe sikukusudia kutenda yote haya ni shetani tu alinipitia nisaidie mama ni wewe pekee unaweza kuwa karibu na mimi" waliendelea kuzungumza baadaye mama Robert alinyanyuka na kuelekea chumbani huku akimtaka Joyce aende chumbani kwake akapumzike. ITAENDELEA 

INAPOENDELEA
Huko chumbani Joyce alikuwa akiwaza "Eeee Mungu naomba unisaidie sijui Baba mkubwa akija atanifanya kitu gani, si anaweza kunifukuza hapa nyumbani,  sijui nitaenda wapi mimi".

Nyumbani kwa  Sukari alikuwa akiishi na dada zake ambao ndiyo walikuwa wakimuangalia mtoto wa Joyce mmoja alikuwa akiitwa Samanda na mwingine aliitwa Sungi siku hiyo walikuwa wamekaa pamoja kibarazani wakiteta "Ndugu yangu Samanda hivi ukimuangalia huyu mtoto wa kaka unamuonaje?" Aliuliza Sungi "Mmmh na wewe kwani amefanyaje mi naona ni mtoto mpole hana matatizo kwani wewe unamuonaje".

 Alijibu na kuuliza Samanda huku akiguna kidogo, Sungi akaendelea kusema "Yaani mimi huyu mtoto nikimuangalia tu naona kama si wa kaka yetu kabisa mbona hata hafanani naye. "Huo sasa ni umbea ndugu yangu mimi naona kawaida tu acha mambo ya kizamani kwahiyo asipofanana naye ndiyo unamaanisha kuwa yawezekana kuwa huyu siyo mtoto wake" Alihoji Samanda "Ndiyo, huyu mtoto siwakwake kaka amekurupuka tu" Sungi aliongea huku akijiamini. "Hee! Wewe Sungi umechanganyikiwa,  tena nyamaza kaka asije kukusikia kwasababu anaweza hata akakufukuza hapa nyumbani".

Jumatatu, Septemba 30, 2013

SIMULIZI YA KOSA LANGU NI LIPI SEHEMU YA 19



ILIPOISHIA
Joyce alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwa Hoteli aliwaza sana  “Eeeh Mungu naomba unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui nitafanyaje, yaani nahisi kuchanganyikiwa, nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa Lina. Hapa nilipo nina nina ujauzito wa Fredy, yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na hayazoleki. nimeharibu kila kitu na Fredy hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura yangu.eeh Mungu nisaidie" aliendelea kuwaza Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA  18. 

INAPOENDELEA         
Fredy aliamua kwenda nyumbani kwa walezi wa Joyce na kuwaeleza hali halisi kuhusiana na  yaliyotokea  alikuwa akiendesha gari huku akiwa mwingi wa mawazo “Huyu mwanamke ameniaibisha sana sikuwahi kutegemea kama ana tabia mbaya kiasi hiki ni vyema nikawafahamishe na wazazi wake ili wajue nimemfukuza  binti yao”  Alikuwa akiwaza huku akiwa anaendesha gari kwa kasi  bado kidogo asababishe ajali baada ya kumkosakosa  jamaa mmoja dereva taksi “Wewe kijana mpumbavu sana, mlevi nini wewe unaendesha gari ovyo yaani ungenigonga leo ungenilipa gari jipya” Aliongea dereva taksi kwa ukali huku Fredy akijifanya kama hajamuona na kuendelea na safari yake.

Alipofika nyumbani kwa walezi wa Joyce alikaribishwa vizuri sana “Shikamoo mama habari za hapa” “Marahaba Karibu mwanangu habari za nyumbani jamani mbona mmekuwa kimya sana yaani mnashindwa kabisa kuja kutusalimia” Alilalamika Mama Robert “Asante Mama majukumu tu ndiyo yanasabisha kimya kinakuwa kingi” alisema Fredy huku Mama Robert akiwa anaketi katika sofa lilokuwa pembeni yake “Jamani wanangu haiwezekani mkapotea kwa kiasi hicho sisi ni wazazi wenu mnatakiwa kuja kutujulia hali mara kwa mara, haya na huyo mwenzio yuko wapi mbona hamkuongozana?” Aliuliza Mama Robert .

Fredy aliyekuwa amejiinamia kana kwamba kuna kitu anatafakari “Mama kuna jambo ambalo limenifanya nije hapa leo ni vyema na baba angekuwepo ili niweze kuzungumza nanyi wote jambo lenyewe linamuhusu Joyce” Mama Robert  akiwa anamtazama kwa umakini sana Fredy akasema “Mbona unanitisha mwanangu kuna nini kimetokea mwenzio anaumwa au ni nini tena jamani?” Hapana Joyce siyo mgonjwa ila kuna mambo yametokea nadhani ni vyema ukamuita na Baba” Alisisitiza Fredy .

Jumatano, Julai 24, 2013

SIMULIZI KOSA LANGU NI LIPI......SEHEMU YA ....18......



 ILIPOISHIA
Joyce alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwa Hoteli aliwaza sana  “Eeeh Mungu naomba unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui nitafanyaje, yaani nahisi kuchanganyikiwa, nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa Lina. Hapa nilipo nina nina ujauzito wa Fredy, yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na hayazoleki. nimeharibu kila kitu na Fredy hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura yangu.eeh Mungu nisaidie" aliendelea kuwaza Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA  18. 

INAPOENDELEA
Fredy aliamua kwenda nyumbani kwa walezi wa Joyce na kuwaeleza hali halisi kuhusiana na  yaliyotokea . Alikuwa akiendesha gari huku akiwa na mawazo mengi “Huyu mwanamke ameniaibisha sana sikuwahi kutegemea kama ana tabia mbaya kiasi hiki. Ni vyema nikawafahamishe na wazazi wake. Ili wajue nimemfukuza  binti yao”.

  Alikuwa akiwaza huku akiwa anaendesha gari kwa kasi  sana. Kutokana na mwendokasi aliokuwa nao   kidogo asababishe ajali. Ni baada ya kumkosakosa  jamaa mmoja dereva taksi “Wewe kijana mpumbavu sana, mlevi nini wewe unaendesha gari ovyo. yaani ungenigonga leo ungenilipa gari jipya” Aliongea dereva taksi kwa ukali huku Fredy akijifanya kama hajamuona na kuendelea na safari yake.

Alipofika nyumbani kwa walezi wa Joyce kwa bahati nzuri aliwakuta wote wapo nyumbani. Walimkaribisha “Shikamoo Mama habari za hapa” “Marahaba Karibu mwanangu habari za nyumbani jamani mbona mmekuwa kimya sana yaani mnashindwa kabisa kuja kutusalimia”.

 Alilalamika Mama Robert “Asante Mama majukumu tu ndiyo yanasabisha kimya kinakuwa kingi” alisema Fredy huku Mama Robert akiwa anaketi katika sofa lilokuwa pembeni yake “Jamani wanangu haiwezekani mkapotea kwa kiasi hicho sisi ni wazazi wenu mnatakiwa kuja kutujulia hali mara kwa mara.Haya na huyo mwenzio yuko wapi mbona hamjaongozana” Aliuliza Mama Robert .

Jumamosi, Julai 20, 2013

SIMULIZI...KOSA LANGU NI LIPI....?...SEHEMU YA ....17........



ILIPOISHIA
Fredy alishangaa kusikia hivyo na kusema “Embu mkaribishe ndani”  Sukari ambaye muda wote alikuwa amenyamaza kimya aliingia ndani Fredy alimtizama huku akijiuliza maswali na nafsi yake "Mbona mimi huyu mtu simfahamu, na anamfahamu vipi mke wangu." Aliwaza na kumsalimia Sukari "Habari  yako, karibu sana, sijui ulikuwa na shida gani" Aliuliza Fredy huku Sukari akiwa anamtizama bila ya kuzungumza chochote. Je nini kitaendelea usikose ...SEHEMU ....YA 17.....

 INAPOENDELEA

Fredy kuona Sukari amenyamaza kimya, aliamua kuuliza tena “Vipi ndugu ulikuwa na shida gani?” Sukari alimtazama Fredy huku akionyesha tabasamu la kinafki “Sijui nianzie wapi ili unielewe nadhani Joyce angekuwepo ingekuwa vizuri zaidi, nafikiri wewe utakuwa ni mume wake." Aliuliza Sukari “ Ndiyo, Unaweza kuongea tu mimi ni mume wa Joyce, kwani ulikuwa unashida gani?Mbona unazungusha maneno, kama kuna jambo lolote unaweza kuniambia bila tatizo, karibu sana, tunaweza kusogea na kwenda kuketi sebuleni" Waliongozana na Fredy alimkaribisha vizuri Sukari.

Wakiwa pale sebuleni walianza mazungumzo "Karibu sana kaka, sijui nikusaidie kinywagi aina gani kuna soda, maji na juisi" Alisema Fredy huku akiwa anamtizama Sukari "Asante sana, ila sihitaji kinywaji chochote, jambo kubwa lililonileta hapa, ni kuonana na Joyce, ili..." Kabla hajamaliza kuzungumza Fredy alimkatisha na kusema "Joyce hayupo, lakini kama nilivyokueleza, mimi ni mume wake unaweza kunieleza jambo lolote na akirudi nitamfikishia ujumbe, kwani wewe ulikuwa na shida gani na mke wangu?".

Jumatano, Julai 17, 2013

SIMULIZI KOSA LANGU NI LIPI...? SEHEMU YA ......16........



 ILIPOISHIA
"Naomba unisamehe mume wangu, nilishindwa kukuambia  kutokana na kwamba sikupenda kabisa kukumbuka mateso niliyoyapata kipindi cha nyuma, nisamehe mume wangu, nakupenda sana kamwe siwezi kukuficha jambo lolote lile. JE NINI ....KITAENDELEA ....USIKOSE....SEHEMU ....YA .....16...

INAPOENDELEA
Zilipita kama siku mbili Joyce akiwa bado anasumbuliwa na Sukari kuhusu mtoto. Alikuwa na wasiwasi sana muda wote alikuwa hana raha. Huko hospitalini  hali ya mgonjwa haikuwa nzuri , hatimaye Maliki alifariki baada ya kuugua sana.Maisha yaliendelea siku moja Joyce aliamua kumpigia simu Lina ili amsaidie kuhusu matatizo aliyonayo lakini alipiga simu iliita bila ya mafanikio, na hata alipojaribu tena baadaye hakupokea, "Eeeh Mungu yaani huyu Lina kweli ananifanyia hivi angalau angepokea simu yangu basi" alisema Joyce huku akiinama chini na kutikisa kichwa kwa masikitiko mambo yalizidi kuwa mabaya kwa upande wa Joyce ambaye muda wote alikuwa anawaza nini kitatokea endapo mume wake akigundua mchezo mchafu alioufanya.

 Fredy alikuwa akihisi mke wake ana matatizo kutokana na namna ambavyo alikuwa akionyesha wasiwasi katika kila jambo akiwa kazini Fredy aliwaza “Hivi siku hizi mke wangu ana matatizo gani yaani simuelewi amekuwa mtu wa kuishi kwa wasiwasi sana. Leo nikirudi nyumbani itabidi nimuulize hadi aniambie nini kinachomsibu” Aliwaza  Fredy na baadaye alipotoka kazini ilikuwa mida ya saa moja jioni alifika nyumbani na kuingia bila ya kugonga mlango.

 Joyce alishtuka kumuona “Mama yangu umenishtua sana Fredy” Fredy alishangaa kumuona namna ambavyo Joyce alivyoshtuka na kusema “Sasa nimekushtua na kitu gani halafu wewe una matatizo sana embu keti hapo tuzungumze” Alihamaki Fredy huku akimuangalia kwa umakini mke wake Joyce taratibu alijisogeza na kuketi huku akisema “Yaani wewe huoni kama umenishtua umeingia bila ya kugonga mlango halafu unaniambia mimi nina matatizo sawa bwana” Alilalamika Joyce Fredy akamuuliza “Unajua kinachonishangaza ni mabadiliko ya tabia yako umekuwa mtu wamashaka mashaka sana siku hizi vipi una matatizo gani? Au kuna kitu unanificha”.

Jumamosi, Julai 13, 2013

KOSA LANGU NI LIPI...? SEHEMU YA ...15......



 ILIPOISHIA
“Wewe una kichaa mtoto si wa kwako tena naomba uondoke katika nyumba yangu kabla sijakuitia Polisi” Sukari akacheka kidogo na kusema “Halafu ukiwaita hao Polisi utakuwa umenisaidia sana, mimi naondoka lakini nitarudi hadi nihakikishe nampata mwanangu”....USIKOSE SEHEMU YA ....15......


INAPOENDELEA
Sukari aliondoka na kumuacha Joyce akiwa kama amechanganyikiwa  “Mungu wangu sijui nitafanyaje Fredy akigundua ataniua, na mambo yanazidi kuwa mabaya. Halafu leo jioni anarudi kutoka safari, sijui itakuwaje, naogopa sana Mungu wangu nisaidie.Hivi ni kwaninini Lina ameamua kunisaliti jamani yaani  amempa Sukari namba yangu ya simu? Sijui itakuwaje, yaani nimekwisha” Aliwaza Joyce.

Jioni ya siku hiyo Fredy alirudi kutoka safari. Alimkuta Joyce akiwa amekaa sebuleni “Mke wangu kipenzi habari za  masiku” Joyce kwa furaha alimsogelea Fredy na kumkumbatia “Karibu mume wangu, pole na uchovu wa safari,ni matumaini yangu umekuja na habari njema za huko” Fredy  huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake akasema  “ Habari za huko ni nzuri, lakini si kwema kuna taarifa nimezipata zinasikitisha sana” Joyce alishtuka akifikiri Fredy ameshaambiwa ukweli kuhuhusu mtoto wake.  Alishusha pumzi huku akionekana kujiumauma na sauti iliyojaa kigugumizi akasema “ Umesema kuna nini? Kwanini? Ilikuwaje?” Fredy alishangaa kumuona Joyce katika hali ile  "Vipi mama James mbona umeshtuka sana" Alihoji Fredy.

 "Hapana nilikuwa nataka kufahamu kuna nini? Eeeh kuna nini?" Alisema Joyce huku akiwa kama hajiamini  Fredy aliguna kidogo "Mmh wewe utakuwa una matatizo, sijawahi kukuona katika hali kama hiyo,habari nilizozipata za kusikitisha ni kuhusu  rafiki yangu yangu kipenzi ambaye tulipotezana kitambo,  amekamatwa na polisi, na kutokana na kutaka kuwashabulia polisi, basi wamempiga sana kabla ya kufikishwa kituoni na sasa ninavyozungumza nasikia hali yake ni mbaya" Joyce aliyekuwa akimsikiliza kwa umakini huku akitikisa kichwa akasema "Maskini kwani amefanya kosa gani?" "Huyu jamaa   kumbe alikuwa anajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya  kwa muda mrefu sana, kama unavyojua siku zote  siku za mwizi ni arobaini, hivyo polisi walipokwenda kumkamata kulikuwa na malumbano, na jamaa alikuwa anamiliki Bastola kinyume cha sheria, yaani ni kisa kirefu kwakweli”.

Jumatano, Julai 10, 2013

SIMULIZI....KOSA LANGU NI LIPI...SEHEMU YA ...14......


 ILIPOISHIA
“Vipi shemeji yupo” Joyce akamjibu “Hayupo amesafiri kikazi kama baada ya wikimbili ndiyo atarudi” Lina akaonyesha tabasamu na kusema “ Afadhali kama hayupo sasa sikiliza rafiki hapa nilipo nimekuja kwako jana nilikutana na Sukari anakutafuta yaani ananisumbua sana” Joyce alimwangalia Lina na kusema “ sitaki hata kulisikia hilo jina hapa nyumbani kwangu najuta sana kumsaliti mume wangu”..

INAPOENDELEA
 Kwa dharau Lina akacheka “unanichekesha kweli wewe hutaki kulisikia hilo jina wakati ni baba wa mtoto wako, bila yeye ungepata mtoto embu acha mambo ya kijinga, Sukari  atakusaidia upate na mtoto wa pili” Joyce kwa jazba akasema “ sikiliza nikuambie Lina mimi nilitenda kosa na siwezi kurudia kosa hata sikumoja. Tena naomba kama unataka urafiki wangu na wewe uendelee basi usinitajie huyo mtu hapa nilipo ni mjamzito kwa sasa na  hii mimba ni ya Fredy najuta kutokuwa na subira kwani mume wangu alikuwa na uwezo wa kunipa mimba”

Hahahahahah kicheko cha Lina “leo ndiyo unatambua kuwa ulitenda kosa.Sikiliza nikuambie Joyce mimi sina haja ya urafiki na wewe na ukicheza nitamwambia Sukari kuhusu mtoto wake tuone nani mjanja kati yangu mimi na wewe” aliongea huku akiwa ananyanyuka na kuondoka Joyce aliyekuwa amembeba mtoto wake alisema “siogopi chochote mwanga mkubwa wewe mwanamke una roho mbaya nia yako kunivurugia ndoa yangu” Lina aliondoka na kumuacha Joyce katika Dimbwi la mawazo. 

Baadaye  Lina aliondoka  huku akiendelea kutoa vitisho kwa Joyce kuwa atamueleza ukweli Sukari. Tokea siku hiyo Joyce hakuishi kwa amani alikuwa na hofu sana nini kitatokea iwapo Sukari akija kudai mtoto wake "Sijui nitafanya nini mimi Fredy atakapobaini ukweli najuta sana kutenda kosa hili" yalikuwa ni mawazo ya Joyce.  

Lina kutokana na tamaa ya pesa alimtafuta Sukari na kumueleza kila kitu kuhusu Joyce. kwamba kipindi yupo naye alipata ujauzito na alimweleza kuwa Joyce alimficha kwani nia yake ilikuwa apate mimba na amlee mtoto na mume wake.

Jumapili, Julai 07, 2013

KOSA LANGU NI LIPI ..SEHEMU YA ..13....


 

 ILIPOISHIA
Joyce alimsikiliza Mama Fredy kwa umakini na kusema "Lakini mama mbona unafika huko" Alilalama Joyce Mama Fredy akamjibu kwa sauti iliyojaa jazba "Huko wapi?Ahera au, tena sikiliza nikuambie fanya ufanyalo mimi nahitaji mjukuu. alaah! Hivi unafikiri hili jambo ni dogo eeh, mimi naondoka lakini tuliyoyazungumza hapa ukae nayo kichwani na uyafanyie kazi" Aliongea huku akiondoka na kumuacha Joyce akiwa ameketi pale sebuleni. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU YA ......13..

INAPOENDELEA

 Hali hiyo ilimuumiza sana Joyce. Baadaye aliamua kwenda kwa Lina na kumueleza hali halisi mambo yanavyoendelea. “Lina rafiki yangu nisaidie, naogopa kwenda Hospitali nina hofu maisha niliyopitia zamani, nadhani hata wewe unajua kuwa mimi nilikuwa nikitoa sana mimba.yawezekana ikawa ndiyo sababu.Na Fredy amenionyesha vipimo vyake yeye hana tatizo embu nishauri nifanyeje”.

 Lina aliguna kidogo na kusema “Sasa hapo rafiki mimi nakushauri jaribu kuwa na mwanamume mwingine uangalie kama utapata mimba” Joyce alishtuka na kusema “Wewe Lina yaani nimsaliti mume wangu? Hapana haiwezekani na tena yeye hana tatizo nahisi mimi ndiye mwenye matatizo.” Lina alicheka kidogo kwa dharau nakusema “Unanichekesha wewe, inamaana Joyce umeshakuwa na wanaume wangapi kipindi cha nyuma,  leo hii unaogopa kujaribu kuwa na mwanamume mmoja tu.” Joyce kwa sauti ya upole akasema "Usiseme hivyo Lina hayo mambo yalikuwa zamani nawala sikudhamiria kutenda zilikuwa ni shida tu, mimi sikupenda kuwa dada poa. Hata na hivyo nimeolewa na namuheshimu sana mume wangu" Alisema Joyce.

 "hahahaha unanichekesha wewe” Kilikuwa ni kicheko cha Lina huku akiendelea kusema  “Sikiliza nikuambie, kama kweli unataka kuendelea kuishi na Fredy jaribu kupata mimba nje kwani kila kitu kinawezekana, mbona hayo ni mambo ya kawaidia tu, vinginevyo unataka Fredy achukue mwanamke mwingine." Aliendelea kumshawishi mwisho wa siku Joyce alikubali kujaribu kwa shingo upande.

Akiwa nyumbani Joyce alikuwa akiwaza sana juu ya uamuzi wake wa kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine "Hili jambo ninalotaka kulifanya ni hatari sana, lakini sina namna inabidi nifanye hivi, ila  nafsi yangu inasita, kwani namsaliti mume wangu ila nikifikiria Fredy anaweza kutafuta mwanamke mwingine." Alikuwa akiwaza huku akijiuliza maswali aliyokuwa akijijibu mwenyewe.

Jumamosi, Juni 29, 2013

KOSA LANGU NI LIPI....? SURA YA ....11......



 ILIPOISHIA
Joyce aliyekuwa anakunywa Juisi kwa wakati huo alishusha glasi yake mezani. Kisha  alimkumbatia mpenzi wake kwa furaha “ Jamani Fredy nimefurahi kusikia hivyo, nami nakupenda sana nipo tayari maisha yangu niishi na wewe  katika shida na raha nakupenda sana mpenzi”  Basi ilikuwa ni furaha, waliendelea kuzungumza na baadaye waliondoka. Fredy alimrudisha Joyce nyumbani kwao wakiwa njiani Fredy alitoa ahadi ya kwenda kujitambulisha rasmi kwa kina Joyce mapema siku za usoni. JE NINI KITAENDELEA......USIKOSE SURA  YA......11

INAPOENDELEA
Alimfikisha Joyce nyumbani siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Joyce. Kutokana na namna ambavyo alikuwa akimpenda sana Fredy. Ilipita kama wiki moja Fredy aliamua kwenda kujitambulisha rasmi kwa walezi  wa Joyce.  Walimpokea na kumpa Baraka zote, hawakuwa na kipingamizi walitoa ushauri wao na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lolote watakalohitaji."Sisi hatuna kipingamizi alimradi mmependana, lakini kumbukeni maisha ya ndoa yanahitaji sana uvumilivu msisite kutushirikisha kwa lolote kwani ndoa si lele Mama".

 Alisema Baba Robert huku akiwatazama kwa macho ya mkazo Joyce na Fredy .  Mama Robert aliongeza kwa kusema "Ni kweli wanangu sisi tunaheshimu maamuzi yenu na tunawatakia kila la heri katika maisha yenu.Upendo na uaminifu iwe silaha muhimu sana kwenu.na pia msisahau kumshirikisha Mungu katika maisha yenu.
 
BAADA YA MWEZI MMOJA

 Tokea Fredy aende kujitambulisha kwa walezi wa Joyce. Mikakati ya ndoa ilianza haraka na hatimaye Joyce na Fredy walifunga pingu za maisha. Na sasa kuwa mke na mume. Joyce alianza maisha mapya ya ndoa. Walikuwa wakiishi maeneo ya Mikocheni katika nyumba ya Fredy, ilikuwa ni  nyumba nzuri sana, waliishi maisha yaliyojaa furaha na upendo. "Nafurahi sana kupata mke mwema na anayejua kumjali mume wake" Alisema Fredy akiwa anamuangalia Joyce aliyekuwa anaandaa chakula mezani. 

Alitabasamu na kusema "Jamani nakupenda pia mume wangu karibu ule chakula" Akionyesha uso wenye tabasamu Fredy alisema "Asante mke wangu na wewe nakuaminia kwa mapishi".Waliendelea kula na baadaye walielekea kupumzika.Maisha yaliendelea Joyce ilimbidi aache  kazi yake ya dukani aliyokuwa akiifanya katika duka la baba yake mkubwa. Alianza kusimamia biashara zake binafsi, ambazo mume wake alimfungulia. Maisha yalikuwa ya furaha sana.

Jumamosi, Juni 22, 2013

KOSA LANGU NI LIPI...? SURA YA .....9.......



 ILIPOISHIA
Ilikuwa ni majira ya  saa moja za jioni. Joyce alilia na kumuomba sana Maliki asiwafukuze lakini hakuswasikiliza, kwani yule mwanamke aliyekuja naye alikuwa hataki kina Joyce waendelee kuishi pale, hivyo hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuondoka. Huku wakifukuzwa kwa maneno ya kashfa.Bila  ya kujua wapi wanaenda walitembea huku na kule ili kutafuta sehemu ya kujipumzisha kwa usiku huo. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA....9....

 INAPOENDELEA


Walirudi katika maisha ya mitaani ambayo yalikuwa ni maisha ya shida sana. Kwasababu walikuwa hawana chochote zaidi ya kuomba huku na kule. Siku moja kutokana na kuishi maisha ya tabu  James alianza kuumwa homa. Lakini dada yake alikuwa hana pesa ya kununua dawa. Ilimbidi aombe watu ili wamsaidie, alipata msaada wa kununua dawa,  lakini siku zilivyozidi kwenda hali ya James ilizidi kuwa mbaya.  kutokana na hali halisi ya maisha Joyce alikuwa kama amechanganyikiwa akimtizama mdogo wake anavyoumwa “Nitafanya nini mimi, nimejaribu kutafuta pesa bila mafanikio na James anaumwa sana” Joyce ilimbidi aanze kujiuza ili apate pesa za kumpeleka mdogo wake Hospitalini. Alijiingiza katika biashara ya ukahaba ili aweze kupata pesa za mahitaji mbalimbali.

Wakati mwingine iliwabidi walale njaa kutokana na hali halisi ya maisha. Akiwa anaendelea na biashara hiyo alikutana na changamoto nyingi sana. Siku moja alikutana na mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa na umbo kubwa mithili ya mmbeba vyuma, alimchukua na kumuahidi kuwa angemlipa kiasi kikubwa cha fedha. Walipofika chumbani yule mwanaume alimtaka Joyce afanye naye mapenzi kinyume na maumbile lakini Joyce alikuwa akikataa “Sitaki, naomba uniache, unaniumiza jamani, sitaki siwezi mimi” Alikuwa akilalamika Joyce huku akijitoa mikononi mwa yule mwanaume bila mafanikio. Kwani aliambulia kipigo kikali sana, yule mwanaume alimpiga Joyce na kumlazimisha kufanya naye mapenzi kwa nguvu.Joyce alilia sana kwa uchungu. Baadaye yule kaka aliondoka bila hata ya kumlipa pesa yoyote na Joyce alibaki akilia kutokana na  maumivu makali sana aliyokuwa akiyasikia.

  Pesa alizokuwa anapata Joyce zilikuwa hazitoshi kuwasaidia na huku  hali ya James haikuwa nzuri hatimaye alifariki Dunia. ni siku ambayo Joyce alilia kwa uchungu bila ya kujua nani atamsaidia katika maisha yake. Alisaidiwa na watu mbalimbali wa mitaani katika mazishi ya mdogo wake  na baadaye alibaki pekee bila kujua ataenda kwa nani ili aweze kumsaidia.
  

Jumatano, Juni 19, 2013

SIMULIZI YA KOSA LANGU NI LIPI?.....SURA YA ....8.....



 ILIPOISHIA
Siku moja alikuja na mwanamke  hadi nyumbani. Ilikuwa ni usiku wa saa nne ambapo Joyce alikuwa bado hajalala akimsubiri Maliki arudi, mara Maliki akaingia na huyo mwanamke huku wakiwa wamekumbatiana Joyce hakuamini alichokuwa anakiona kwa mshangao alisema "Heee! Maliki! huyu ni nani?" Masikini Joyce misukosuko inazidi kumuandama. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA ....8......

INAPOENDELEA 

Wakati Joyce akiwa anashangaa kumuona Maliki akiwa na mwanamke tena huku wakiwa wamekumbatiana na kupeana mabusu motomoto. Bila ya kujali  chochote, Maliki alimgeukia Joyce na kusema "Hivi wewe una mamlaka gani ya kuniuliza huyu ni nani?" Joyce alimjibu kwa sauti ya upole "Kweli Maliki unanijibu kama hunijui? Nimekukosea nini mimi, unanifanyia yote haya. Umeona haitoshi kuwa na wanawake nje, umeamua kuwaleta kabisa na hapa ndani".

 Kwa dharau yule mwanamke aliyekuwa na Maliki alicheka na kumtizama Maliki huku akiwa anamshika kwenye paji la uso wake. "Mpenzi nimechoka sana jamani, huyu naye ni  nani? Mbona anaongea sana" Alisema yule mwanamke huku akionekana kujishebedua kwa maringo. Joyce kusikia hivyo alishikwa na hasira na kumsogelea yule mwanamke kwa nia ya kumpiga "Wewe unauliza mimi ni nani? mwendawazimu mkubwa usiye kuwa na haya kuchukua mabwana za watu" alisema Joyce huku akiwa amemkamata yule mwanamke ambaye alionekana ana umbo kubwa kuliko la Joyce. Wakati akiwa anafanya hivyo Maliki alimvuta na kumsukuma maskini Joyce alianguka chini huku akiwa analia kwa uchungu .


Jumamosi, Juni 08, 2013

SIMULIZI ....KOSA LANGU NI NINI....... SURA YA ....5........


ILIPOISHIA
Baada ya muda kupita mnamo saa sita usiku Joyce alikuwa bado amejilaza sebuleni na mlango wa sebuleni ulikuwa haujafungwa, Maliki alirudi usiku huo aliingia moja kwa moja  na kumkuta Joyce akiwa amelala kwenye kochi alisimama kwa muda pale mlangoni huku akimtazama Joyce kwa umakini na moyoni mwake akisema "mmmh huyu mtoto nampenda sana embu tizama alivyolala kama Malaika, mzuri sana huyu binti namtamani" JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA....5...

INAPOENDELEA 
Akiwa anawaza huku anasogea taratibu katika kochi alilokuwa  amelala.Joyce alikuwa amevalia gauni fupi, na kwa namna alivyokuwa amelala sehemu ya paja ilikuwa inaonekana basi Maliki alipofika alianza kumshika pajani Joyce huku akimpapasa taratibu Joyce alishtuka kutoka usingizini "Aaah jamani kaka Maliki umenishtua" .

Maliki alinyanyua mkono wake wa kulia na kumshika Joyce mikono yake miwili "Joyce mpenzi kwa nini unanitesa hivi si unajua kwa kiasi gani mimi nakupenda nahitaji penzi lako nakuomba unikubalie naahidi sintokuumiza nakupenda sana". Alisisitiza Maliki huku akimpapasa Joyce viganja vya mikono yake.
 Joyce aliyekuwa amejiinamia kwa  aibu alisema "Kaka Maliki mimi naogopa haiwezekani mimi bado mdogo,wewe niache mimi siwezi naomba unisamehe kama kuna jambo nimekukosea naomba uniache usinifanyie hivi mimi sitaki". Maliki aliyekuwa anaonekana amelegea macho huku akimtazama Joyce kwa matamanio  alimkumbatia Joyce kwa nguvu  "nikupe nini mpenzi nakupenda nikubalie ombi langu".

 Joyce huku akiwa  anatetemeka alijaribu kujivuta ili ajitoe mikononi mwa Maliki bila mafanikio. Akiwa anaendelea kujaribu kujitoa Maliki aliisogeza midomo yake karibu na midomo ya Joyce, na kuanza kumbusu kwa umakini kabisa aliendelea kumshikilia kwa nguvu baadaye alimbeba na kumpeleka Chumbani ambapo Joyce alibaki akilalamika "Kaka Maliki mimi naogopa naomba uniache unaniumiza" Alisema Joyce ambaye ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuwa katika mapenzi.

 Maliki aliyekuwa kama amechanganyikiwa hakumsikiliza aliendelea hadi alipomaliza alichokuwa anakitaka kwa Joyce baada ya kumaliza  akaanza kumbembeleza Joyce aliyekuwa akilia kwa maumivu makali "Pole mpenzi usijali mimi nakupenda Joyce usilie nyamaza mpenzi" Joyce aliendelea kulia baadaye aliondoka huku akichechemea kwa maumivu, alienda kuoga na kurudi chumbani kwake kulala huku moyoni akiwa anawaza "Siamini kama Kaka Maliki amenifanyia  kitendo kibaya hivi,sijui nitoroke na mdogo wangu, mimi siwezi kuishi haya maisha inaniuma sana, na je kama nitatoroka nitaenda wapi? Na sina mtu wa kunisaidia" Aliwaza Joyce huku akiwa analia kwa uchungu.

Wakati Joyce akiwa anaendelea kulia na kuwaza kama atoroke au aendelee kuishi katika nyumba ya Maliki, usingizi ulimpitia na kulala hadi mida ya saa moja asubuhi ambapo mdogo wake alikuja kubisha hodi ili kumuamsha dada yake, kwani ilikuwa siyo kawaida yake kulala hadi muda huo. Siku zote alikuwa akiamka mapema na kufanya kazi za pale nyumbani ikiwemo kumuandalia mdogo wake kifungua kinywa kabla ya kwenda shule.

Jumamosi, Juni 01, 2013

SIMULIZI ....KOSA LANGU NI LIPI..?....SURA YA .....3........




 ILIPOISHIA
Wakati huo Mama Joyce alikuwa  hajitambui walimuhamishia Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam  kuendelea na matibabu.  Huko nyumbani mazishi yalifanyika, vilio na simanzi vilitawala, watoto walilia sana kwa uchungu na hata kupoteza fahamu huku wakiwa hawajui nini hatima ya Mama yao mzazi. Hapo ndipo maisha ya Joyce na mdogo wake  yalianza kubadilika. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA...3..

INAPOENDELEA
Baada ya kumuhifadhi Marehemu kwenye makazi yake ya milele.Watu walitawanyika pale nyumbani na kuwaacha akina Joyce wakiwa na simanzi na wakati huo waliishi kwa kumtegemea Mzee Ngonyani na mke wake. Maisha yaliendelea huku baadhi ya watu ambao walikuwa ni majirani na marafiki wa karibu,  walitoa michango yao kwa ajili ya matibabu ya Mama Joyce ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Yule rafiki yake na marehemu Mzee Ndesanjo alirudi Dar es salaam baada ya mazishi ya mke wake. Akiwa anatokea  Morogoro alikuwa hajui hili wala lile, na  nini kimempata rafiki yake kipenzi. Kwani hata marafiki zake walimficha kwasababu naye pia alikuwa katika matatizo ya kufiwa na mke wake. Aliporudi Dar es salaam alienda  nyumbani kwa marehemu ili kumjulia hali, alipofika alimkuta Mama Ngonyani akiwa pamoja na Joyce wakiwa wanajiandaa kwenda Hospitali kumuona mgonjwa.

 Joyce alikuwa akimfahamu rafiki wa Baba yake ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Mzee Simba. Alipomuona akaanza kumfuata huku akilia kwa uchungu “Baba mdogo Baba mdogo, ulikuwa wapi Baba yangu amefariki na Mama anaumwa sana” Mzee Simba alimuangalia Joyce  kisha akasema  kwa mshtuko  "Eti nini! Mzee Ndesanjo amefariki haiwezekani jamani nini kilitokea, siamini mimi haya maneno” alizungumza huku akiwa amemshika mkono Joyce aliyekuwa analia kwa uchungu.

 Mama Ngonyani akamsimulia kila kitu kuhusu ajali waliyoipata marehemu Mzee Ndesanjo na mkewe wakati wakielekea msibani Morogoro, Mzee Simba  aliinama kwa uchungu na machozi yalimbubujika katika paji la uso wake. Alisikitika sana kumpoteza rafiki yake, "Siamini kilichotokea sasa kwanini walinificha jambo hili jamani  eeh Mungu ilaze roho ya marehemu mahali pema peponi".  Alisema Mzee Simba.Baadaye waliondoka pamoja hadi hospitalini kwenda kumjulia hali  Mama Joyce.


Jumapili, Mei 26, 2013

SIMULIZI YA KOSA LANGU NI NINI.....SURA YA .....1..........



“ Mungu naomba unisaidie maisha yangu yamekuwa na matatizo mengi kila ninalofanya linashindikana, sijui nikimbilie wapi nashindwa kuelewa kosa langu ni nini? nimepitia tabu nyingi sana, lakini bado maisha yangu sina raha siku zote mimi nimekuwa ni mtu wa kulia nisaidie Mungu wangu ”.

“Nimechoka sana leo na bado kuna kazi zinanisubiri halafu sijisikii vizuri nahisi nataka kuugua” ni maneno aliyokuwa akiwaza moyoni Mama Joyce ambaye alikuwa alikuwa akiosha vyombo, “Hii hali yangu  nahisi kama kuna jambo ambalo haliko sawa embu niandae chakula cha mchana Joyce na James wakirudi wakute nimekwisha waandalia chakula” Alinyanyuka na kuelekea jikoni kuandaa chakula.

Ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya saa kumi na mbili jioni Mzee Ndesanjo alikuwa akiendesha  gari aina ya Eskudo. Alifika nyumbani   na haraka alishuka ndani ya gari  kitendo cha kuingia ndani tu  alianza kuita kwa sauti "Mama Joyce Mama Joyce" huko chumbani Mama Joyce alimsikia na kuitika "Abeeee Mume wangu,vipi mbona mbiyo mbiyo hivyo "?  Alihoji  Mama Jocye huku akiwa anamuangalia mume wake kwa umakini.

 Mzee Ndesanjo ambaye ni mume wa Mama Joyce, alionekana kuwa na wasiwasi mwingi huku akimsisitiza mke wake ajiandae haraka "Hakuna muda wa kupoteza,  "Mimi ndani siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro, kuna matatizo yamejitokeza. Rafiki yangu Mzee Simba ambaye tunafanya kazi ofisi moja  amefiwa na mke wake wake inabidi tuwahi kwenda msibani”

Mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari kwani ile habari ilimshtua "Mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa! masikini" Aliongea kwa masikitiko  "Alikuwa anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke".  Mama Joyce akamjibu  "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani"? Aliuliza Mama Joyce.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom