ILIPOISHIA
Joyce aliinama chini kwa aibu "Mama naomba unisamehe sikukusudia kutenda yote haya ni shetani tu alinipitia nisaidie mama ni wewe pekee unaweza kuwa karibu na mimi" waliendelea kuzungumza baadaye mama Robert alinyanyuka na kuelekea chumbani huku akimtaka Joyce aende chumbani kwake akapumzike. ITAENDELEA INAPOENDELEA
Huko chumbani Joyce alikuwa akiwaza
"Eeee Mungu naomba unisaidie sijui Baba mkubwa akija atanifanya kitu gani, si anaweza kunifukuza hapa nyumbani, sijui nitaenda wapi mimi".
Nyumbani kwa Sukari alikuwa akiishi na dada zake
ambao ndiyo walikuwa wakimuangalia mtoto wa Joyce mmoja alikuwa akiitwa Samanda
na mwingine aliitwa Sungi siku hiyo walikuwa wamekaa pamoja kibarazani wakiteta
"Ndugu yangu Samanda hivi ukimuangalia huyu mtoto wa kaka unamuonaje?" Aliuliza Sungi "Mmmh na wewe kwani amefanyaje mi naona ni mtoto mpole hana
matatizo kwani wewe unamuonaje".
Alijibu na kuuliza Samanda huku akiguna kidogo, Sungi
akaendelea kusema "Yaani mimi huyu mtoto nikimuangalia tu naona kama si wa
kaka yetu kabisa mbona hata hafanani naye. "Huo sasa ni umbea ndugu yangu
mimi naona kawaida tu acha mambo ya kizamani kwahiyo asipofanana naye ndiyo
unamaanisha kuwa yawezekana kuwa huyu siyo mtoto wake" Alihoji Samanda
"Ndiyo, huyu mtoto siwakwake kaka amekurupuka tu" Sungi aliongea huku akijiamini. "Hee! Wewe
Sungi umechanganyikiwa, tena nyamaza kaka
asije kukusikia kwasababu anaweza hata akakufukuza hapa nyumbani".
Wakiwa
wanaendelea na mazungumzo Sukari alifika na kuwakuta lakini hakuwasikia walichokuwa wanazungumza "Habari za kushinda" "Salama tu kaka pole na kazi" Huku Sungi akinyanyuka na kumpokea mfuko
aliokuwa ameweka zawadi za mtoto James. Maisha yaliendelea huku Joyce akiwa
hajui nini muskabali wa maisha yake na alimfikiria pia Baba yake mkubwa
akigundua itakuwaje."Yaani najuta sana, kutenda kosa hili, Baba mkubwa akijua nahisi atanifukuza nyumbani kwake eeh Mungu nisaidie".
Ikiwa takribani kama wiki mbili tokea mtafaruku wote huo
utokee Joyce akiwa anaendelea kuishi nyumbani kwa Baba yake mkubwa bila amani kutokana na kuwa na mawazo sana alimkumbuka mtoto wake.Wakati wote huo Baba Robert alikuwa hayupo.
Siku moja Mama Robert akiwa ameketi Sebuleni akitizama tamthilia huku akiwa hana hili wala lile, mara ghafla Robert aliingia "Mama Mama
eeh Mungu wangu" Aliongea Robert kama amechanganyikiwa Mama yake alimshangaa kumuona katika hali ile, na kumuuliza "Wewe unawazimu? ni kitu gani, embu tulia kuna nini? "Baba
amefariki Mama Baba amegongwa na gari Mama"Robert alionekana kutetemeka huku kijasho chembamba kikimtoka katika paji la uso wake aliongea moja kwa moja huku Mama yake aliyekuwa ameketi alinyanyuka kwa mshtuko "Eti unasema nini wewe? eeeh ni nini, ajali nani eeh Mungu wangu".
Ghafla Mama Robert aliishiwa nguvu akaanguka chini na kupoteza fahamu. Joyce alikuwa kama amepigwa butwaa asijue nini cha kufanya huku akimtizama Robert "Wewe Robert umefanya nini jamani, angalia sasa Mama ameanguka, Mama,
Mama, amkaMama" aliongea kwa sauti iliyojaa wasiwasi mwingi. Lakini Mama
Robert alikuwa amezimia kwa mshtuko alioupata. Robert na Joyce walikimbia kwa majirani
kuomba msaada. Walikuja na haraka walimbeba Mama Robert kisha kumpeleka Hospitalini.
Baba robert alikuwa amepata ajali
mbaya iliyosababisha kifo chake palepale wakati akiwa anatokea safarini kurudi
nyumbani. Vilio na majonzi vilitawala katika familia ya kina Joyce taratibu za
mazishi zilianza huku Fredy akimsaidia Joyce na kusahau tofauti zilizopo baina
yao kwani kwa wakati huo Joyce alikuwa katika wakati Mgumu na hata kwa upande
wa Fredy Baba Robert alikuwa ni kama Baba yake mzazi.
Joyce alikuwa analia kwa
uchungu huku moyoni akiwaza "Eeh Mungu nakuomba umsaidie Mama arudi
katika hali yake ya kawaida. Ni balaa gani hili jamani Baba mkubwa ndiyo ametutoka, Mama naye hali yake siyo nzuri. Matatizo yamekuwa mengi "Akiwa anaendelea kuwaza Fredy aliyekuwa
anatembea huku na kule kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki alimuona na
kusogea karibu.
"Pole Joyce kwa matatizo ni mapenzi ya Mungu.Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi" Fredy alikuwa akimfariji, Joyce alikuwa akibubujikwa na machozi "Inaniuma sana Fredy
siamini kama Baba mkubwa amefariki na hali ya mama hospitalini bado si nzuri”
Aliongea kwa uchungu huku akimtazama Fredy aliyekuwa akimfariji, Huko
Hospitalini hali yaMama Robert
iliendelea kuwa mbaya kwani kipindi chote hicho alikuwa hajitambui.Kutokana na presha kuwa katika hali mbaya sana iliwabidi waendelee na taratibu za mazishi hivyo Baba Robert alizikwa
bila hata ya mke wake kuhudhuria.
Baada ya wiki moja tokea Baba Robert
apumzike kwenye makazi yake ya milele, Joyce pamoja na Robert waliendelea
kwenda Hospitalini ili kumjulia Mama hali “Mgonjwa anaendeleaje Daktari” Joyce
alimuhoji Daktari aliyekuwa akimuhudumia Mama Robert , “Karibuni ofisini
mgonjwa amepumzika mnaweza kuzungumza naye hapo baadaye. ITAENDELEA
Maoni 2 :
joyce mwaya pole.
dada adela samahani ujue namesoma hii story lkn nimetatufa part 1 na nyinginezo napata nusunusu hebu nambie nifanyeje nianze mwanzo wa story hiii mpaka mwisho?
Chapisha Maoni