Jumatatu, Oktoba 14, 2013

UJUMBE WA LEO KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA "NI UJINGA KUTOA PESA KWA MASIKINI NA KUPELEKA KWA MATAJIRI"

Mwalimu Nyerere alikuwa akisisitiza suala la elimu, malezi, utamaduni na mazingira. Mchango wake unaonekana na unapaswa kuendelezwa na kuenziwa na siyo kupuuzwa.


ALIWAHI KUSEMA "Taifa lisilokubali kutaabika kwa faida yake lenyewe bila shaka litataabishwa kwa faida ya wengine" Je, kama wananchi tulizubaa na kitaifa tukapuuza kuwajibika au kutaabika kwa faida yetu, bado tutaendelea kukubali kutaabishwa au kuwajibishwa kwa faida ya wengine?

Iko wapi ari yetu ya kuwa Taifa linalokubali kutaabika kwa faida yake na si kutaabishwa kwa faida ya wengine? Naamini, dhamira hii ndiyo iliyokuwa imeshibisha mioyo ya wazalendo waliokuwa wakipigania Uhuru  Nani ameitia mfukoni dhamira hii?


MILELE DAIMA TUTAMKUMBUKA BABA WA TAIFA

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom