Pages

Jumatano, Juni 19, 2013

SIMULIZI YA KOSA LANGU NI LIPI?.....SURA YA ....8..... ILIPOISHIA
Siku moja alikuja na mwanamke  hadi nyumbani. Ilikuwa ni usiku wa saa nne ambapo Joyce alikuwa bado hajalala akimsubiri Maliki arudi, mara Maliki akaingia na huyo mwanamke huku wakiwa wamekumbatiana Joyce hakuamini alichokuwa anakiona kwa mshangao alisema "Heee! Maliki! huyu ni nani?" Masikini Joyce misukosuko inazidi kumuandama. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA ....8......

INAPOENDELEA 

Wakati Joyce akiwa anashangaa kumuona Maliki akiwa na mwanamke tena huku wakiwa wamekumbatiana na kupeana mabusu motomoto. Bila ya kujali  chochote, Maliki alimgeukia Joyce na kusema "Hivi wewe una mamlaka gani ya kuniuliza huyu ni nani?" Joyce alimjibu kwa sauti ya upole "Kweli Maliki unanijibu kama hunijui? Nimekukosea nini mimi, unanifanyia yote haya. Umeona haitoshi kuwa na wanawake nje, umeamua kuwaleta kabisa na hapa ndani".

 Kwa dharau yule mwanamke aliyekuwa na Maliki alicheka na kumtizama Maliki huku akiwa anamshika kwenye paji la uso wake. "Mpenzi nimechoka sana jamani, huyu naye ni  nani? Mbona anaongea sana" Alisema yule mwanamke huku akionekana kujishebedua kwa maringo. Joyce kusikia hivyo alishikwa na hasira na kumsogelea yule mwanamke kwa nia ya kumpiga "Wewe unauliza mimi ni nani? mwendawazimu mkubwa usiye kuwa na haya kuchukua mabwana za watu" alisema Joyce huku akiwa amemkamata yule mwanamke ambaye alionekana ana umbo kubwa kuliko la Joyce. Wakati akiwa anafanya hivyo Maliki alimvuta na kumsukuma maskini Joyce alianguka chini huku akiwa analia kwa uchungu .
Maliki alimsogelea na kusema "Unataka kujifanya wewe ni kichaa? Nitakufukuza pakashume mkubwa wewe, nimekuokota huko barabarani unataka kujifanya unayomamlaka ya hii nyumba? Maskini mkubwa wewe" aliongea maneno hayo Maliki bila hata ya huruma. Joyce alibaki analia na Maliki akamchukua yule mwanamke wake wakaelekea chumbani kulala na kumuacha Joyce akiwa anaendelea kulia. Mdogo wake Joyce alikuwa amelala lakini alishtuka baada ya kusikia malumbano yakiwa yanaendelea. Alitoka chumbani na kuelekea sebuleni ambapo alimkuta dada  yake analia. Alimsogelea kwa masikitiko huku akiwa anafikicha macho kutokana na usingizi.

"Kuna nini dada mbona  unalia hivi,  mimi nimechoka kila siku unalia bora tuondoke" Alisema James huku akiwa anamuangalia dada yake ambaye alinyanyuka na kumshika mdogo wake huku akisema " Hapana mdogo wangu usijali mimi niko sawa" James kwa hasira akamwambia " huwezi kunidanganya dada nimesikia kila kitu shemeji Maliki anakunyanyasa sana, bora tuondoke kama ni shule hata mimi nitaacha tuondoke dada" aliongea James huku machozi yakiwa yana mlengalenga ".
 Joyce alinyamaza kimya akamshika mdogo wake na kuelekea chumbani. Siku hiyo Joyce alilala na mdogo wake hadi asubuhi.Alipoamka  hakumkuta  Maliki alikuwa ameondoka na yule mwanamke.Ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Joyce aliyekuwa na mawazo na masikitiko. Zilipita kama siku mbili akiwa anaendelea kuishi maisha ya shida, Joyce alijigundua kuwa ni mjamzito kwa mara nyingine. kitu ambacho kilimuumiza sana kichwa kwa mawazo,  kuwa  atafanya nini, ilimbidi amueleze Maliki hali halisi ambapo kama kawaida Maliki alimtaka aitoe hiyo mimba.
 

Joyce aliyekuwa hana la kufanya zaidi ya kumsikiliza Maliki  kile alichokuwa anataka. Baada ya siku mbili tatu aliitoa tena ile mimba na kurudi nyumbani, huku akiwa anaishi kwa mateso bila kujua nini hatima ya maisha yake. Kila kukicha kwa Maliki vituko vilikuwa haviishi.Siku moja Joyce akiwa amelala chumbani aliwaza moyoni mwake na kusema "Hivi nini hatima ya maisha yangu si nitakufa mimi napigwa sana,nikipata mimba natoa, Eee Mungu naomba unisaidie, sitaki James ateseke angalau yeye angesoma, lakini nitaweza kweli kuendelea kuishi katika hali hii si nitakufa nimuache mdogo wangu akiteseka" Aliwaza Joyce huku akiwa analia kwa uchungu.

Maisha yaliendelea hadi siku moja mida ya jioni ambapo siku hiyo Maliki alikuja na mwanamke mwingine tena na kumtaka Joyce na mdogo wake waondoke. Ilikuwa ni majira ya  saa moja za jioni. Joyce alilia na kumuomba sana Maliki asiwafukuze lakini hakuswasikiliza, kwani yule mwanamke aliyekuja naye alikuwa hataki kina Joyce waendelee kuishi pale, hivyo hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuondoka. Huku wakifukuzwa kwa maneno ya kashfa.Bila  ya kujua wapi wanaenda walitembea huku na kule ili kutafuta sehemu ya kujipumzisha kwa usiku huo. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA....9....

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Malik htalaanika hatopta watto wala.mke mwema

Bila jina alisema ...

imenigusa, Dunia hii ina mambo magumu hasa mtu ukosa wazazi

Bila jina alisema ...

Jamani Joyce asijali Mungu atamsaidia tu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom