ILIPOISHIA
Joyce aliyekuwa anakunywa Juisi kwa wakati huo
alishusha glasi yake mezani. Kisha alimkumbatia mpenzi wake kwa furaha “
Jamani Fredy nimefurahi kusikia hivyo, nami nakupenda sana nipo tayari maisha
yangu niishi na wewe katika shida na raha
nakupenda sana mpenzi” Basi ilikuwa ni
furaha, waliendelea kuzungumza na baadaye waliondoka. Fredy alimrudisha Joyce
nyumbani kwao wakiwa njiani Fredy alitoa ahadi ya kwenda kujitambulisha rasmi
kwa kina Joyce mapema siku za usoni. JE NINI KITAENDELEA......USIKOSE SURA YA......11
INAPOENDELEA
Alimfikisha Joyce nyumbani siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa
Joyce. Kutokana na namna ambavyo alikuwa akimpenda sana Fredy. Ilipita kama
wiki moja Fredy aliamua kwenda kujitambulisha rasmi kwa walezi wa Joyce.
Walimpokea na kumpa Baraka zote, hawakuwa na kipingamizi walitoa ushauri wao na
kuahidi kutoa ushirikiano kwa lolote watakalohitaji."Sisi hatuna
kipingamizi alimradi mmependana, lakini kumbukeni maisha ya ndoa yanahitaji
sana uvumilivu msisite kutushirikisha kwa lolote kwani ndoa si lele Mama".
Alisema Baba Robert huku akiwatazama kwa macho ya mkazo Joyce na Fredy . Mama Robert aliongeza kwa kusema "Ni
kweli wanangu sisi tunaheshimu maamuzi yenu na tunawatakia kila la heri katika
maisha yenu.Upendo na uaminifu iwe silaha muhimu sana kwenu.na pia msisahau
kumshirikisha Mungu katika maisha yenu.
BAADA YA MWEZI MMOJA
Tokea Fredy aende kujitambulisha
kwa walezi wa Joyce. Mikakati ya ndoa ilianza haraka na hatimaye Joyce na Fredy
walifunga pingu za maisha. Na sasa kuwa mke na mume. Joyce alianza maisha mapya
ya ndoa. Walikuwa wakiishi maeneo ya Mikocheni katika nyumba ya Fredy, ilikuwa
ni nyumba nzuri sana, waliishi maisha
yaliyojaa furaha na upendo. "Nafurahi sana kupata mke mwema na anayejua
kumjali mume wake" Alisema Fredy akiwa anamuangalia Joyce aliyekuwa
anaandaa chakula mezani.
Alitabasamu na kusema "Jamani nakupenda pia mume
wangu karibu ule chakula" Akionyesha uso wenye tabasamu Fredy alisema
"Asante mke wangu na wewe nakuaminia kwa mapishi".Waliendelea kula na
baadaye walielekea kupumzika.Maisha yaliendelea Joyce ilimbidi aache kazi
yake ya dukani aliyokuwa akiifanya katika duka la baba yake mkubwa. Alianza
kusimamia biashara zake binafsi, ambazo mume wake alimfungulia. Maisha yalikuwa
ya furaha sana.
Ilipita kama miaka miwili tokea
wafunge ndoa. Siku hiyo Fredy alikuwa ametoka kazini akiwa amechoka sana. Alimkuta
mke wake akiandaa chakula cha jioni na kusema “Habari za hapa Joyce” Joyce
alionyesha tabasamu mwananana usoni na kusema “Nzuri mume wangu kipenzi, pole
na kazi”
Fredy aliitika kwa unyonge, huku akiwa anaketi katika kochi pale sebuleni “Joyce alimuangalia Fredy na kuhisi labda kutakuwa kuna tatizo. Kwani alikuwa amechoka sana na alionekana mwingi wa mawazo. Joyce alijisogeza na kuketi karibu “Vipi mpenzi unaonekana umechoka sana leo ungeenda kukoga kwanza” Fredy alimtazama Joyce kisha akamwambia usijali Joyce kuna kitu nataka tuzungumze”
Fredy aliitika kwa unyonge, huku akiwa anaketi katika kochi pale sebuleni “Joyce alimuangalia Fredy na kuhisi labda kutakuwa kuna tatizo. Kwani alikuwa amechoka sana na alionekana mwingi wa mawazo. Joyce alijisogeza na kuketi karibu “Vipi mpenzi unaonekana umechoka sana leo ungeenda kukoga kwanza” Fredy alimtazama Joyce kisha akamwambia usijali Joyce kuna kitu nataka tuzungumze”
Joyce alivuta pumzi kwa umakini na kusema “Sawa mume wangu, vipi lakini
kuna tatizo” Fredy akamjibu ndiyo kuna tatizo, inamaana wewe huoni kama kuna
tatizo? Joyce mke wangu tumeishi kwenye ndoa ni miaka miwili hakuna
ujauzito wala mtoto wewe huoni kama hili ni tatizo”. Alihoji Fredy. Joyce
alinyamaza kimya kidogo na kusema “Lakini
hilo siyo tatizo Fredy, kwani bado muda upo, Mungu atatusaidia tutapatamtoto”
Fredy aligeuka na kusema “Natamani sana kuwa na mtoto Joyce, haina haja ya kuvuta subira huu ni muda muafaka tufanye vyovyote lakini tupate mtoto” Aliongea Fredy huku akinyanyuka kuelekea chumbani. Joyce alibaki pale sebuleni akiwaza “Mmh sijui itakuwaje, eeh Mungu nisaidie, hata mimi natamani sana kupata mtoto” alinyanyuka na kuendelea na shughuli za pale nyumbani.
Fredy aligeuka na kusema “Natamani sana kuwa na mtoto Joyce, haina haja ya kuvuta subira huu ni muda muafaka tufanye vyovyote lakini tupate mtoto” Aliongea Fredy huku akinyanyuka kuelekea chumbani. Joyce alibaki pale sebuleni akiwaza “Mmh sijui itakuwaje, eeh Mungu nisaidie, hata mimi natamani sana kupata mtoto” alinyanyuka na kuendelea na shughuli za pale nyumbani.
Kesho yake Joyce aliamua kwenda kumtembelea
rafiki yake maeneo ya kinondoni aliyekuwa anaitwa Lina. Alipofika alimkuta Lina
ameketi kibarazani anapunga upepo. Lina
alipomuona Jocye alisimama na kusema “Hee leo umepotea njia” Joyce alicheka
kidogo na kusema “Lina na wewe hata salamu” Lina akamjibu “Mwenzangu
nimeshangaa kukuona. hatujaonana siku nyingi au ndiyo shemeji anakuficha” Baadaye
alimkaribisha ndani na kumpatia kinywaji, na waliendelea kuzungumza “Eeh rafiki
yangu, niambie za huko kwako vipi shemeji mzima” Alisema Lina.Joyce alinyamaza kimya kidogo na kujibu “Mzima lakini huko si kwema sana,
nina tatizo kidogo”. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA.....12.......
Maoni 6 :
Daaah! maskini joyce anaanza kupata suluba ya kukosa mtoto. ee mola uwe naye ukamsikilize kilio chake,,..!
Da adela umenikoshaje sasa nilivyoona jina languuuu,teh teh teh teh teh,Mdau no 1.uwiiiiiiiiiiii maskn ila naomba nimshauri vzr,asijl htapta mtto tu.
God bless Joyce. She z innocent
kwel mwaka wa hasara hasara.
ASANTENI SANA WADAU KWA KUENDELEA KUWA NAMI
umenifurahisha sana umeweka jina langu na rafiki yangu pia. ok nahisi tatizo ni mwanaume.
Chapisha Maoni