Jumamosi, Juni 29, 2013

KOSA LANGU NI LIPI....? SURA YA ....11......



 ILIPOISHIA
Joyce aliyekuwa anakunywa Juisi kwa wakati huo alishusha glasi yake mezani. Kisha  alimkumbatia mpenzi wake kwa furaha “ Jamani Fredy nimefurahi kusikia hivyo, nami nakupenda sana nipo tayari maisha yangu niishi na wewe  katika shida na raha nakupenda sana mpenzi”  Basi ilikuwa ni furaha, waliendelea kuzungumza na baadaye waliondoka. Fredy alimrudisha Joyce nyumbani kwao wakiwa njiani Fredy alitoa ahadi ya kwenda kujitambulisha rasmi kwa kina Joyce mapema siku za usoni. JE NINI KITAENDELEA......USIKOSE SURA  YA......11

INAPOENDELEA
Alimfikisha Joyce nyumbani siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Joyce. Kutokana na namna ambavyo alikuwa akimpenda sana Fredy. Ilipita kama wiki moja Fredy aliamua kwenda kujitambulisha rasmi kwa walezi  wa Joyce.  Walimpokea na kumpa Baraka zote, hawakuwa na kipingamizi walitoa ushauri wao na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lolote watakalohitaji."Sisi hatuna kipingamizi alimradi mmependana, lakini kumbukeni maisha ya ndoa yanahitaji sana uvumilivu msisite kutushirikisha kwa lolote kwani ndoa si lele Mama".

 Alisema Baba Robert huku akiwatazama kwa macho ya mkazo Joyce na Fredy .  Mama Robert aliongeza kwa kusema "Ni kweli wanangu sisi tunaheshimu maamuzi yenu na tunawatakia kila la heri katika maisha yenu.Upendo na uaminifu iwe silaha muhimu sana kwenu.na pia msisahau kumshirikisha Mungu katika maisha yenu.
 
BAADA YA MWEZI MMOJA

 Tokea Fredy aende kujitambulisha kwa walezi wa Joyce. Mikakati ya ndoa ilianza haraka na hatimaye Joyce na Fredy walifunga pingu za maisha. Na sasa kuwa mke na mume. Joyce alianza maisha mapya ya ndoa. Walikuwa wakiishi maeneo ya Mikocheni katika nyumba ya Fredy, ilikuwa ni  nyumba nzuri sana, waliishi maisha yaliyojaa furaha na upendo. "Nafurahi sana kupata mke mwema na anayejua kumjali mume wake" Alisema Fredy akiwa anamuangalia Joyce aliyekuwa anaandaa chakula mezani. 

Alitabasamu na kusema "Jamani nakupenda pia mume wangu karibu ule chakula" Akionyesha uso wenye tabasamu Fredy alisema "Asante mke wangu na wewe nakuaminia kwa mapishi".Waliendelea kula na baadaye walielekea kupumzika.Maisha yaliendelea Joyce ilimbidi aache  kazi yake ya dukani aliyokuwa akiifanya katika duka la baba yake mkubwa. Alianza kusimamia biashara zake binafsi, ambazo mume wake alimfungulia. Maisha yalikuwa ya furaha sana.


 Ilipita kama miaka miwili tokea wafunge ndoa. Siku hiyo Fredy alikuwa ametoka kazini akiwa amechoka sana. Alimkuta mke wake akiandaa chakula cha jioni na kusema “Habari za hapa Joyce” Joyce alionyesha tabasamu mwananana usoni na kusema “Nzuri mume wangu kipenzi, pole na kazi”

 Fredy aliitika kwa unyonge,  huku akiwa anaketi katika kochi pale sebuleni “Joyce alimuangalia Fredy na kuhisi labda kutakuwa kuna tatizo. Kwani alikuwa amechoka sana na alionekana mwingi wa mawazo. Joyce alijisogeza na kuketi karibu “Vipi mpenzi unaonekana umechoka sana leo ungeenda kukoga kwanza” Fredy alimtazama Joyce kisha akamwambia usijali Joyce kuna kitu nataka tuzungumze”

Joyce alivuta pumzi kwa umakini na kusema “Sawa mume wangu, vipi lakini kuna tatizo” Fredy akamjibu ndiyo kuna tatizo, inamaana wewe huoni kama kuna tatizo? Joyce mke wangu tumeishi  kwenye ndoa ni miaka miwili hakuna ujauzito wala mtoto wewe huoni kama hili ni tatizo”. Alihoji Fredy.  Joyce alinyamaza kimya kidogo na kusema  “Lakini hilo siyo tatizo Fredy, kwani bado muda upo, Mungu atatusaidia tutapatamtoto”


 Fredy aligeuka na kusema “Natamani sana kuwa na mtoto Joyce, haina haja ya kuvuta subira huu ni muda muafaka tufanye vyovyote lakini tupate mtoto” Aliongea Fredy huku akinyanyuka kuelekea chumbani. Joyce alibaki pale sebuleni  akiwaza “Mmh sijui itakuwaje, eeh Mungu nisaidie, hata mimi natamani sana kupata mtoto” alinyanyuka na kuendelea na shughuli za pale nyumbani.

Kesho yake Joyce aliamua kwenda kumtembelea rafiki yake maeneo ya kinondoni aliyekuwa anaitwa Lina. Alipofika alimkuta Lina ameketi  kibarazani anapunga upepo. Lina alipomuona Jocye alisimama na kusema “Hee leo umepotea njia” Joyce alicheka kidogo na kusema “Lina na wewe hata salamu” Lina akamjibu “Mwenzangu nimeshangaa kukuona. hatujaonana siku nyingi au ndiyo shemeji anakuficha” Baadaye alimkaribisha ndani na kumpatia kinywaji, na waliendelea kuzungumza “Eeh rafiki yangu, niambie za huko kwako vipi shemeji mzima” Alisema Lina.Joyce alinyamaza kimya kidogo na kujibu “Mzima lakini huko si kwema sana, nina tatizo kidogo”. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA.....12.......

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

Daaah! maskini joyce anaanza kupata suluba ya kukosa mtoto. ee mola uwe naye ukamsikilize kilio chake,,..!

Bila jina alisema ...

Da adela umenikoshaje sasa nilivyoona jina languuuu,teh teh teh teh teh,Mdau no 1.uwiiiiiiiiiiii maskn ila naomba nimshauri vzr,asijl htapta mtto tu.

Unknown alisema ...

God bless Joyce. She z innocent

Unknown alisema ...

kwel mwaka wa hasara hasara.

ADELA KAVISHE alisema ...

ASANTENI SANA WADAU KWA KUENDELEA KUWA NAMI

Bila jina alisema ...

umenifurahisha sana umeweka jina langu na rafiki yangu pia. ok nahisi tatizo ni mwanaume.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom