ILIPOISHIA
"Naomba
unisamehe mume wangu, nilishindwa kukuambia kutokana na kwamba
sikupenda kabisa kukumbuka mateso niliyoyapata kipindi cha nyuma,
nisamehe mume wangu, nakupenda sana kamwe siwezi kukuficha jambo lolote
lile. JE NINI ....KITAENDELEA ....USIKOSE....SEHEMU ....YA .....16...
INAPOENDELEA
Zilipita kama siku mbili Joyce akiwa bado anasumbuliwa na Sukari kuhusu
mtoto. Alikuwa na wasiwasi sana muda wote alikuwa hana raha. Huko hospitalini hali ya mgonjwa haikuwa nzuri , hatimaye Maliki alifariki baada ya kuugua sana.Maisha
yaliendelea siku moja Joyce aliamua kumpigia simu Lina ili amsaidie kuhusu
matatizo aliyonayo lakini alipiga simu iliita bila ya mafanikio, na hata
alipojaribu tena baadaye hakupokea, "Eeeh Mungu yaani huyu Lina kweli
ananifanyia hivi angalau angepokea simu yangu basi" alisema Joyce huku
akiinama chini na kutikisa kichwa kwa masikitiko mambo yalizidi kuwa mabaya kwa
upande wa Joyce ambaye muda wote alikuwa anawaza nini kitatokea endapo mume
wake akigundua mchezo mchafu alioufanya.
Fredy alikuwa akihisi mke wake ana matatizo kutokana na namna
ambavyo alikuwa akionyesha wasiwasi katika kila jambo akiwa kazini Fredy
aliwaza “Hivi siku hizi mke wangu ana matatizo gani yaani simuelewi amekuwa mtu
wa kuishi kwa wasiwasi sana. Leo nikirudi nyumbani itabidi nimuulize hadi
aniambie nini kinachomsibu” Aliwaza Fredy na baadaye alipotoka kazini
ilikuwa mida ya saa moja jioni alifika nyumbani na kuingia bila ya kugonga
mlango.
Joyce alishtuka kumuona “Mama yangu umenishtua sana Fredy” Fredy
alishangaa kumuona namna ambavyo Joyce alivyoshtuka na kusema “Sasa nimekushtua
na kitu gani halafu wewe una matatizo sana embu keti hapo tuzungumze” Alihamaki
Fredy huku akimuangalia kwa umakini mke wake Joyce taratibu alijisogeza na
kuketi huku akisema “Yaani wewe huoni kama umenishtua umeingia bila ya kugonga
mlango halafu unaniambia mimi nina matatizo sawa bwana” Alilalamika Joyce Fredy
akamuuliza “Unajua kinachonishangaza ni mabadiliko ya tabia yako umekuwa mtu
wamashaka mashaka sana siku hizi vipi una matatizo gani? Au kuna kitu
unanificha”.
Joyce alimtazama Fredy kwa macho ya upole na kusema “Nina mashaka?
Hapana mume wangu mbona mimi nipo sawa sina matatizo yoyote” Fredy akacheka
kidogo na kusema “Wewe ndiye unajiona uko sawa mimi nakujua vizuri sana mke
wangu. Huwezi kunidanganya kuwa hauna matatizo haya hebu niambie ukweli sitaki
unifiche kitu kama kuna tatizo kuwa muwazi” Joyce aliendelea kudanganya na
kusema “mimi sina matatizo niko sawa jamani mume wangu kama kuna tatizo kwanini
nikufiche” Fredy aliguna kidogo na kusema “Sawa kama hakuna tatizo mimi naingia
ndani niandalie maji ya kuoga” aliongea huku akiwa anaelekea chumbani.
Joyce alibaki akiwa na wasiwasi na kuelekea kumuandalia maji ya kuoga
mume wake. Kwa upande wa Sukari alipanga namna ya kuja kumuumbua Joyce kama
ataendelea kukaidi kumtambulisha kwa mtoto wake. "Yaani haiwezekani kabisa, mimi mwanaume mzima na akili zangu, mtoto wangu analelewa na baba mwingine, hivi huyu Joyce ananionaje, siwezi kukubali hata kidogo lazima nimchukue mtoto wangu. yaani wanawake wengine ni watu wa ajabu sana. Aliwaza Sukari huku akionekana kuwa na hasira nyingi.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya
Jumatatu ambapo Joyce alikuwa katika shughuli zake za kibiashara na mume wake
Fredy alikuwa nyumbani kwani siku hiyo alikuwa amewahi sana kutoka kazini
ilikuwa ni mida ya saa nane za mchana Sukari alifika nyumbani Kwa Joyce na
kugonga geti.
Mlinzi wa getini alifungua na kumuona Sukari “Ni wewe tena, umefuata nini?
hakuna kuingia hapa, ishia hapohapo. Mama mwenye nyumba alisema hata siku moja
nisikufungulie geti” Alisema mlinzi kwa sauti kali, akiwa anazungumza Fredy alimsikia
kwasababu alikuwa maeneo ya karibu na kwenye geti akauliza “Kuna nini hapo? Nani unabishana naye, mkaribishe ndani” mlinzi akamjibu “Huyu kijana kuna siku alikuja
walikuwa wakigombana na Mama kwahiyo Mama alisema hata sikumoja nisimfungulie
geti, vinginevyo atanifukuza kazi”.
Fredy alishangaa kusikia hivyo na kusema
“Embu mkaribishe ndani” Sukari ambaye muda wote alikuwa amenyamaza kimya
aliingia ndani Fredy alimtizama huku akijiuliza maswali na nafsi yake "Mbona mimi huyu mtu simfahamu, na anamfahamu vipi mke wangu." Aliwaza na kumsalimia Sukari "Habari yako, karibu sana, sijui ulikuwa na shida gani" Aliuliza Fredy huku Sukari akiwa anamtizama bila ya kuzungumza chochote. Je nini kitaendelea usikose ...SEHEMU ....YA 17.....
Maoni 6 :
Ehee mungu naomba waende wakapime. DNA akute si mtt wake akome. Kiherehere cha kumsumbua Joyce na. Lina haaibike
mhhhhhhhhhhh am sure sukari hataumbuka,mna naic uyo mtto hajafanana nae,lina nae hatkufa mdomo wazi.
Daaaaaaah! siamini macho yangu, hapo siongei nakaa pembeni kusikilizia mchezo unavyoendelea.
He! he! he! he! he! he! he! ukisikia kufa kwa nyani miti yote huteleza ndo hapo, na hapo lazima miti yote ya joyce lzm iteleze tu.
"Assalale mtume wangu! hapo kapatikana"
"Yesu na maria,! mungu na mtume!" udanganyifu wake umefikia mwisho. akumbuke kuwa uongo haufai katika ndoa.
Chapisha Maoni