ILIPOISHIA
Ilikuwa ni majira ya saa moja za jioni. Joyce alilia na kumuomba sana Maliki asiwafukuze lakini hakuswasikiliza, kwani yule mwanamke aliyekuja naye alikuwa hataki kina Joyce waendelee kuishi pale, hivyo hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuondoka. Huku wakifukuzwa kwa maneno ya kashfa.Bila ya kujua wapi wanaenda walitembea huku na kule ili kutafuta sehemu ya kujipumzisha kwa usiku huo. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA....9....
INAPOENDELEA
Walirudi katika maisha ya mitaani ambayo yalikuwa ni maisha ya shida sana.
Kwasababu walikuwa hawana chochote zaidi ya kuomba huku na kule. Siku moja
kutokana na kuishi maisha ya tabu James alianza kuumwa homa. Lakini dada
yake alikuwa hana pesa ya kununua dawa. Ilimbidi aombe watu ili wamsaidie, alipata
msaada wa kununua dawa, lakini siku
zilivyozidi kwenda hali ya James ilizidi kuwa mbaya. kutokana na hali halisi ya maisha Joyce
alikuwa kama amechanganyikiwa akimtizama mdogo wake anavyoumwa “Nitafanya nini
mimi, nimejaribu kutafuta pesa bila mafanikio na James anaumwa sana” Joyce
ilimbidi aanze kujiuza ili apate pesa za kumpeleka mdogo wake Hospitalini. Alijiingiza
katika biashara ya ukahaba ili aweze kupata pesa za mahitaji mbalimbali.
Wakati mwingine iliwabidi walale njaa kutokana na hali halisi ya maisha. Akiwa
anaendelea na biashara hiyo alikutana na changamoto nyingi sana. Siku moja
alikutana na mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa na umbo kubwa mithili ya mmbeba vyuma,
alimchukua na kumuahidi kuwa angemlipa kiasi kikubwa cha fedha. Walipofika
chumbani yule mwanaume alimtaka Joyce afanye naye mapenzi kinyume na maumbile
lakini Joyce alikuwa akikataa “Sitaki, naomba uniache, unaniumiza jamani,
sitaki siwezi mimi” Alikuwa akilalamika Joyce huku akijitoa mikononi mwa yule
mwanaume bila mafanikio. Kwani aliambulia kipigo kikali sana, yule mwanaume
alimpiga Joyce na kumlazimisha kufanya naye mapenzi kwa nguvu.Joyce alilia sana
kwa uchungu. Baadaye yule kaka aliondoka bila hata ya kumlipa pesa yoyote na
Joyce alibaki akilia kutokana na maumivu
makali sana aliyokuwa akiyasikia.
Pesa alizokuwa anapata Joyce zilikuwa hazitoshi kuwasaidia na huku
hali ya James haikuwa nzuri hatimaye alifariki Dunia. ni siku ambayo
Joyce alilia kwa uchungu bila ya kujua nani atamsaidia katika maisha yake. Alisaidiwa
na watu mbalimbali wa mitaani katika mazishi ya mdogo wake na baadaye
alibaki pekee bila kujua ataenda kwa nani ili aweze kumsaidia.
Siku zilienda Huku Joyce akiwa amekata tamaa ya maisha. Baadaye aliamua
kutafuta kazi za ndani ili aweze kujikimu katika maisha. Alihangaika sana
huku na kule bila ya mafanikioBaadaye alifanikiwa kupata kazi katika nyumba ya Mama
mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama Robert. alimuonea sana huruma baada
ya kumueleza kila kitu kuhusu mkasa mzima wa maisha yake basi alianza rasmi
kufanya kazi katika nyumba hiyo.
Ambapo kwa wakati huo mume wake na Mama Robert alikuwa
amesafiri, pamoja na watoto wake wawili. Zilipita kama wiki mbili Joyce
akiwa anaendelea na kazi bila matatizo yoyote "Mwanangu unafanya kazi
vizuri sana lakini pia uwe unapumzika siyo lazima ufanye kazi zote kwa mara
moja" Alisema Mama Robert huku akimsisitiza Joyce awe anapumzika kwani
Joyce alikuwa akifanya kazi sana bila ya kuchoka. Kesho yake ilikuwa ni siku
ambayo Baba Robert ndiyo anarudi kutoka
safari.
Kesho yake Mama Robert aliandaa chakula kizuri akishirikiana
na Joyce. Yalikuwa ni maandalizi ya kumpokea mume wake pamoja na watoto wake. Waliandaa
kila kitu mazingira ya nyumbani yaliwekwa katika hali ya usafi. Baadaye Mama
Robert alijiandaa na kwenda kumpokea mume wake ilikuwa ni furaha isiyo na
kifani, Mama Robert alimkaribisha mume wake pamoja na watoto wake kwa furaha na
baadaye walielekea nyumbani. Ambapo moja kwa moja walienda kukoga kwanza na
baadaye walienda mezani kupata chakula cha jioni. Wakati huo Joyce
alikuwa amejipumzisha chumbani kwake kwa
muda mrefu hivyo hakuonana na wageni.NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA....10
Maoni 2 :
Mhhhhh uyo baba Robert nawasi was naye.
Mungu msaidie, kapita kwingi
Chapisha Maoni