Pages

Jumamosi, Juni 22, 2013

WANAWAKE MNAKARIBISHWA KUJIUNGA NA CLUB YA WANAWAKE WoFI


WoFI (Women Footprints initiative) ni shirika lisilo la kiserekali linalojishughulisha na maswala ya wanawake na watoto wa Tanzania.
Ni shirika lillilosajiliwa na lenye makao makuu yake Sinza.
Tunapenda kuwakaribisha wanawake kujumuika na kujiunga club  kama ifuatavyo;
Umri ;kuanzia miaka 25 na kuendelea.

Aina; wafanyakazi, wajasiriamali, wamama wa nyumbani.
Muda;saa nne kamili mpaka saa sita
Siku;Kila jumamosi (baada ya kujiunga siku maalumu itakubaliwa)

LENGO
·      Kunetwork pamoja
·         Kujifunza kutoka kwa wenzetu
·         Kujadili mamnbo yanayo tuhusu nay a kijamii. (malezi,ndoa,kazi)

Kwa ujumla ni katika hali ya kutiana moyo na kusaidiana ili sote tusonge mbele.

Young girls club
Umri ;kuanzia miaka 16 mpaka 24
Muda;saa saba mpaka saa tisa.

·         Kujadili changamoto zilizopo na namna ya kukabiliana nazo
·         Afya ya uzazi
·         Kupata ushauri
·         Kupata msaada kwa mabinti waliokwama

Kwa ujumla ni kumfanya binti aweze kuanza kujiunga katika mikakati ya maendeleo mapema pia aweze kujitambua.

Counseling
Pia tutakuwa na huduma ya ushauri binafsi,ndoa,vijana .Ni muhimu kupiga na kufanya appointment.

Bedroom lessons
Kila jumamosi ya kwanza ya mwezi tutakua na mafundisho malumu kwa wanawake.

Ofisi zetu zipo Sinza, unashuka makaburini ,kama watokea Mwenge ukifika Makaburini utaona kushoto kibao chetu (WoFI) kifuate .

Kwa maelezo zaidi tupigie 0659 707985

Au tuandikie womenfootprints@yahoo.com


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom