Jumatano, Julai 24, 2013

SIMULIZI KOSA LANGU NI LIPI......SEHEMU YA ....18......



 ILIPOISHIA
Joyce alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwa Hoteli aliwaza sana  “Eeeh Mungu naomba unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui nitafanyaje, yaani nahisi kuchanganyikiwa, nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa Lina. Hapa nilipo nina nina ujauzito wa Fredy, yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na hayazoleki. nimeharibu kila kitu na Fredy hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura yangu.eeh Mungu nisaidie" aliendelea kuwaza Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA  18. 

INAPOENDELEA
Fredy aliamua kwenda nyumbani kwa walezi wa Joyce na kuwaeleza hali halisi kuhusiana na  yaliyotokea . Alikuwa akiendesha gari huku akiwa na mawazo mengi “Huyu mwanamke ameniaibisha sana sikuwahi kutegemea kama ana tabia mbaya kiasi hiki. Ni vyema nikawafahamishe na wazazi wake. Ili wajue nimemfukuza  binti yao”.

  Alikuwa akiwaza huku akiwa anaendesha gari kwa kasi  sana. Kutokana na mwendokasi aliokuwa nao   kidogo asababishe ajali. Ni baada ya kumkosakosa  jamaa mmoja dereva taksi “Wewe kijana mpumbavu sana, mlevi nini wewe unaendesha gari ovyo. yaani ungenigonga leo ungenilipa gari jipya” Aliongea dereva taksi kwa ukali huku Fredy akijifanya kama hajamuona na kuendelea na safari yake.

Alipofika nyumbani kwa walezi wa Joyce kwa bahati nzuri aliwakuta wote wapo nyumbani. Walimkaribisha “Shikamoo Mama habari za hapa” “Marahaba Karibu mwanangu habari za nyumbani jamani mbona mmekuwa kimya sana yaani mnashindwa kabisa kuja kutusalimia”.

 Alilalamika Mama Robert “Asante Mama majukumu tu ndiyo yanasabisha kimya kinakuwa kingi” alisema Fredy huku Mama Robert akiwa anaketi katika sofa lilokuwa pembeni yake “Jamani wanangu haiwezekani mkapotea kwa kiasi hicho sisi ni wazazi wenu mnatakiwa kuja kutujulia hali mara kwa mara.Haya na huyo mwenzio yuko wapi mbona hamjaongozana” Aliuliza Mama Robert .


Fredy alyekuwa amejiinamia kana kwamba kuna kitu anatafakari  akasema “Mama kuna jambo ambalo limenifanya nije hapa leo ni vyema na Baba angekuwepo ili niweze kuzungumza nanyi wote. Jambo lenyewe linamuhusu Joyce” Mama Robert  alikuwa anamtazama kwa umakini sana Fredy nakusema “Mbona unanitisha mwanangu kuna nini kimetokea mwenzio anaumwa au ni nini tena jamani?” Hapana Joyce siyo mgonjwa ila kuna mambo yametokea nadhani ni vyema ukamuita na Baba” Alisisitiza Fredy.  “Baba Robert ametoka hayupo hapa nyumbani wewe zungumza tu mwanangu hakuna tatizo” Fredy alivuta pumzi na kuanza kumueleza Mama mlezi wa Joyce kila kitu kuhusu Joyce na mambo yote yaliyotokea.

Wakati wote akiwa anaelezea Mama Robert alikuwa akimtazama kwa umakini huku akiwa ameweka mkono wake wa upande wa kulia shavuni, “Mungu wangu kweli Joyce anaweza kufanya mambo ya aibu hivyo. Amepatwa na nini huyu mtoto sasa yuko wapi na mbona hapa nyumbani hajafika. Jamani balaa gani tena hili” Alizungumza mama Robert huku akionyesha kupatwa na hasira kwa kile kilichotokea.

Fredy akamjibu”Mama binafsi haya mambo yananiumiza sana akili .Mimi mwenyewe sikutarajia kama Joyce angeweza kunifanyia mambo yote haya na ukiniuliza ameenda wapi mimi siwezi kujua labda atakuwa amemfuata huyo mwanaume aliyezaa naye. Inaniuma sana mimi sina lakuongeza nimekuja kutoa taarifa tu kuwa binti yenu sipo naye tena ameniaibisha sana”.

 Mama Robert akainama chini na kuinua uso wake huku akimtazama Fredy “Yaani unajua siamini ninayosikia inamaana .....” Kabla hajamaliza kuzungumza mlangoni kulisikika mtu anabisha hodi  “Nani tena huyu muda huu karibu ingia mlango uko wazi” Aliyekuwa amekuja kwa wakati huo alikuwa ni Joyce. Alifungua mlango na kuingia alishtuka sana baada ya kumuona Fredy ameketi pale sebuleni. Alisogea taratibu huku akiwa amejaa wasiwasi mwingi.Fredy alimtizama kwa hasira na kunyanyuaka huku akiaga “Mama mimi naondoka nafikiri utakuwa umenielewa”.

Joyce alipoona Fredy anataka kuondoka alisoge na kusema  "Fredy naomba usiondoke Mume wangu, naomba unisikilize mwenzako  sikukusudia kukutendea hivyo nakuomba unisikilize” Aliongea Joyce huku akipiga magoti na mchozi yakiwa yanamtoka “Nikusikilize kitu gani Joyce, sidhani kama mimi na wewe tuna lakuzungumza hata kidogo.Mimi siwezi kukusamehe hata kidogo, wewe endelea na maisha yako” Fredy alifungua mlango na kuondoka bila ya kusikiliza chochote na sasa alibaki Joyce na Mama yake mlezi.

“Ni aibu gani hii wewe Joyce unajua nashindwa hata kuelewa kwa yote haya yaliyotokea. Kwanini umeamua kutuaibisha kiasi hiki. Kweli wewe ni mtu wa kumsaliti mume wako, tena umezaa nje ya ndoa? Halafu unadiriki kumdanganya mume wako kuwa mtoto ni wa kwake na ni  kwa muda mrefu ukiwa umeficha siri. Wewe mtoto si muuaji wewe ni upumbavu gani huu Joyce?”.

 Mama Robert alizungumza kwa hasira Joyce akiwa amepiga magoti huku mikono yake ikiwa kichwani Akasema  “Mama naomba unisamehe sikukusudia kufanya hivi ni shetani tu alinipitia na ushauri mbaya wa rafiki yangu nisamehe mama nampenda sana mume wangu. “Funga bakuli lako eti shetani alinipitia na rafiki alikudanganya inamaana wewe hauna akili udanganyike kirahisirahisi tu mjinga sana wewe tena subiri Baba Robert arudi sijui atakufanya nini wewe. JE NINI KITAENDELEA ...USIKOSE...SEHEMU YA ....19...

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

majuto ni mjukuu,marafk wabayaaaaaaaaa hatmk kusikia.

Bila jina alisema ...

Safi sana mama robert. ikiwezekana hasira zako zote ziishie kwake kwa kichapo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom