Pages

Jumatano, Julai 10, 2013

SIMULIZI....KOSA LANGU NI LIPI...SEHEMU YA ...14......


 ILIPOISHIA
“Vipi shemeji yupo” Joyce akamjibu “Hayupo amesafiri kikazi kama baada ya wikimbili ndiyo atarudi” Lina akaonyesha tabasamu na kusema “ Afadhali kama hayupo sasa sikiliza rafiki hapa nilipo nimekuja kwako jana nilikutana na Sukari anakutafuta yaani ananisumbua sana” Joyce alimwangalia Lina na kusema “ sitaki hata kulisikia hilo jina hapa nyumbani kwangu najuta sana kumsaliti mume wangu”..

INAPOENDELEA
 Kwa dharau Lina akacheka “unanichekesha kweli wewe hutaki kulisikia hilo jina wakati ni baba wa mtoto wako, bila yeye ungepata mtoto embu acha mambo ya kijinga, Sukari  atakusaidia upate na mtoto wa pili” Joyce kwa jazba akasema “ sikiliza nikuambie Lina mimi nilitenda kosa na siwezi kurudia kosa hata sikumoja. Tena naomba kama unataka urafiki wangu na wewe uendelee basi usinitajie huyo mtu hapa nilipo ni mjamzito kwa sasa na  hii mimba ni ya Fredy najuta kutokuwa na subira kwani mume wangu alikuwa na uwezo wa kunipa mimba”

Hahahahahah kicheko cha Lina “leo ndiyo unatambua kuwa ulitenda kosa.Sikiliza nikuambie Joyce mimi sina haja ya urafiki na wewe na ukicheza nitamwambia Sukari kuhusu mtoto wake tuone nani mjanja kati yangu mimi na wewe” aliongea huku akiwa ananyanyuka na kuondoka Joyce aliyekuwa amembeba mtoto wake alisema “siogopi chochote mwanga mkubwa wewe mwanamke una roho mbaya nia yako kunivurugia ndoa yangu” Lina aliondoka na kumuacha Joyce katika Dimbwi la mawazo. 

Baadaye  Lina aliondoka  huku akiendelea kutoa vitisho kwa Joyce kuwa atamueleza ukweli Sukari. Tokea siku hiyo Joyce hakuishi kwa amani alikuwa na hofu sana nini kitatokea iwapo Sukari akija kudai mtoto wake "Sijui nitafanya nini mimi Fredy atakapobaini ukweli najuta sana kutenda kosa hili" yalikuwa ni mawazo ya Joyce.  

Lina kutokana na tamaa ya pesa alimtafuta Sukari na kumueleza kila kitu kuhusu Joyce. kwamba kipindi yupo naye alipata ujauzito na alimweleza kuwa Joyce alimficha kwani nia yake ilikuwa apate mimba na amlee mtoto na mume wake.


 Sukari kusikia hayo maneno alipata hasira sana na kuwaza namna gani anaweza kumpata mtoto wake “yaani huyu mwanamke ni mpumbavu sana anaweza kunifanya nisimjue mwanangu tena analelewa na baba mwingine mtoto wangu mimi haiwezekani mimi mwenyewe sina mtoto lazima niipate damu yangu” aliwaza moyoni mwake Sukari huku Lina akisema "Tena nitakuelekeza na anapoishi na huyo mtoto mmefanana sana" Sukari aliyekuwa amekunja uso kwa hasira akamjibu "Unajua hata wewe Lina ni mtu mbaya sana inamaana ulikuwa unataka mtoto wangu nisimjue yaani ninyi ni wauaji".

 Lina kwa kujishaua akasema "Najua nimekukosea sana Sukari naomba unisamehe nitakusaidia ili mtoto wako akutambue kama baba yake mzazi" Sukari alisimama na kuzunguka huku na kule bila kujua wapi anaelekea akitafakari "Sijui nikamshtaki huyu mwanamke kwanini amenifanyia hivi inaniuma sana yaani mtoto wangu, damu yangu, halafu anitambui kama mimi ni baba yake hapana kwakweli imeniuma sana".

Lina alimwelekeza Sukari hadi Joyce anapoishi na mume wake pamoja na sehemu ambazo anafanya kazi zake ndipo siku hiyo aliamua kumfuata nyumbani kwake aliingia moja kwa moja ndani baada ya kubishana na mlinzi wa getini. "Unaelekea wapi kijana mbona nakuuliza unijibu unataka kuingia kwa nguvu" Alihoji mlinzi "Sikiliza wewe ninapoelekea ni hapa nilipofika niitie mama mwenye nyumba" alisema Sukari huku akimkazia macho mlinzi.

  Joyce alitoka nje baada ya kusikia sauti za malumbano kwa mbali, alishtuka  alipomuona Sukari mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi huku akiwa kama amepigwa butwaa, Sukari  alisogea kwa ukaribu  na kumwambia "Haina haja ya kushangaa wala kuogopa kila kitu nafahamu wewe mwanamke ni muuaji mkubwa”  Joyce aliyekuwa amesimama kana kwamba haamini anachokiona alimgeukia yule mlinzi "Nenda getini unamtizama nani hapa" yule mlinzi alirudi getini na kuwaacha Sukari na Joyce na  kwa wakati huo Fredy bado alikuwa safarini kikazi.

 Joyce alimwangalia Sukari na kusema “Sikiliza nikuambie  huyo aliyekuambia hayo maneno amekudanganya hayana ukweli wowote” Sukari alisogea karibu ya Joyce na kumtazama huku akiwa amemkazia macho, akizungumza kwa sauti iliyojaa  jazba. Joyce alikuwa akionekana kuwa na hofu kubwa. “Mimi sitaki ugomvi na wewe ninachotaka ni mtoto wangu fanya utakavyoweza lakini fahamu kwamba namtaka mwanangu atambuwe kuwa mimi ni baba yake” alisema Sukari. Joyce akamjibu “Wewe una kichaa mtoto si wa kwako tena naomba uondoke katika nyumba yangu kabla sijakuitia Polisi” Sukari akacheka kidogo na kusema “Halafu ukiwaita hao Polisi utakuwa umenisaidia sana, mimi naondoka lakini nitarudi hadi nihakikishe nampata mwanangu”....USIKOSE SEHEMU YA ....15......Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

nimemchukia wajina wangu sana,ndo kafanya nn ss?naomba mtto awe ajafanana na sukari plzzzzzzzzzzzzzzz,coz sitopenda joy alie tna.

Bila jina alisema ...

pole dadaa,always shortcut is a longcut

Bila jina alisema ...

Ayaaaaa,! patamu hapo! siamini macho yangu nini kitatokea hapo. dada adela 2pe vi2 hivyo 2jue mwisho wake. big up dada ye2.

Bila jina alisema ...

Mamaaaaa! ukickia kuwa kula kulipa ndo hapo. jamani namstikia sana joyce kwa kutokuwa mwaminifu 7bu ya kumsiliza sana shoga yake linah.

Bila jina alisema ...

Yeeleewiii! yesu na maria! bora joyce akimbilie kibololon akajifiche maana fred akirudi na kuckia hizo habari atazimia kama c kukata roho.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom