ILIPOISHIA
Joyce
alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwa Hoteli aliwaza sana “Eeeh
Mungu naomba unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui nitafanyaje, yaani
nahisi kuchanganyikiwa, nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama
watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa Lina. Hapa nilipo nina
nina ujauzito wa Fredy, yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya
yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na hayazoleki. nimeharibu kila
kitu na Fredy hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura yangu.eeh Mungu
nisaidie" aliendelea kuwaza Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI
KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA 18.
INAPOENDELEA
Fredy aliamua
kwenda nyumbani kwa walezi wa Joyce na kuwaeleza hali halisi kuhusiana na yaliyotokea
alikuwa akiendesha gari huku akiwa mwingi wa mawazo “Huyu mwanamke
ameniaibisha sana sikuwahi kutegemea kama ana tabia mbaya kiasi hiki ni vyema
nikawafahamishe na wazazi wake ili wajue nimemfukuza binti yao”
Alikuwa akiwaza huku akiwa anaendesha gari kwa kasi bado kidogo asababishe ajali baada ya
kumkosakosa jamaa mmoja dereva taksi
“Wewe kijana mpumbavu sana, mlevi nini wewe unaendesha gari ovyo yaani
ungenigonga leo ungenilipa gari jipya” Aliongea dereva taksi kwa ukali huku
Fredy akijifanya kama hajamuona na kuendelea na safari yake.
Alipofika nyumbani kwa walezi wa Joyce alikaribishwa vizuri sana “Shikamoo mama habari za hapa”
“Marahaba Karibu mwanangu habari za nyumbani jamani mbona mmekuwa kimya sana
yaani mnashindwa kabisa kuja kutusalimia” Alilalamika Mama Robert “Asante Mama
majukumu tu ndiyo yanasabisha kimya kinakuwa kingi” alisema Fredy huku Mama
Robert akiwa anaketi katika sofa lilokuwa pembeni yake “Jamani wanangu
haiwezekani mkapotea kwa kiasi hicho sisi ni wazazi wenu mnatakiwa kuja
kutujulia hali mara kwa mara, haya na huyo mwenzio yuko wapi mbona hamkuongozana?” Aliuliza Mama Robert .
Fredy aliyekuwa amejiinamia kana kwamba kuna kitu
anatafakari “Mama kuna jambo ambalo limenifanya nije hapa leo ni vyema na baba
angekuwepo ili niweze kuzungumza nanyi wote jambo lenyewe linamuhusu Joyce”
Mama Robert akiwa anamtazama kwa umakini
sana Fredy akasema “Mbona unanitisha mwanangu kuna nini kimetokea mwenzio
anaumwa au ni nini tena jamani?” Hapana Joyce siyo mgonjwa ila kuna mambo
yametokea nadhani ni vyema ukamuita na Baba” Alisisitiza Fredy .
“Baba Robert ametoka hayupo hapa nyumbani
wewe zungumza tu mwanangu hakuna tatizo” Fredy alivuta pumzi na kuanza
kumueleza Mama mlezi wa Joyce kila kitu kuhusu Joyce na mambo yote yaliyotokea,
wakati wote akiwa anaelezea Mama Robert alikuwa akimtazama kwa umakini huku
akiwa ameweka mkono wake katika paji la uso wake.
“Mungu wangu kweli Joyce
anaweza kufanya mambo ya aibu kiasi hiki amepatwa na nini huyu mtoto. Na sasa atakuwa amekwenda wapi na mbona hapa nyumbani hajafika, jamani balaa gani tena
hili” Alizungumza mama Robert huku akionyesha kupatwa na hasira kwa kile
kilichotokea.Fredy akamjibu”Mama binafsi haya mambo yananiumiza sana
akili mimi mwenyewe sikutarajia kama Joyce angeweza kunifanyia mambo yote haya
na ukiniuliza ameenda wapi mimi siwezi kujua labda atakuwa amemfuata huyo
mwanaume aliyezaa naye inaniuma sana mimi sina lakuongeza nimekuja kutoa
taarifa tu kuwa binti yenu sipo naye tena ameniaibisha sana”.
Mama Robert akainama chini na kuinua uso wake
huku akimtazama Fredy “Yaani unajua siamini ninayosikia inamaana .....” Kabla
hajamaliza kuzungumza mlangoni kulisikika mtu anabisha hodi
“Nani tena huyu muda huu karibu ingia mlango uko wazi”
Aliyekuwa amekuja kwa wakati huo alikuwa ni Joyce alifungua mlango na kuingia
alishtuka sana baada ya kumuona Fredy ameketi pale sebuleni alisogea taratibu
huku akiwa amejaa wasiwasi mwingi Fredy alimtizama kwa hasira na kunyanyuaka
huku akiaga.
“Mama mimi naondoka nafikiri utakuwa umenielewa” Fredy naomba
usiondoke Mume wangu naomba unisikilize mwenzio sikukusudia kukutendea hivyo
nakuomba unisikilize” aliongea Joyce huku akipiga magoti na mchozi yakiwa
yanamtoka “Nikusikilize kitu gani Joyce sidhani kama mimi na wewe tuna
lakuzungumza wewe endelea na maisha yako” Fredy alifungua mlango na kuondoka
bila ya kusikiliza chochote na sasa alibaki Joyce na mama yake mlezi.
“Ni aibu gani hii wewe Joyce unajua nashindwa hata kuelewa
kwa yote haya yaliyotokea kwanini umeamua kutuaibisha kiasi hiki kweli wewe ni
mtu wa kumsaliti mume wako tena umezaa nje yandoa yako huku ukimdanganya mume
wako kuwa mtoto ni wa kwake na ni kwa
muda mrefu ukiwa umeficha siri, wewe mtoto si muuaji wewe ni upumbavu gani huu
Joyce” Mama Robert alizungumza kwa hasira Joyce akiwa amepiga magoti huku
mikono yake ikiwa kichwani .
“Mama naomba unisamehe sikukusudia kufanya hivi ni
shetani tu alinipitia na ushauri mbaya wa rafiki yangu nisamehe mama nampenda
sana mume wangu. “Funga bakuli lako eti shetani alinipitia na rafiki
alikudanganya inamaana wewe hauna akili udanganyike kirahisirahisi tu mjinga
sana wewe tena subiri Baba Robert arudi sijui atakufanya nini wewe.
Joyce alibaki kama amemwagiwa maji huku Mama
Robert akiendelea kuzungumza "haya na mtoto yuko wapi" huku akiwa
amejiinamia chini "Mtoto amemchukua Sukari" kwa mshangao mama Robert
akamwambia "Hee! Kweli unajua haya mambo mimi siamini jamani hivii ni kitu
gani hasa kilikupelekea kumsaliti mume wako aibu kubwa sana hii sikuwahi
kufikiria una tabia za ajabu kiasi hiki".
Joyce aliinama chini kwa aibu
"Mama naomba unisamehe sikukusudia kutenda yote haya ni shetani tu
alinipitia nisaidie mama ni wewe pekee unaweza kuwa karibu na mimi"
waliendelea kuzungumza baadaye mama Robert alinyanyuka na kuelekea chumbani
huku akimtaka Joyce aende chumbani kwake akapumzike. ITAENDELEA KITABU HIKI KITAWAJIA HIVI KARIBUNI USIKOSE NAKALA YAKO.
Maoni 4 :
jaman dada adela mlete kandida na mauza2 yake kwan nimemmis sana.
habari Dear/samahani kama nitakukwaza naju blog ni yako,lakini kuna kitu kimenishangaza mimi nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa hadithi na blog yako kwa ujumla, sasa ukawa unatuhadithia hadithi mbalimbali lakini kabla hadithi hizo hazijaisha, ukaacha, then umeamua kuanza upya hadithi hizo kwa ambao hawajazisoma, sijaelewa logic behind this, naomba unisaidie kunielewesha.
Tupo pamoja mpendwa, UPO JUU!
pa1 xana.. upo juu kama mawingu..!
Chapisha Maoni