Pages

Jumapili, Julai 07, 2013

KOSA LANGU NI LIPI ..SEHEMU YA ..13....


 

 ILIPOISHIA
Joyce alimsikiliza Mama Fredy kwa umakini na kusema "Lakini mama mbona unafika huko" Alilalama Joyce Mama Fredy akamjibu kwa sauti iliyojaa jazba "Huko wapi?Ahera au, tena sikiliza nikuambie fanya ufanyalo mimi nahitaji mjukuu. alaah! Hivi unafikiri hili jambo ni dogo eeh, mimi naondoka lakini tuliyoyazungumza hapa ukae nayo kichwani na uyafanyie kazi" Aliongea huku akiondoka na kumuacha Joyce akiwa ameketi pale sebuleni. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU YA ......13..

INAPOENDELEA

 Hali hiyo ilimuumiza sana Joyce. Baadaye aliamua kwenda kwa Lina na kumueleza hali halisi mambo yanavyoendelea. “Lina rafiki yangu nisaidie, naogopa kwenda Hospitali nina hofu maisha niliyopitia zamani, nadhani hata wewe unajua kuwa mimi nilikuwa nikitoa sana mimba.yawezekana ikawa ndiyo sababu.Na Fredy amenionyesha vipimo vyake yeye hana tatizo embu nishauri nifanyeje”.

 Lina aliguna kidogo na kusema “Sasa hapo rafiki mimi nakushauri jaribu kuwa na mwanamume mwingine uangalie kama utapata mimba” Joyce alishtuka na kusema “Wewe Lina yaani nimsaliti mume wangu? Hapana haiwezekani na tena yeye hana tatizo nahisi mimi ndiye mwenye matatizo.” Lina alicheka kidogo kwa dharau nakusema “Unanichekesha wewe, inamaana Joyce umeshakuwa na wanaume wangapi kipindi cha nyuma,  leo hii unaogopa kujaribu kuwa na mwanamume mmoja tu.” Joyce kwa sauti ya upole akasema "Usiseme hivyo Lina hayo mambo yalikuwa zamani nawala sikudhamiria kutenda zilikuwa ni shida tu, mimi sikupenda kuwa dada poa. Hata na hivyo nimeolewa na namuheshimu sana mume wangu" Alisema Joyce.

 "hahahaha unanichekesha wewe” Kilikuwa ni kicheko cha Lina huku akiendelea kusema  “Sikiliza nikuambie, kama kweli unataka kuendelea kuishi na Fredy jaribu kupata mimba nje kwani kila kitu kinawezekana, mbona hayo ni mambo ya kawaidia tu, vinginevyo unataka Fredy achukue mwanamke mwingine." Aliendelea kumshawishi mwisho wa siku Joyce alikubali kujaribu kwa shingo upande.

Akiwa nyumbani Joyce alikuwa akiwaza sana juu ya uamuzi wake wa kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine "Hili jambo ninalotaka kulifanya ni hatari sana, lakini sina namna inabidi nifanye hivi, ila  nafsi yangu inasita, kwani namsaliti mume wangu ila nikifikiria Fredy anaweza kutafuta mwanamke mwingine." Alikuwa akiwaza huku akijiuliza maswali aliyokuwa akijijibu mwenyewe.


Baada ya wiki moja,  Lina alimkutanisha Joyce na kaka mmoja mfanyabiashara aliyeitwa Sukari. Baada ya kufahamiana taratibu walianzisha uhusiano wa siri. Lakini wakati Joyce akiwa anafanya hivyo hakutaka  Sukari agundue lengo lake kuwa ni kupata mtoto.Kwa kipindi chote Sukari alikuwa hajui kama Joyce ni mke wa mtu.
 Joyce alifanya mambo yote hayo kwa siri sana. Kwani kwa wakati huo pia alikuwa akijihusisha kimapenzi na mume wake kama kawaida.

BAADA YA MIEZI MIWILI

Baada ya miezi miwili kupita  hali ya Joyce ilibadilika alijigundua kuwa ni mjamzito. Alifurahi sana. Huku moyoni mwake akijua ujauzito alionao siyo wa mume wake.Alimfahamisha Fredy siku hiyo walikuwa pamoja nyumbani Fredy alifurahi sana huku akimkumbatia Joyce kwa furaha.Wakati huu mapenzi yaliongezeka maradufu kwa mke wake kipenzi. Baada ya kupata ujauzito Joyce alianza kukata mawasiliano na Sukari, hakutaka kabisa kuonana naye. 

Na mara nyingi Sukari alimtuma Lina akamwambie ni kwa kiasi gani anamuhitaji lakini Joyce hakutaka  kabisa kumsikia.Ilifikia kipindi Sukari alikata tama ya kuendelea kumfuatilia Joyce. Maisha yaliendele, Baada ya miezi tisa kutimia Joyce alijifungua salama mtoto wa kiume. Alimbatiza jina na kumuita  James. Kwa kipindi kirefu Sukari alikuwa amesafiri  alikuwa Mkoani Mwanza katika biashara zake. Wakati wote huo hakuwa na mawasiliano na Joyce.

BAADA YA MIAKA MITATU
Baada ya miaka mitatu kupita Sukari alirudi Dar es Salaam. Siku moja  akiwa katika mizungunguko ya hapa na pale alikutana na Lina.  Alifurahi sana na kumwambia kuwa angependa kuonana na Joyce, kwani bado alikuwa akimpenda."Nimefurahi sana kukutana na wewe Lina natamani sana kumuona Joyce, nilimpenda sana natamani angekuwa mke wangu" Alisema Sukari huku akimtizama  Lina. "Umechelewa sana Sukari  Joyce ameolewa na ana maisha yake na mume wake kwani hawezi tena kuwa na wewe kwahiyo ni vyema ukamsahau" lakini aliendelea kumsisitiza amsaidie huku akimuahidi kumpatia pesa nyingi endapo atafanikiwa.

 Lina kutokana na kuahidiwa fedha nyingi na Sukari, aliamua siku moja kumfuata Joyce nyumbani kwake alimkuta anacheza na mtoto wake “Mambo shosti naona unazidi kupendeza na mwanao” hahahaha kilikuwa ni kicheko cha Joyce “mwenzangu nina furaha sana James ananichekesha hapa na maneno yake na hivi hajui kuongea vizuri” huku akimkaribisha lina walikaa kibarazani na kuanza kuzungumza Lina alimuuliza Joyce “Vipi shemeji yupo” Joyce akamjibu “Hayupo amesafiri kikazi kama baada ya wikimbili ndiyo atarudi” Lina akaonyesha tabasamu na kusema “ Afadhali kama hayupo sasa sikiliza rafiki hapa nilipo nimekuja kwako jana nilikutana na Sukari anakutafuta yaani ananisumbua sana” Joyce alimwangalia Lina na kusema “ sitaki hata kulisikia hilo jina hapa nyumbani kwangu najuta sana kumsaliti mume wangu”..

..je nini kitaendelea usikose  SEHEMU YA 14....

 

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

hapo sasa wajina wangu kabug steps,duh wajina mtata balaha,yn naomba hamkimbie kma ukoma,na pia uyo james naomba afanane na kaka yake joyce jmn ili siri iwe ngumu kutoka,basi fred c mzma kma sukar kampa mimba joy.

Bila jina alisema ...

Ndo tatizo la kuwa na marafiki wasiokuwa na mwelekeo wa maisha kama lina,:

Bila jina alisema ...

Hongera kwa kufanikiwa kupata mtoto dada joyce japokuwa umemkosea sana fred kwa kumcheat. mungu akusamehe sana

Bila jina alisema ...

Daaaaah! namshauri joyce aachane na lina la sivyo atapotea mithili ya barafu iyeyukavyo ndani ya maji

Bila jina alisema ...

Heeee,! mimi nashindwa kuelewa tatizo ni nin kwa fred. vipimo vinasema yupo fit, sasa kashindwa nin hapo mpaka mke wake anatoka nje ya ndoa!

Bila jina alisema ...

damu zao haziendani ndio maana,

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom