Mwanamke anapoandaa chakula na kula pamoja na mwenza wake inapendeza sana,kwani imekuwa ni kawaida baadhi ya wanaume kujisahau kabisa kwamba natakiwa niwahi nyumbani nikale pamoja na mwenzangu,,au kutoka out tukapate dinner,jamani kula pamoja pia ni njia ya kuweka ukaribu zaidi na yule unayempenda,, kama anapika chakula ambacho hukipendi bora umueleze na kumuelewesha kuliko kukaa kimya na kula unapopajua wewe.. |
Maoni 7 :
Hahahahaa adela hapa umepaonaje duuuh!! hii tabia ipo kwa watu wengi sana, yaani utakuta mtu kwake kashiba, au hata akila anakula tu kidogo utamsikia kashiba au atajidai chakula sio kizuri, kumbe kashakula nje kwa kioski, coz kuna watu wamezowea kulakula nje, au wengine wanakula kwa wanawakezao wa nje, wakija kwao wameshiba, hii tabia ipo sana sana kwa wanaume, jamani tuacheni, coz mke/mwanamke anafurahi sana kama ataandaa chakula kisha wewe muhusika unaesoma hii comment ukafurahia chakula na kula pamojanae!!
Adela ni kweli mpendwa wangu, lakini kuna zaidi ya hapo. Unajuwa maisha yanakuwa matamu zaidi pale mnaposhirikiana kila kitu (kumbuka kwamba wawili wamekuwa mwili mmoja)? Mkijenga utaratibu wa kuwa pamoja nyumbani na hata mnapotoka out ni pamoja yafuatayo yatafanyika; 1. Wakati wa kuamdaa mulo wa mchana siku za weekend au jioni, wapendanao huwa wanashirikiana na kinapokuwa tayari hufurahia matunda ya maandalizi yao, na maandalizi hayo huendelea kuzaa matunda mazuri hadi mtakapo enda kupumzika usiku. 2. Kama wapendanao huwa na kawaida ya kutoka out kwa pamoja, mtajikuta mnajenga utaratibu wa kuwajibika kwa pamoja na hawa kama wote manafanya kazi/biashara inayo waingizia kipato; siku moja huyu anahudumia out hii na siku nyinghine mwingine anahudumia out ile au kwa pamoja mnagawana ghalama za uot, hapo upendo hunoga zaidi.
Adela upendo hujengwa na tabia ya wahusika, moja ya tofari ni kipindi cha kushiriki chakula kwa pamoja.
Kadili.
...inategemea ni chakula cha namna gani na aina ya mapishi bibi, au vipi?
@Hashir tuko pamoja @Kdili pamoja pia@Chacha pamoja sana....kula na mwenzio inaleta raha,,na kama hajui kupika mfundishe na si kunyamaza kimya na kula pembeni mapenzi hayaendi hivyo
Kweli bwana kula pamoja inaleta raha sanaaaa...Alafu Blog yako ni nzuri Mdada.keep it up.
kweli bwana kula pamoja inaleta raha sanaa.
Alafu blog yako ni nzuri mdada.
@Edna asante mwaya tuko pamoja mpenzi hata yako nimeipenda sana wangu..
Chapisha Maoni