Jumapili, Septemba 26, 2010

Kuwa mbunifu katika mahusiano ni jukumu la wote mwanamke na mwanaume..

Ubunifu katika mapenzi ni ile hali ya kujaribu kuleta vitu tofauti katika mahusiano baina ya wapendanao,ili kufanya penzi kuonekana jipya kila wakati,tazama picha hii huyu kaka anamsaidia mwenza wake katika mapishi huku wote wakiwa na furaha,inawezekana mwanamke ni jukumu lake kuandaa chakula lakini katika suala la ubunifu mwanaume naye anaweza kuamua siku moja kumuandalia mwenza wake chakula ili kuleta ladha tofauti, kwa kuamua yeye mwenyewe inapendeza sana..



Wakati mwingine unaweza kuwa mbunifu kwa kumwandalia mwenzio zawadi katika hali ya suprise huku ukiwa umeandika ujumbe mzuri inawezekana ukawa unahusu kwa namna gani unavyompenda au namna ambavyo unafurahia penzi lenu,inapendeza na huongeza mvuto pia..

Inawezekana ukafanya hivi pia ukapamba kitanda chako vizuri  ukaweka maua mazuri pamoja na mvinyo kama unavyoona kama huwa mnatumia mwenzio akirudi kutoka kazini na kukuta mabadiliko kama haya mara mojamoja inampa faraja na kuona hakuna kama mke au mume wangu,,Ubunifu huu unaweza kuwa katika sehemu  mbalimbali katika mapishi, maongezi, mavazi, urembo,maendeleo nk. Ni jukumu lako kuwa mbunifu wakati wote ili kuongeza mvuto katika penzi lenu....

Maoni 1 :

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

.....kwa wengine utaonekana kama vile unajikomba! Hivo inabidi ulichukulie kwa umakini kabla hujaanikwa mtaani kwa mashostito na mablazameni kuwa 'yule kadata, anajikomba kwa kuniletea hiki ama kile'... :-(

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom