Katika picha hii nimeonyesha tafakari akilini mwako je kwa nini nataka kupekua simu ya mwenzangu?je kuna ulazima wowote au lazima nipekue ili nione kama kweli ananipenda peke yangu,, je itanisaidia au itaniletea matatizo? haya ni mambo ya kutafakari.... |
Maoni 5 :
Hapo sasa itakuwa ishu kama unahisi umwamini mpenzi wako inabidi uchukue tu hiyo simu usome kwa sababu wapenzi wanaopendana na kuaminiana siku zote hakuna siri kati yao mtu yeyote anaweza akachukua simu ya mwenzake akasoma sms lakini ukiona mtu anakuwa mkali na simu yake ujue kuna kitu. by pipo
Asante sana wangu tuko pamoja kikubwa uaminifu ndio nguzo pekee katika mahusiano,,kwani kuna ubaya gani mwenzio akishika simu yako mi naona ni kutokujiamini...na tatizo sasa siku ukiwa umeiacha mwenzio akipekua ukirudi ugomvi unaanza na wengine unakuta wanaacha kwasababu ya simu ya mkononi,....
Unachofikiria ndicho kinachokuwa! na unachokitaka ama kukikataa ndicho kinachokuja maishani mwako! Ukimhisi mwenzio unatuma nguvu ambayo inakuunganisha na wanaomtaka mwandani wako na akinasa nawe unambamba inakuwa nzugwe ati....lol!
simu mara nyingi zimekuwa chanzo cha magomvi ya mahusiano. kama mtu una ujasiri ni vema kukaa mbali na simu ya mwenzio. kumbuka usemi hasira hasara
KWA UPANDE WANGU SIONI KWANINI NISISOME SMS KWENYE SIMU YA MPENZI WANGU, KWANI SMS NDIZO ZITAKAZO NIPA UHALISIA HALISI WAKE ANAOSEMA KUWA ANANIPENDA NA NIKO PEKE YANGU. SO WALA WATU WASIOGOPE KUSOMA SMS KWANI UTAUJUA UKWELI LINI???? NA KWANINI UISHI KWENYE MAISHA YALIYOJAA UONGO?? MIMI NINASUPPORT SANA TENA SANA MWANAUME AU MWANAMKE KUSOMA SMS ZA MWENZI WAKE. KWENYE MAPENZI KUNAITAJI UJASIRI SO KWANINI UOGOPE KUFACE UKWELI ULIOMBELE YAKO?? HASWA KWA HALI HII YA GONJWA HILI HATARI LA UKIMWI!
Chapisha Maoni