Jumapili, Septemba 19, 2010

Katika mapenzi usiseme hautopenda tena,, kwasababu mapenzi hayatabiriki,,,

Katika picha hii haya ni maneno ambayo watu wengi waliotendwa katika mahusiano hupenda kutamka kwamba sintokaa nipende katika maisha yangu nawachukia sana wanaume au wanawake,,au hakuna mapenzi siku hizi yote ikiwa ni sababu ameshaumizwa sana katika mapenzi na kukata tamaa kabisa.
Kutokana na kuumizwa sana katika mahusiano mwanamke au mwanaume anaweza kuchukia hata watu waliomzunguka ambao hawana makosa,,na hata kuchukia mahusiano ya watu wengine,na mtu huyu hata ukimfuata kwa ajili ya ushauri wa kimapenzi ni vigumu sana kukupa ushauri mzuri na yote ni  kwasababu anachukia mapenzi.
Tazama picha hii hawa ni watu waliokata tamaa ya kupenda katika mapenzi,,,na katika hatua ya kuchukia mapenzi wengine huwa wanachanganyikiwa kabisa,,inaanza hali ya kuacha kujipenda,wengine kunywa sumu,wengine kuanza kutumia kilevi na mwingine anaamua kuwa na wanawake au wanaume wengi huku akiwa hana mapenzi nao na yote ni kwasababu anaamini mapenzi ya kweli hakuna...
Kwasababu ya kutendwa moyo wako unaweza kuwa katika hali ambayo inaonekana katika picha yaani umevunjka kutokana na maumivu ya kutendwa,,sasa kwa mtu aliye katika hali hii huwa anahitaji ushauri kutoka kwa wataalamu ili kurudi katika hali yake ya kawaida,,kwani kuna watu wengi sana ambao wamepitia misukosuko mingi sana katika mapenzi lakini baadae wanasahau na kujikuta wakipenda tena,,na wakati huu unajikuta umempata mtu sahihi ambaye anayo mapenzi ya dhati na hawezi kukuumiza tena hivyo basi nashauri tusikate tamaa katika mapenzi........

Maoni 6 :

alice alisema ...

ni kweli kabisa Adela unachokizungumza,,huwezi kusema sintopenda tena kwani ni kitu ambacho kipo na hata siku moja huwezi kuwa mpweke maisha yako yote unaweza hata kuchanganyikiwa hongera sana kwa mada zako nzuri,kila laheri

o'Wambura Ng'wanambiti! alisema ...

kama unachokisema hapa ni kweli nina wasiwasi kwa kuwa huko 'kutendwa' mnakokusema hakuna uhusiano na upendo bali hisia.

unaposema sitapenda tena maana yake ni kuwa huna hisia za upendo na si kwamba huna upendo la sivo dunia hii ingekuwa mbaya sana. upendo hauwezi kuisha abadani bali hisia za upendo huenda ama kupungua na kurejea kulingana na tukio ama mazingira.

wabheja sana ng'wanawane!

Anneth Nyoni alisema ...

Nikweli mapenzi hayatabiriki c vizr sana kuweka nadhiri ya kutopenda tena upepo waweza geuka

Unknown alisema ...

Ni kweli dada Dally! maelezo yako nimeyapenda, kwanza mapenzi ni matamu, ukisusa utakosa raha ya Duniani, kilichotuweka hapa Duniani ni Mapenzi tu, Mwenyezi Mungu alisema "Nendeni mkazaliane muijaze Dunia" Kwanini hakusema "Nendeni mkatafute Pesa!?". Ila ukifikiria sana Mapenzi unaweza kuwa Chizi. Thanx Da' Dally.

Susan Wamunza alisema ...

Adella usiombi kutendwa ni kusema sitopenda tena ni jambo la kawaida mana unakuwa upo kwenye hasira za mapenzi unaweza kumchukia hata baba yako mana unaona wanaume wote wapo sawa kumbe sio.

Unknown alisema ...

sister huwa nihasira hata mimi nilisha wai kusema hayo maneno lkn mwisho wa siku nikaingia tena ktk mapenzi tena kwa kasi kupita hata ile ya mara kwanza.kutendwa kunaumiza cster.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom