Jumapili, Septemba 12, 2010

kuna tamu na chungu ya wivu katika mapenzi,,,,,,Tamu ni wivu ulio na mipaka ambao unaleta furaha na kuongeza mapenzi zaidi,,wakati chungu ya wivu ni ule uliopitiliza na kuleta migogoro..

wivu ni kidonda katika mahusiano na unaweza kukufanya ukawa hauna amani katika maisha yako,mtazame huyu dada upande wa kulia akiwa anamtazama huyo kaka katikati kwa hasira kutokana na kuona wivu jinsi ambavyo wanzungumza na kufurahi pamoja na huyu dada wa upande wa kushoto,wakati mwingine mtu unaweza ukajiumiza kwa kitu ambacho sio kweli unaweza ukahisi mpenzi wako anakudanganya lakini kumbe sivyo unavyofikiria ndio maana unakuta mtu mwingine anapigana kutokana na wivu wengine wanaachana kutokana na wivu,jamani mapenzi si lelemama hutakiwi kuwa na wivu kupita kipimo,,wivu uwepo lakini usizidi kipimo kwani inakera na unaweza ukafikiri kwa kufanya hivyo unajenga kumbe unabomoa.ndio maana wengine utasikia kanywa sumu kutokana na wivu wa kimapenzi au amemuua mke wake kisa amehisi anatoka nje ya ndoa mtu ukifikia katika hatua hii kweli utakuwa ni kichaa yaani unaamua kufanya tukio la kuhatarisha maisha yako bila hata ya huruma na tena kwa kufanya hivyo ndio unajiongezea matatizo,,jamani ni vizuri unapoona kuna tatizo katika mahusiano yenu basi ni bora kukaa na kuzungumza kujua nini cha kufanya ili kujenga na si kubomoa............
.

Maoni 1 :

alice alisema ...

wivu ni kidonda ukishiriki unakonda.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom