Alhamisi, Septemba 16, 2010

Maisha ya Ciara kwa ufupi......

Ciara amezaliwa kwa wazazi mchanganyiko wenye asili ya Ireland na Ujerumani akiwa mtoto pekee wa baba Carltonna na mama Jackie Harris kwa kuwa baba yake alikuwa katika jeshi la Marekani hivyo ciara alikulia katika kambi ya Jeshi la Ujerumani,Ciara amesema licha ya kuchukia kuwapoteza marafiki zake wazuri kutokana na kuhamahama kutokana na kusafiri kumemsaidia kuimarisha kipaji chake kwa kujua mazingira tofauti..
Ciara ni binti wa kimarekani aliyezaliwa oktoba 25,1985 na amekuwa akitumia jina lake la Ciara katika shughuli zake za sanaa,kwani mbali na kuwa muimbaji Ciara ni dansa mkali ndio maana video zake hufanya kazi ya nzuri,lakini pia ni muigizaji na mwanamitindo,Wimbo wa kwanza wa Ciara ulikuwa ni wimbo mkali  uliotamba sana wa Goodies,na katika album yake ya kwanza iliyoitwa GOODIES ilikuwa  mafanikio makubwa ikiuza nakala milioni tano duniani kote.
Ciara ameweza kufahamika zaidi na nyimbo mbalimbali kama promice,like a boy,i can't live him alone na love sex magic ya mwaka 2009,,lakini kwa sasa mambo yake kimuziki yameonekana sio mazuri,na video ya wimbo wake wa .Ride, ulipigwa marufuku kuchezwa katika kituo cha television  cha BET ilidaiwa kuwa inaonyesha vitendo vya kikubwa mno lakini vituo vingine vinaicheza video hiyo kila siku,na hivi karibuni Ciara aliondolewa katika ushirikiano wa wimbo wa Usher Raymond katika wimbo wa Hot Toddy,Pia album yake mpya iliyotarajiwa kutoka Agost 17 mwaka huu, uzinduzi wake ulisogezwa mbele na taarifa kamili lini itatoka haijafahamika.lakini Ciara yupo juu naamini anaweza kurudi vizuri katika gemu,,
katika ukurasa wake rasmi wa internet Ciara amemtaja Bow Wow pekee kama mwanaume ambaye amepata kuwa na mahusiano naye, hakuzungumzia mahusiano yake kabla hajawa maarufu na hakuwataja 50cent na Ludacriss ambao amepata kuhusishwa nao katika vipindi tofauti,.Alianza mahusiano na Bow Wow mwaka 2005 hadi April 2006  mahusiano yakavunjika na kusitisha uvumi uliokuwa umezagaa kuwa wanafunga ndoa,pia alidaiwa kuwa na uhusiano na 50cent mwaka2007-2009, lakini yeye mwenyewe hakuwahi kulizungumzia hilo na pia tetesi zinadai alishakuwa na Ludacris mwaka2008,,lakini yeye anamtaja Bow Wow pekee kuwa ndiye aliyewahi kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi.mapenzi ya masuperstar kazi kweli kweli, wengi wao hawadumu katika mahusiano. na hayo ndio maisha ya Ciara.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom