Alhamisi, Septemba 16, 2010

Serengeti breweries leo wametangaza rasmi mchakato wa kuwatafuta washiriki wa TUSKER PROJECT FAME IN TANZANIA....2010

Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja Uhusiono wa Serengeti Breweres Teddy Mapunda amesema nia ya mashindano hayo ni kutafuta vijana wenye uwezo wa kuimba ili kuonyesha vipaji vyao,na amesema kwa upande wa nchi kama Kenya ,Uganda na Rwanda wenyewe tayari wamekwisha maliza mchakato wa kuwatafuta washiriki na kwa mwaka huu washiriki kutoka nchi ya Sudan pia watashirikishwa.



Pia amesema kwa wale ambao wangependa kujiandikisha usaili unafanyika Peacock Hotel siku ya Jumamosi september 18 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni,  mshiriki lazima awe na umri wa miaka 23 na kuendelea na kila mshiriki anatakiwa aende na cheti ili kuonyesha ukweli wa umri alionao.


Vile vile forms za maombi zinapatikana Mlimani City,Benjamin Wiliam Mkapa Towers,Jengo la IPS  na Peacock hotel.inawezekana kama unacho kipaji jaribu bahati yako.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom