Tazama picha hii huyu kaka amekasirika na mpenzi wake naye amekasirika ,sasa nini hatma yake,,kila mmoja akiamua kununa katika mahusiano,,mwisho wake unakuwa mbaya kwani inaweza kumpelekea mwanaume au mwanamke kumsaliti mwenza wake kwasababu ya kutokuwa na maelewano.. na wakati huo wote mkiwa mnayafumbia macho matatizo mliyonayo katika mahusiano yenu, Utakuta mtu na mke wake wanaishi nyumba moja lakini wananuniana wiki na hata miezi tena mama anadiriki kwenda kulala chumba cha watoto au cha wageni ili tu asiwe karibu na mume wake kwasababu amemnunia,jamani huko sio kujenga bali ni kubomoa nyumba yenu wenyewe. muhimu kubembelezana na kuzungumza pamoja ili kutatua tatizo na si kuongeza matatizo...... |
Alhamisi, Septemba 23, 2010
Mwenzio akiwa amenuna au kukasirika na wewe ukanyamaza kimya na kununa pia,,ni hatari sana katika mahusiano
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Maoni 2 :
....inategemea na hali ilivo na nani anaweza kufunguka kwenye maongezi na yakawa ya maana badala ya kuongeza matatizo!
Adela unafaa kweli kuwa na hiyo fani kwani mambo yako yanafana sana.Endelea kutupa vionjo mama.
Chapisha Maoni