Kuna baadhi ya vijana ambao wanatamani kuingia katika ndoa lakini kuna baadhi ambao wanasema kwamba ,,bado nipo nipo kwanza,, na hii ni kwa wanaume na wanawake,,katika uchunguzi wangu nimeona kwamba vijana wengi wanachelewa kuoa au kuolewa kutokana na kuogopa majukumu kwani anaona bado hajajipanga vizuri, wengine ni kushindwa kujiamini anaogopa kuingia kwenye ndoa kwa hofu ya kukosa uhuru anaoutaka katika mambo yake ya starehe,,
Wengine kutokana na kulazimishwa na wazazi kuoa au kuolewa na wachumba watakaowachagua wao na kikubwa pia ni hali duni ya maisha kwani kuna mwingine anatamani kuoa lakini anaona kipato chake ni kidogo kufanya hivyo.
Jamani mapenzi ni zaidi ya kipato ulichonacho kwani unaweza kuamua kuingia kwenye ndoa na huku mkiwa katika hali duni ya maisha,,baadae mkafanikiwa kwa juhudi zenu binafsi na kwa ushirikiano kati ya mke na mume muhimu ni kujiamini na kujitambua.....
Maoni 5 :
Me nadhani kwamba ukioa katika umri wa kijana unakuwa kama unajidanganya kwa sababu ile hali ya kutamani tamani inakuwa ndo inaanza sasa ukioa utatamani utoke nje ili ukajue ladha ya nje si ndo mwanzo wa kupeleka magonjwa ndani ya nyumba na kusababisha ugomvi na mwenzio. Kama mtu anataka kuoa ama kuolewa aweke tamaa zote nje ili akiingia ndani awe safi. by Pipo
maisha magumu na tamaa pia huchangia vijana kchelewa kuoa na kuolewa by ARON john
napenda mada zako miss upo on fire sana....unajua suala la kuoa ama kuolewa ni suala moja nyeti sana adela na ya kupasa kujipanga vilivo,kwani ukishakiri kuoa ama kuolewa maana yake...upo teyari kuachana na yote ya ulimwengu na kiridhika na yule uliye naye...shida iwapatayo vijana wengi mpaka kuchelewa kuoa ama kuolewa nafikiri ni bashasha zipatikanazo nje ya ndoa kwa lugha nyingine tunaita ANASA...dunia tuliyonayo sasa si kama ile ya zamani kwani wazee wetu waliweza kuyakabili hayo ila si kwa dunia hii ya leo!!!....nafikiri kuna kila sababu ya vijana kubadilika kwani kuchelewa kuingia katika ndoa yaweza leta madhara makubwa sana kwani ukaribisha magonjwa kwa vijana na ivo kupoteza nguvu kazi ya taifa...yatupasa kubadilika sasa!!!!by MWAKA T!!!!!
asanteni sana Pipo,,Aron John na Mwaka T tuko pamoja kiukweli ndoa ni mipango na kikubwa zaidi ni maelewano,,ila muhimu kuwa na uhakika na kile unachokifanya...
NI KWELI UNAWEZA UKAWA UMEFIKAI UMRI WA KUOLEWA AU KUOWA,NA IKAWA NGUMU SANA KOZ MWANAUME NDIO ANAKWAMBIA NATAKA KUOWA SI MWANAMKE ATAKWAMBIA NATAKA KUOWA.NDIO KAMA UNAVYOSEMA NDOA NI MAELEWANO,WAPO WATU WANAPATA WANAUME AU WANAWAKE WAZURI NA HAWAJUI NA KUMBE WAO BADO WANATAKA MAMBO YA UJANA NA UTOTO,WA KUNYWA POMBE SANA,OUTING SANA,MARAFIKI SANA,ME NILIKUWA NA BOYFRIEND NILIJUA NIKIWA NAMUELEZA UKWELI KUWA HIKI SI KIZURI,ATANIELEWA KUMBE MWENZANGU ALIKUWA ANAPASS TIME TU,ANAPENDA POMBE NA NI MKUBWA YUPO NA 35 YRS ILA ANAISHI KWAO.NAMWAMBIA HAMA KWENU HATAKI,ACHA POMBE SIWEZI KUACHA KIRAHISI NAMNA HIYO ANASEMA,NIKIMWAMBIA ME NAUMWA NAENDA HOSPITAL ANAJIBU HAYA, HAJUI KAMA YY NI WAJIBU WAKE PIA KUWA KARIBU NA ME KWA HALI YOYOTE,NIKIWA KAMA NIMEKWAMA KIFEDHA NIKIMWAMBIA DEAR NAOMBA PESA KIDOGO NIMEKWAMA,HUNIJIBU SINA, SAWA WOTE TUNAFANYA KAZI ILA YY ME NIKIWA NACHO NAMNUNULIA KITU CHOCHOTE NACHOONA KINAMPENDEZA MWENZANGU YEYE CHAKE KUSHARE NA MIE HATAKI SASA JMN HUYO NI MPENZI,ANATAKA MM NDIO NIMLEE,KOZ HISTORIA YAKE ALIKUWA ANALELEWA NA WADADA,SASA MTU KAMA HUYU UTASEMA NI MVUMILIE KWELI?
Chapisha Maoni