Kuna mambo mengi sana yanayosababisha wapendanao kushindwa kuwa na uhusiano wa kudumu kwanza kabisa leo tutaangalia hali ya kulipiza kisasi ikiwa ni moja kati ya chanzo cha wapendanao kushindwa kudumu katika uhusiano:
-Katika kulipiza kisasi hali hii huwa inatokea pale ambapo mwanaume au mwanamke anakuwa ameumizwa na mpenzi wake na kutokana na hasira anafikiria njia sahihi ni kulipiza kisasi.
-kulipiza kisasi haiwezi kuwa njia sahihi ya kumaliza matatizo ila inaongeza matatizo kwani inawezekana mkawa mnaendelea na huo mchezo kila mmoja anapokosea basi mnaona njia ni kulipiza kisasi na mwisho wake unakuwa mbaya.kwani itakuwa kama mchezo kwamba niumize nami nikuumize na hatimye kinachofuata ni kutengana kutokana nakuona mmeshindwana.
-Kulipiza kisasi haiwezi kuwa ni tabia ya mtu kwani ni kitu ambacho unaweza kujizuia pale ambapo unahisi mwenzio kakufanyia ubaya kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kukaa na kutulia ili kuweza kutatua tatizo katika hali ya ustaarabu ambapo ni pamoja na kutafakari tatizo lililotokea na tumia njia sahihi ya mazungumzo baina ya wewe na mwenza wako ili kuyamaliza.
- mfano: umegundua mwenzako ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke au mwanaume mwingine njia sahihi kwanza unatakiwa kuchunguza je ni kweli au ni maneno ya watu,pia unaweza kufanya mazungumzo na mwenzako ili kuweza kupata uhakika wa jambo lenyewe, lakini kutokana na hasira walio wengi huwa hawafanyi hivi wengi wao ndio hutumia njia kama kulipiza kisasi au kupigana na hatma yake ni kutengana tunatakiwa kufahamu kwamba katika mahusiano mazungumzo ni ya muhimu sana baina ya wapendanao katika matatizo na wakati wote hata pasipo na matatizo,unapoona mwenzako ana matatizo basi mkalishe kitako na kuzungumza naye,kwani kuna wengine wanakosea lakini hawajui kama wamekosea.
-Na pia kumbuka lengo kubwa la kuwepo na mazungumzo baina ya wapendanao nikuondoa hisia mbaya na maumivu yaliyojitokeza katika uhusiano na baada ya mazungumzo kila kitu kinasahauliwa na kusameheana, kwani vitu kama matusi,hasira na uamuzi wa ghafla siku zote ndio chanzo cha kuharibu na kuvunja uhusiano baina ya wapendanao.......tuwe makini tujenge uhusiano wa kudumu jiulize je,,utaacha au utaachika mpaka lini...yote yanawezekana mapenzi hadi uzeeni.......
Maoni 1 :
Hongera my sister kuandika maada inayoelimisha
jamii
Chapisha Maoni