Katika mapenzi inapotokea ugomvi baina ya wapendanao kila mtu huwa na mamuzi yake kuna mwingine ataamua kumuacha mwenzake kutokana na kushindwa kuvumilia mabaya anayofanyiwa,lakini pia katika mapenzi uvumilivu ni nguzo muhimu sana kwani yanapotokea matatizo usichukue uamuzi wa haraka,kwamba unaona bora tuachane lakini huku ukijua kabisa bado unampenda na wakati mwingine unakuta matatizo yaliyotokea yanaweza kurekebishwa,kuwa makini katika hili
|
Kuwa makini sana usije ukaamua kumuacha mpenzi wako huku bado unampenda tena kwa mambo ambayo mngeweza kukaa na kuyamaliza,kwani kuna wengine wanaachana halafu baadae mwenzie akishapata mchumba mwingine anaanza kumfuata au kumtumia ujumbe kwamba siwezi kuacha kukupenda,,mara ooh nimekumis nakupenda na wakati huo inakuwa ni too late...be care jamani |
Maoni 3 :
Hapa umesema kweli wangu, yaani kuna watu wa aina kama hii, kama umekerana na mwenzio usiwe mwepesi wa kuchukuwa maamuzi hasi, coz baadae utajikuta unajiumiza roho, coz utakuta mwenzio amepata mwengine, nawewe ilihali ulikuwa unampenda bado, utakuwa unaishia kujiumiza moyo!!!
asante Hashir tuko pamoja unajua watu wanachukua maamuzi ya haraka kutokana na hasira lakini baadae ndio anajuta cha muhimu ni kuzi control hasira ili kuepukana na uamuzi usio sahihi
Maamuzi ya haraka hara karibu katika kila kitu si mazuri hasa kama unayafanya ukiwa na hasira!:-(
Chapisha Maoni